Yapi ni matarjio yako kuhusu mradi wa SGR? Haya ni matarajio yangu!

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,211
42,072
Baada ya kuona uzinduzi wa treni ya kisasa leo na ikitarajiwa kuanza safari za Dar-Morogoro ni ukweli usiopingika watu wanajua kabisa ni mradi mzuri lakini kila mtu hana imani na wasimamizi wa mradi huu Tanzania Railways Corp na hii imetokana tuncho kishuhudia kwenye mwendokasi na ni wazi taasisi za serikali zimefeli kabisa kuendesha mira na miradi mingi inakufa kwenye mikono yao na kodi zetu zinachezewa sana!

Mimi binafsi nina matarajio yangu kwenye huu mradi bila shaka kila mtu ana matarajio yake!
Haya ndio matarajio yangu!

1. Sitarajii kusikia kuwa nauli za treni hii ni kubwa kuliko za kusafiri na basi hata kama watu wanafika haraka kwani hapo ndio mradi utakapo anza kufia!

2. Sitarajii kusikia kuona nauli zinakusanywa kwa mfumo wa kizamani yani mkononi na bila tiketi kuscaniwa!

3. Natarajia kuona serikali inatafuta kampuni itakyofanya kazi ya kukatisha ticketi na kuchukua nauli kisasa maana serikali haiwezi kukusanya na kuendesha hili shirika kwenye kila jambo!

3. Sitarajii kusikia kuwa mashine za ku scan ticketi hazifanyi kazi kisa mtandao na ticketi haziscaniwi ...tunayaona kwenye mwendokasi!

4. Sitarajii station na treni hizi kutumika kama kichaka cha vibaka na walanguzi hivyo swala la usalama tunatarajia wamejipanga kwenye hili mwendokasi nawapongeza!

5. Sitarajii treni ya abiria kama SGR kutumika kusafirisha mizigo ambayo abiria awezi beba au kuwekwa kwenye carier.....

6.Sitarajii kuona station na treni hii inageuzwa kama soko la kufanyia biashara kwa kuruhusu wamachinga na wale waonao jiita wachungaji kuanza kuchafua stand na treni hiyo hivyo lazima haya mambo yapigwe marufuku mapema!

7. Sitarajii kuona treni hii na maeneo ya treni hii kukosekana wahudumu wenye kujali wateja na kazi yao kwani vijana wapo wengi sana mtaani

8. Sitarajii kusikia treni hii haina watoa huduma waliopewa vibali vya kutoa huduma ya chakula na vinywaji kwa utaratibu mzuri sitarajii kusikia watu wanafanya biashara ya umachinga kwenye miundombinu hii inayovutia!

9. Sitarajii kusikia tren hii imeshindwa kwenda kutokana na kukosekana kwa UMEME AU MAFUTA ni vyema umeme wa treni hii ukajitegemea na ukawa haukatiki maana mwanzo tuliambiwa itakuwa na umeme wa peke yake...

10. Sitarajii kusikia mradi huu unatumiwa kisiasa kuanza kusafirisha makada bure hii ndio itauwa kabisa huu mradi maana tunayaona kwenye ndege za AIR TANZANIA

Mimi ni hayo tuuu.. mengine mtaongezea wenzangu! Mnamatarajio gani kutoka kwenye huu mradi?

Wasalaam
 
Naona huu mradi hautafika mbali kutokna na wanasiasa wengi kuwa na mabasi yao binafsi ..lazima watahujum ili gar zao zipige kazi huu mrad una maadui wengi sanaa
 
Back
Top Bottom