Kupigwa billioni 75 ni ujinga au upumbavu? Tutaendelea kukubali kufanywa kichwa cha mwendawazimu hadi lini?

Shida sio katiba tusitoane ufahamu shida inaanzia kwenye bongo zetu.
Ubongo wetu umefanyaje ? Rais anateua watu wake watakaomsaidia kushind next electioo basi sasa utasemaje shida sio katiba, wateule wote wako obligated kumsikiliza mkuu kwa lolote analosema akipinga anatolewa kwenye nafasi hata kama alichokipinga kina maslai kwa taifa, mkuu hapa everything is connected to everything tuanze kwenye the root cause sio huku juu juu, unampaje mtu kazi kisa tu ni mkwe wako ? Ujinga ni mwingi masta
 
Mikataba yote ya hovyo imepitishwa na serikali ya CCM na imevunjwa na serikali ya CCM
Na walio shindwa mahakama ni serikali ya CCM
Baada ya kuuza maeneo karibia yote ya madini kuna siku tunasikia Serengeti na ngorongoro pia zimeuzwa

Watanzania kwakuwa tumekubali kutawaliwa na watu wajinga tuwe wavumilivu.
 
Huo ni ujinga na upumbavu wa chama chako cha kijani usikatie Kona mbali, kwa sababu wao ndio wahusika wa huo ujuha uliofanyika, kuanzia kuingia mikataba ya kipumbavu na wizi hadi kuivunja kiholela
 
PM again at his best with the same lengthy, old, classic, familiar, bizarre Tanzanian narrative. Anyway tunashukuru kwa kutiririka tena kuhusu “maajabu” tuliyoyazoea ya nchi hii.

Jibu kama sisi ni wajinga au wapumba wanalo mashabiki wa kejeli ya “tutashitakiwa MIGA”; “mzalendo wa kusimamia rasilimali za nchi”; “Chiba”, etc.

Rais mmoja wa CCM anaingia mikataba ya kifisadi ya kuhujumu nchi. Anashangiliwa kwa shangwe zote kama mkombozi wa nchi kiuchumi. Rais wa CCM anayefuatia anavunja hiyo mikataba na kubadilisha sheria zinazohusika. Anashangiliwa kweli kweli kama mkombozi wa nchi kwa kulinda rasilimali. Halafu nchi ikibanwa kwenye mahakama za kimataifa analipa madai kisirisiri na kulalamikia “wasaliti”. Rais wa CCM anayefuatia analipa kiroho safi na kwa uwazi madai yote yanayojitokeza kutokana na madhambi ya waliomtangulia. Hakuna maelezo yanayotolewa kwa wananchi wala hakuna anayewajibishwa.

What a charade!

Ujinga na upumba ni wa kudumu hadi siku uchawa kwa magenge ya viongozi wa CCM utakapokoma na kura za wananchi kuheshimiwa kwenye chaguzi zetu. Kama nguvu ya wananchi kuweka viongozi madarakani na kuwawajibisha haipo nchi itaendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu.
Well said CCM NDIO TATIZOO
 
Nashukuru leo umeandika kama Paschal Mayalla, kimsingi hizi ni dili za Mkwere, hii kesi haikuwepo imefufuliwa mwezi wa 7 2023 September 2023 malipo yakafanyika sijui kwa budget ipi? Ukisikia wateule wanamsifia sn maza kupita MUNGU wao sababu ni dili kama hizi, mara awe Mama wa Taifa sijui Dkt huku nchi ipo gizani, hakuna maji petrol shida, majibu ni haya. Tuacheni uchawa tusimame na nchi yetu
Huyu babu wa Msoga tutamwambia Mungu amrudishe kwake na akamchome moto wa kutosha!
 
Ubongo wetu umefanyaje ? Rais anateua watu wake watakaomsaidia kushind next electioo basi sasa utasemaje shida sio katiba, wateule wote wako obligated kumsikiliza mkuu kwa lolote analosema akipinga anatolewa kwenye nafasi hata kama alichokipinga kina maslai kwa taifa, mkuu hapa everything is connected to everything tuanze kwenye the root cause sio huku juu juu, unampaje mtu kazi kisa tu ni mkwe wako ? Ujinga ni mwingi masta
Utaongea yoote ila mkuu shida inaanzia kwenye bongo zetu.

