Kupanda kwa nauli za mwendokasi: Mkakati wa kuboresha sekta ya usafirishaji wa umma utakaoleta matokeo mazuri katika usimamizi na uendeshaji wa mradi

FPT

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
1,201
1,839
Kufuatia Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) kumtangaza bei mpya za nauli, nimeona mtazamo wa baadhi ya watu ukiwa kulekule vitu vinapanda bei sana.

Kufuatia mtazamo wa namna hiyo nami nitachangia machache juu ya faida za kupanda kwa nauli za usafiri huo husasani katika suala zima la uendeshaji na usimamizi wa mradi.

Mradi huu ni msaada mkubwa katika usafirishaji katika mkoa wa Dar es salaam. Umepunguza adha ya usafiri kwa kiwango kikubwa.

Tukirudi kwenye historia ya mradi, mradi huu umeanza kufanya kazi rasmi mwaka 2016 na mpaka kufikia mwaka huu wa 2023 mradi umetimiza miaka 7 ya uendeshaji wake.

Tofauti na miradi mingine katika sekta ya usafirisha kwa kampuni binafsi ,mradi wa mwendokasi ni wenye uwekezaji mkubwa na kiasi kikubwa Cha uwekezaji huo ni mikopo ambayo haina budi kurejeshwa hivyo unahitajika usimamizi na uendeshaji mzuri.

Moja ya vitu vinavyoangaliwa sana kwenye usimamizi na uendeshaji wa miradi ni gharama. Na kwa kuwa mradi huu unategemea nauli ili kukidhi gharama hivyo kupanda kwa nauli hakuepukiki.

Kama nilivyosema mradi huu ni mkubwa ,unahusisha wafanyakazi wengi na kama mpaka sasa mradi una miaka 7 hivyo magari na miundombinu mingine ya mradi imeanza kuchoka na kuchakaa na hivyo panahitajika ukarabati mkubwa. Pia, wafanyakazi wa mradi wanahitaji ongezeko la mishahara na mambo mengine.

Pia, kama Return On Investment sio ya kiwango kikubwa kiasi Cha kugharamia mradi na kurejesha mkopo basi suala la kupanda kwa hakuepukiki.

Kupanda kwa gharama za nauli za mwendokasi ni kwa lengo la kutengeneza matokeo mazuri mazuri zaidi kwenye usimamizi na uendeshaji wa mradi.

Nitoe wito na rai, tuwaepuke wale wote wenye nia ovu ambao kwa kujua wanaamua kupotosha juu ya kupanda kwa nauli huku.
 
Hoja yako yooote imejaa upotofu wa mantiki.

Mradi hauna unafuu wowote kwa wananchi sana sana ni sehemu ya wakubwa kula
 
Hivi huu uharo wote unautoa uko kichwani kwako au? Shilingi 100 inaboresha nn,?pumbaf
Usiiangalie shillingi 100 kutoka kwako pekee angali mia mia za watu wote wanaotumia mradi husika
 
10% zipo nyingi na kwa Mamamba wengi ndio maana huo mradi unachechemea watu wamepewa bara bara yao haina ushindani ni kubeba abiria na kushusha lakini wanaferi wenzao abiria wanagombaniana na Tochi za kumwaga bara barani pamoja na fine ila wanafauru huo mradi utakua hivyo hivyo na tabia zake za UDA miaka nenda miaka rudi...
 
Wizi ni tatizo kwenye huduma Zinazotolewa zikishirikiana na serikali.

Basi la Mwendo Kasi halifuati SHERIA ya Usalama Barabarani . Hawalipi ushuru kwenye standi , wanajaza abiria kama soko la Kariakoo na Mwendo hauna vibao vya 50 lakini Bado wanasuasua .

Waruhusu Wawekezaji wengine waweke mabasi yao ili usafiri wa Jiji ubaki kama huduma .
 
Kwa idadi ile wanayojaza abiria tokea asubuhi mpaka usiku harafu wanakwambia shirika halifanyi vizuri kama sio wizi ni nini nilishangaa Waziri Mkuu alivamia mara moja tuu pale Jangwani kama vile Shirika limetoka China kumbe kila kitu ni wa hapa hapa..wakileta bus wanasua sua kulipa kodi mpaka wapate msamaha sasa sijui hiyo hasara wanaipata wapi?
 
Mleta mada umeleta upuuzi wa ajabu kabisa ni bora ungekaa kimya tu!
1. Huduma zenu ni mbovu kupindukia (bora hata daladala)
2. Abiria wanajazana hadi kukaribia kuzimia kwa kukossa hewa!
3. Abiria kukaa vituoni (hadi kwa saa nzima) bila kupata usafiri, ni aibu sana sana!
4. Lugha chafu za wakata tiketi wenu (hasa pale kituo cha Kimara)

Pongezi pekee

vIjana wenu wa ulinzi (hasa pale Kimara mwisho na Kituo cha kivukoni) wameanza kusimamia kwa ukamilifu kuingia kwenye mabasi mabasi kwa foleni. HAWA NAWAPA KONGOLE SANA SANA
 
Nini faida ya Usafiri Bora kwa Jamii ?

