Jatropha
JF-Expert Member
- Apr 9, 2009
- 1,151
- 199
Ndugu WaJF taarifa kutoka mtaani zinaonyesha kuwa bei za bidhaa mbali mbali zimepanda maradufu mara tu baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010; Kama tutakavyokumbuka suala hili la mfumko wa bei ilikuwa ni moja ya ajenda kuu za CHADEMA katika uchuguzi huu.
Habari zinaonyesha kuwa saruji imepanda kutoka Shs 12,500/ kufikia 15,000/= hapa mjini, ndoo ndogo ya mafyta ya kula imepanda kutoka Shs 16,000/= hadi Shs 24,000/= n.k
Wakati natoa wito kwa wabunge wa CHADEMA kuanza kuisurubu Serikali kwa hali hii, naomba wanaJF wenye taaluma ya kiuchumi watusaidie nini chanzo cha hali hii kutokea tena kwa kiwango kikubwa kiasi hiki?