Kwani hata katiba iliyopo tuu hatujawahi kuifanyia kazi .
 
Nashukuru leo umeandika kama Paschal Mayalla, kimsingi hizi ni dili za Mkwere, hii kesi haikuwepo imefufuliwa mwezi wa 7 2023 September 2023 malipo yakafanyika sijui kwa budget ipi? Ukisikia wateule wanamsifia sn maza kupita MUNGU wao sababu ni dili kama hizi, mara awe Mama wa Taifa sijui Dkt huku nchi ipo gizani, hakuna maji petrol shida, majibu ni haya. Tuacheni uchawa tusimame na nchi yetu
Mungu anawaona wote wanaohusika !
Kama ipo hujuma kwa Nchi basi KARMA itamlipa kila anayehusika kwa wakati muafaka !🙏🙏🙏
 
Lissu aliwaonya watu wa Serikali namna bora ya ku-deal ya hii mikataba badala ya kupokonya leseni, Mzee mmoja mjanja akapokonya leseni zote halali za wachimbaji hasa wakubwa akakaa nazo ofisini kwake, wengine wakavumilia wakaondoka ila wengine wakafungua kesi. Sasa kesi hii si ya mwisho na zingine zinakuja, wacha tulipe.

Dawa ya deni ni kulipa, tena unalipa na fidia juu. kuliwa tunajitakia wenyewe kwa kutofuata sheria. Hata kama ukiwa mtu mwenye mamlaka yote katika nchi huwezi kuamka asubuhi unapokonya watu leseni zao ambazo wamezipata kwa kufuata sheria za nchi.

CCM -oyeee,
Uchaguzi 2025 oyeeee - Asanteni kwa kunisikiliza.
 
Tujisahihishe kama ambavyo amewahi kuandika baba wa Taifa ili tusirudie makosa ambayo yatakuwa yanatugharimu kama Taifa.
Kwani hakuna idadi ya juu kabisa ya kujisahihisha halafu tukasema basi? Au ni saba mara sabini? Nisiambiwe hapo nimechanganya siasa na dini!!

Ukweli ni huu - imeshaonekana wazi hata tunapopigwa hakuna anayeadhibiwa, watu wetu wenyewe wameweka mikataba yenye masharti dhaifu ili kutengeneza mazingira ya kupigwa huku wakigawana na wapigaji. Hata nikiuliza tu kwa upole, kuna majina yoyote ya watu waliodhibiwa kuanzia mapigo ya makinikia, ndege kukamatwa, mabarabara na kadhalika?? Tunaendeleaje "kujisahihisha" kwa namna ili ile kila mara halafu tutegemee matokeo tofauti?
 
Nani alaumiwe mkuu kama sio ccm. Mmoja apokee wawekezaji mwingine aje wafukuza. Unategemea nini?
Mimi nafikiri tujilaumu sisi watanganyika kwa kushindwa kupigania Katiba mpya ya nchi. Kwa katiba hii hakuna jipya lolote tunalolitegea katika nchi yetu, watu ni walewale, style ya kutawala ni ile ile - kuna kitu hapo.

Bila katiba mpya, hatutoboi.
 
Nchi yenye watu wanaojiframe kwenye kushtakiwa ili wale Cha juu toka kwa mgeni.
Hivi hakuna namna mkaanza kuwalambisha udongo Mmoja Mmoja ?.
 
Kilio chetu ni kwa alie pitisha mkataba huu mpaka wazalendo wakauvunja.
Unadhani akija Rais mzalendo mkataba wa DP world nini kitatokea, hawezi kuvumilia huo uchafu Bora kulipa Tu.
 
Mimi nafikiri tujilaumu sisi watanganyika kwa kushindwa kupigania Katiba mpya ya nchi. Kwa katiba hii hakuna jipya lolote tunalolitegea katika nchi yetu, watu ni walewale, style ya kutawala ni ile ile - kuna kitu hapo.

Bila katiba mpya, hatutoboi.
Tena kwa dharau wanaita "kajitabu"
 
Back
Top Bottom