Pili unajua kitu kinaitwa Economy of Scale ?
 
Kufuatia Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) kumtangaza bei mpya za nauli, nimeona mtazamo wa baadhi ya watu ukiwa kulekule vitu vinapanda bei sana.

Kufuatia mtazamo wa namna hiyo nami nitachangia machache juu ya faida za kupanda kwa nauli za usafiri huo husasani katika suala zima la uendeshaji na usimamizi wa mradi.

Mradi huu ni msaada mkubwa katika usafirishaji katika mkoa wa Dar es salaam. Umepunguza adha ya usafiri kwa kiwango kikubwa.

Tukirudi kwenye historia ya mradi, mradi huu umeanza kufanya kazi rasmi mwaka 2016 na mpaka kufikia mwaka huu wa 2023 mradi umetimiza miaka 7 ya uendeshaji wake.

Tofauti na miradi mingine katika sekta ya usafirisha kwa kampuni binafsi ,mradi wa mwendokasi ni wenye uwekezaji mkubwa na kiasi kikubwa Cha uwekezaji huo ni mikopo ambayo haina budi kurejeshwa hivyo unahitajika usimamizi na uendeshaji mzuri.

Moja ya vitu vinavyoangaliwa sana kwenye usimamizi na uendeshaji wa miradi ni gharama. Na kwa kuwa mradi huu unategemea nauli ili kukidhi gharama hivyo kupanda kwa nauli hakuepukiki.

Kama nilivyosema mradi huu ni mkubwa ,unahusisha wafanyakazi wengi na kama mpaka sasa mradi una miaka 7 hivyo magari na miundombinu mingine ya mradi imeanza kuchoka na kuchakaa na hivyo panahitajika ukarabati mkubwa. Pia, wafanyakazi wa mradi wanahitaji ongezeko la mishahara na mambo mengine.

Pia, kama Return On Investment sio ya kiwango kikubwa kiasi Cha kugharamia mradi na kurejesha mkopo basi suala la kupanda kwa hakuepukiki.

Kupanda kwa gharama za nauli za mwendokasi ni kwa lengo la kutengeneza matokeo mazuri mazuri zaidi kwenye usimamizi na uendeshaji wa mradi.

Nitoe wito na rai, tuwaepuke wale wote wenye nia ovu ambao kwa kujua wanaamua kupotosha juu ya kupanda kwa nauli huku.
Umeongea general, hujaweka hoja za kimantiki kutetea unachosema.

Ni kwa namna gani 650 haitoshi? Wao barabarani hawapati usumbufu wowote ule
 
Soma mpaka mwisho nimesema kwa undani.
 
Mleta mada umeleta upuuzi wa ajabu kabisa ni bora ungekaa kimya tu!
1. Huduma zenu ni mbovu kupindukia (bora hata daladala)
2. Abiria wanajazana hadi kukaribia kuzimia kwa kukossa hewa!
3. Abiria kukaa vituoni (hadi kwa saa nzima) bila kupata usafiri, ni aibu sana sana!
4. Lugha chafu za wakata tiketi wenu (hasa pale kituo cha Kimara)

Pongezi pekee

vIjana wenu wa ulinzi (hasa pale Kimara mwisho na Kituo cha kivukoni) wameanza kusimamia kwa ukamilifu kuingia kwenye mabasi mabasi kwa foleni. HAWA NAWAPA KONGOLE SANA SANA
Ndio maana nauli zinatakiwa zipande ili kuboresha usimamizi na uendeshaji wa mradi
 
Wizi ni tatizo kwenye huduma Zinazotolewa zikishirikiana na serikali.

Basi la Mwendo Kasi halifuati SHERIA ya Usalama Barabarani . Hawalipi ushuru kwenye standi , wanajaza abiria kama soko la Kariakoo na Mwendo hauna vibao vya 50 lakini Bado wanasuasua .

Waruhusu Wawekezaji wengine waweke mabasi yao ili usafiri wa Jiji ubaki kama huduma .
Hujui unachokitamani
 
Nilipomaliza kusoma nilijua ni mkuu wa wilaya ndiye kaandika, maana hapo mwisho sasa eti "nitoe wito ..."

Shubamit!.
 
Watalam wa IT mnajionaje? mwendokasi wanarudi nyuma kila leo,kivipi?wakati mradi unaanza yale maneno ya basi linaenda wapi yalikuwa digital na kila kituo kinachofuata kinatajwa sasa baada ya kuachiwa tumeanza kubandika vibao vya mbao vimeandikwa kwa mkaa.
 
Bongo nyoso,
 
Back
Top Bottom