Kupendwa au kuogopwa, bora nini?

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,889
Msikilize Nicolo machiaveli anavyosema ndani ya The Prince.

SURA YA 17

Kuhusu ukatili, rehema na iwapo ni bora kupendwa kuliko kuogopwa

Kwa kuangalia sifa nilizozitaja hapo juu, nasisitiza kuwa, kila kiongozi anatakiwa ajitahidi asifike kwa rehema na si ukatili. Lakini anatakiwa kuwa makini ili watu wasije kutumia sifa yake hiyo vibaya. Cesare Borgia alikuwa na sifa ya ukatili, lakini ukatili wake uliweza kuisimamisha na kuiunganisha Romagna, pia aliifanya kuwa na amani na utulivu

Kwahiyo basi, iwapo tutaangalia vitu kwa uhalisia wake tutaona kuwa alikuwa na rehema kuliko watu wa Florence, watu ambao ili kuepuka kuonekana ni wakatili walivumilia kuanguka na kusambaratishwa kwa Pistoja na makundi hasimu.

Kiongozi anatakiwa kutojali ikiwa ataonwa katili iwapo hilo linamuwezesha kuunganisha watu wake na kuwafanya kuwa watiifu na watulivu. Mwisho wa siku yule anayezimisha machafuko ndiye ataonekana ni mwenye rehema kuliko yule ambaye anaruhusu mambo yaendelee hadi kusababisha uharibifu wa mali na umwagaji wa damu. Jambo hili huathiri taifa zima wakati ukatili huathiri watu wachache tu.

Na zaidi ya yote ni kuwa, ni vigumu kwa kiongozi mpya kuepuka sifa ya kuonekana katili, sababu ni kuwa taifa(au uongozi) jipya huwa na hatari nyingi sana.

Hata hivyo, kiongozi mpya hatakiwi kuwa mtu wa kwanza kuzua taharuki, bali anatakiwa..........ili kuamini watu kupita kiasi kusijemuweka hatarini na kushuku kusiko na msingi kusije fanya watu wakaacha kumuunga mkono.

Na hapa linakuja swali, je, kupendwa ni bora kuliko kuogopwa au kuogopwa ni bora kuliko kupendwa? Linaweza jibiwa kwamba; binadamu tungependelea kuogopwa na kupendwa kwa wakati mmoja, lakini kwa sababu ni vigumu kwa uoga na upendo kukaa pamoja, hivyo tukiamua kuchagua , ni bora sana kuogopwa kuliko kupendwa.

Inajulikana wazi kwamba binadamu ni viumbe wasio na shukrani, wenye kubadilika, wenye hila, wenye pupa/walafi, wanakuunga mkono wakiwa wanapata faida tu, na kama nilivyosema huko nyuma; wakati wa amani watakuwa tayari kujitolea maisha yao, ya watoto wao na mali zao kwaajili yako, lakini wakati wa taaabu watakugeuka. Kiongozi ambaye hajiimarishi na kuwategemea ataangushwa. Urafiki wako nao si kwa sababu ya upendo wao kwako au uaminifu wao bali ni kwa sababu ya maslahi. Hawawezi kuwa washikamanifu siju zote, badala yake wao hutufelisha pale tunapowahitaji sana.

Pia, watu hawajali na ni rahisi kumkosea mtu anayetafuta kupendwa kuliko yule anayetafuta kuogopwa. Upendo hushikiliwa uaminifu na kutendeana wema, lakini kwa sababu binadamu ni viumbe wasio wakamilifu, huvunja mambo hayo pale mtu anapoona anaweza pata maslahi binafsi, lakini uoga huundwa na wasiwasi juu ya adhabu na hii haifeli katika kunyoosha mtu.

Hata hivyo, kiongozi anatakiwa kufanya aogopwe kwa namna ambayo hata kama haitafanya watu wake wampenda, lakini itafanya wasimchukie.

Inawezekana kabisa kwa mtu kuogopa bila kuchukiwa, na hili linawezekana iwapo atajiepusha na mali za raia wake na wake zao. Na ikitokea akalazimika kumuua mtu, anatakiwa kufanya hivyo pale tu anapokuwa na sababu nzuri. Lakini kikubwa zaidi ni kujiepusha na mali za wananchi wake. Ni rahisi kwa mtu kusahau kifo cha baba yake kuliko kusahau kupotea kwa urithi alioachiwa naye. Haitakiwi kutafutiza visababu vya kutaifisha mali za watu wako na yule anayeanza kuishi kwa kutaifisha mali, kila siku atakuwa anatafuta sababu za kufanya hivyo lakini sababu za kuua watu ni chache na baada ya muda zinakuwa hazipo kabisa.

Lakini kiongozi anapokuwa na jeshi lake, akiongoza jeshi kubwa anatakiwa kutojali kuonekana katili. Bila ya kiongozi kuwa na sifa hiyo, hakuna jeshi analoweza kuliyoosha na kulisimamia vizuri. Pamoja na kuwa na sifa zingine, Hannibal alisifika kwa sifa hii. Hasa kwa kuwa alikuwa na jeshi kubwa sana, jeshi lililoundwa na watu wa mataifa mbalimbali. Hakuna uasi uliotokea na hawakufanya uhaini kwa kiongozi wao iwe wakati wa amani au wa taabu. Hili tunaweza kulihusisha na ukatili uliopita kiasi. Huo, pamoja na uhodari wake, vilimuwezesha kuheshimika na kuogopwa machoni pa wanajeshi wake. Bila ukatili, sifa zingine zisingemletea mafanikio aliyoyapata.

Waandishi wasioona mbali Wanasifia mafanikio yake lakini wanashutumu sifa kuu iliyowezesha yapatikane. Sifa zake nyingine zisingemfanya awe hodari kama alivyokuwa. Tunaweza kuona hilo kwa kumuangalia Scipio, mmoja kati ya makamanda hodari, si tu kwa wakati wake bali katika historia nzima. Jeshi lake lilipomuasi huko Hispania, sababu haikuwa nyingine bali huruma zake za kupita kiasi. Aliwapa uhuru uliopitiliza wanajeshi wake, kitu ambacho hakiendani na nidhamu ya jeshi. Hilo pia ndilo lililomdhoifisha Fabius maximus hadi kufikia kuitwa mharibifu wa Roma na bunge. Aliambiwa kuwa

'Kuna wengi ambao wanajua sana kujizuia kufanya makosa kuliko jinsi ya kuwarekebisha wengine wanapokosea.' Tabia hii baada ya muda huharibu sifa hata za mtu kama Scipio iwapo angeiendeleza, na angeendelea kuwa kamanda. Lakini kwa sababu alikuwa chini ya bunge, sifa hii yenye madhara haikuonekana, na baadaye ikawa inaonekana kama ni ya maana.

Tukirudi kwenye swali kuhusu kupendwa na kuogopwa, nihitimishe kwa kusema; sababu kupendwa kwa kiongozi kunategemea wananchi wake, na kuogopwa kunategemea mwenendo wake, kiongozi mwenye busara anatakiwa kuwa makini na kuimarisha mwenendo wake na si kutegemea maoni ya wengine. Lakini kama nilivyosema, anatakiwa kufanya yote anayoweza kuepuka kuchukiwa.
 
Back
Top Bottom