Kupanda kwa ghafla kwa bei za bidhaa mbali mbali baada ya uchaguzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kupanda kwa ghafla kwa bei za bidhaa mbali mbali baada ya uchaguzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jatropha, Nov 15, 2010.

 1. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #1
  Nov 15, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Ndugu WaJF taarifa kutoka mtaani zinaonyesha kuwa bei za bidhaa mbali mbali zimepanda maradufu mara tu baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010; Kama tutakavyokumbuka suala hili la mfumko wa bei ilikuwa ni moja ya ajenda kuu za CHADEMA katika uchuguzi huu.

  Habari zinaonyesha kuwa saruji imepanda kutoka Shs 12,500/ kufikia 15,000/= hapa mjini, ndoo ndogo ya mafyta ya kula imepanda kutoka Shs 16,000/= hadi Shs 24,000/= n.k

  Wakati natoa wito kwa wabunge wa CHADEMA kuanza kuisurubu Serikali kwa hali hii, naomba wanaJF wenye taaluma ya kiuchumi watusaidie nini chanzo cha hali hii kutokea tena kwa kiwango kikubwa kiasi hiki?
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Nov 15, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  acha tu bei ipande kwani nini..si ndo mijitu ilikuwa inataka mambo yawe hivo acha na yawe hivoo hivoo
   
 3. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #3
  Nov 15, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  kuna siku (kabla ya uchaguzi)nilikuwa navuka naelekea Kigamboni,
  Wakati nakata tiketi nikamwuliza makataji tiket mbona gharama ya kuvuka kwa gari ni kubwa.
  Akasema na bado kwani baada ya uchaguzi gharama itapanda zaidi.
  Nikashangaa kwanini ipande baada ya uchaguzi, nami sikupata jibu.
   
 4. Mnene 1

  Mnene 1 Senior Member

  #4
  Nov 15, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakuu, hili ni tishio na inasikitisha sana, kila kitu kimepanda bei na ukiuliza kwa nini muuzaji anakuambia hii bei ni baada ya kuchakachua.
  Naomba wadau mnaohusika mliangalie hili kwa jicho la tatu.
   
 5. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #5
  Nov 15, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kwani mlitegemea nini zaidi ya hayo kutoka kwa Mkwere? Humu ndani tulikuwa tukilalamika kuhusu CCM watu wanatuona wehu. Juzi naongea na watu wa bush kwangu wanalalamika kwamba wanashindwa kuuza mahindi kwa kuwa bei ipo chini mno. Sasa bei za mazao ya wakulima zimeshuka halafu bei za bidhaa nyingine ambazo wakulima wanazihitaji zimepanda. Hapo mkulima ana chake kweli? Lakini ni hao hao wakulima ndiyo walioongoza kwa kuipa kura CCM. Tuna lipi tena la kushauri. Acha zipande tu hata zaidi ya hapo. Na marufuku mtu kulalamika. Kwani hizo bei sizilifidiwa na Khanga na tshirt?
   
 6. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #6
  Nov 15, 2010
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kura mnawapa CCM, utatuzi wa matatizo ni CHADEMA. Hamwoni kuwa mnawatesa? Dr. Slaa aliwaambia bei ya Saruji haitazidi shs.5,000 watu wakaona haiwezekani sasa ikipanda si ndo kitu wanachotaka watu?
   
 7. chokambayaa

  chokambayaa JF-Expert Member

  #7
  Nov 15, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 528
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Unategemea nini mkuu wakati Tanzania kila kitu tunaagiza

  bei imepanda na shilingi imeshuka maana tunaagiza/nunua zaidi ya tunavyozalisha (unfavourable balance of paymment)
  hatuna cha maana tunachozalisha na kuuza nje zaidi ya madini na ambayo hatulipwi ipasavyo (ufisadi)
   
 8. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #8
  Nov 15, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,675
  Likes Received: 21,903
  Trophy Points: 280
  Umesema sahihi mkuu, asiyesikia la mkuu huvunjika guu. Watanzania wajiandae na maumivu makubwa sana katika miaka hii mitano ijayo. Pamoja na wizi wa kura, kama wengi wangetaka mabadiliko wizi wao usingefua dafu na sasa tungejipanga vingine katika mkakati wa kuinua kipato cha Mtz na kuzibiti mfumko wa bei. Ndugu zangu wa Singida,Lindi,Pwani Tanga na kwingineko mliko ng'ang'ania kuwa CCM ni nambari wani mtaendelea kuishi kwenye Tembe kwa miaka mingine mitano.
   

  Attached Files:

 9. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #9
  Nov 15, 2010
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Hawa watu wa vijijini hawaoni athali kubwa ya maisha, kwani nyumba zao ni za miti na udingo, na nyasi, vyote ni bure, wanahitaji tu chunvi , mafuta ya taa na viberiti, ambavyo havina athali kubwa ukilinganisha na watu wa mijini kila kitu ni cha kununua. Sasa cha msingi ni Kuwaconvisi ndungu zetu wa vijijini wasiipende ccm. kila mwanaharakati wa mjini afanye juhudi hizo.
   
 10. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #10
  Nov 15, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Ndio Bwn Jatropha huo ndio ukweli tumeliwa, wajinga ndio waliwao. Mpaka tumalize hiyo miaka mitano hakuna rangi tutaacha kuona. Ujumbe wa inflation utafika hadi vijijini watakapo nunua chumvi 1Kg Shs 1000/=. Bado tuu uchakachuaji kwenye uchumi unaendelea, na hiyo hakuna mtu wa kukwepa uwe CCM, CHADEMA wala CUF, we are sailing in same boat. Msg ya Dr Slaa itafika tuu!! Watu wataelewa.
   
 11. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #11
  Nov 15, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Iko siku tutachapata hatuwezi endelea kuumia kwa sababu ya watu wachache, Niliingia mtaani kwenda kufanya kiutafiti kidogo haya ndiyo matokeo:
  Karanga Kg1 2000 baada uchaguzi 3000
  Mchelek g1 1300 baada uchaguzi 1500
  Nyama kg1 4000 baada ya uchaguzi 4600
  Soya kg1 3000 baada ya uchaguzi 3600
  Mahindi ya makande kg1 600 baada ya uchaguzi 800
  Choroko kg1 3000 baada ya uchaguzi 4000
  Viazi sado1 1800 baada ya uchaguzi 2500
  Nyanya sado 2000 baada ya uchaguzi 5000
   
 12. R

  Rogers_ic Member

  #12
  Nov 15, 2010
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  watu waichukie ccm mara ngapi? walioipa kura ccm ni wanachama wa ccm
   
 13. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #13
  Nov 15, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180  Na bado!
   
 14. N

  Njaare JF-Expert Member

  #14
  Nov 15, 2010
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135

  Nakumbuka kuna mtu mmoja alitoa wito kwa wapiga kura hapa jamvini. Alisema, Ni vyema watanzania wasilale siku ya uchaguzi (kwa maana ya kupiga kura na kuzilinda) ili wapate serikali isiyolala au walale siku ya uchaguzi ili wapate serikali itakayolala miaka mitano ijayo wakati wao wakikesha kuikimbiza shilingi. Pia Mrema alisha sema kuwa kuichagua CCM ni kukata tiketi ya miaka 5 ya mateso.

  Mfumuko wa bei unaoonekana sasa hivi ni kionjo tu bado mfumuko wenyewe kina mkulo wakisharudi kusimamia uchumi. Tulipewa kunyoa au kusuka tukachagua kusuka sasa nywele zinawasha tunalalamika wakati tulijua kabisa mba wataingia na nyele zinawasha. Kunyoa baada ya kusuka ni gharama mara millioni kuliko kabla. Hatuwezi kubadili serikali ndani ya miaka 5 bila kumwaga damu hivyo tuendelee kuvumilia maumivu.

  Pia jamaa (Waagizaji) lazma wapandishe bei ili kurudisha hela walochangia CCM. Tunasingizia mfumuko wa bei ya dola lakini hii dola imekuwa 1500 toka mwezi wa sita na sasa fluctuation yake ni ndogo. Mbona bei haikupanda toka wakati huo?
   
 15. Lenana

  Lenana JF-Expert Member

  #15
  Nov 15, 2010
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 422
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  that is fucking style of ccm mwashanga nini mmelilia wembe mmepewa mwatarajia nini makato kwa kwenda mbele!
   
 16. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #16
  Nov 15, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ari zaidi Kasi zaidi sijui na nini malizia mwenyewe
   
 17. Gwallo

  Gwallo JF-Expert Member

  #17
  Nov 15, 2010
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 2,322
  Likes Received: 844
  Trophy Points: 280
  :israel:Kijiji changu ninachotoka tulifutilia mbali ccm toka mwaka 1999 mwenzi september wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaaa, ktk serikali ya kjiji changu chenye watu14 yaani m/kiti na katibu + timu ya watu 12 wanaounda serikali ya kijiji (Halmashauri ya kijiji) tuna mtu moja wa ccm naye yupo pale kwa sababu tu ni mpenda maendeleo.
   
 18. t

  truth Member

  #18
  Nov 15, 2010
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu Crashwise thanks for the facts. Sijui utafiti wako ulilenga zaidi maeneo yapi vile?. I really appreciate.
   
 19. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #19
  Nov 15, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  hamjaingia kwenye maduka ya madawa, pharmacies na medical stores, halafu mwananchi wa kawaida anatoa kila kitu toka mfukoni ( kama haujatoboka). Hana bima ya afya wala serikali haimsaidii hata kidogo.
   
 20. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #20
  Nov 15, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Naongezea kidogo (maeneo ya - sinza)

  Chumvi gm 250 toka 150 baada ya uchaguzi 300
  Always za kina dada 1300 baada ya uchaguzi 2000
  Petrol 1500 baada ya uchaguzi 1800
  Samaki fresh 4500 kgbaada ya uchaguzi 5500

   
Loading...