Kuongezeka kwa matukio ya wizi mtaani tofauti na awamu iliyopita. Je, chanzo ni nini?

Lanlady

JF-Expert Member
Feb 27, 2019
1,421
4,729
Kwa maeneo niliyopo, kusemaukweli awamu iliyopita kulikuwa na utulivu kwa kiasi kikubwa. Vijana wengi walihofia kuwekwa ndani na hivyo kujiepusha na matukio ya uhalifu.

Wengi wao walijishughulisha kwa bidii kwa kufanya shughuli mbalimbali kama vile biashara ndogondogo (machinga) ufundi na kazi nyingine za kutwa.

Hivi sasa matukio ya uhalifu wa mitaani yameongezeka sana. Ni kama vile watu walikuwa wanasubiri nafasi ya kutenda.

Je, chanzo hasa ni nini?
 
Leta uthibitisho wa hayo unayosema
Duh, sikupata hilo wazo la kurecord tukio llitokea hivi punde. Kuna jirani kaibiwa kuku wake bandani.

Wengine wanalalamika kuibiwa magodoro na vitu vingine ndani wakiwa hawapo.

Tofauti na hapo kabla hali ilikuwa shwari kwa kiasi kikubwa.

Ninachotamani kujua ni chanzo cha kuongezeka kwa haya matukio!

Je, ni ugumu wa maisha? Ukosefu wa ajira? Kumomonyoka kwa maadili?

Kukosa mtu/watu wa kukekemea?
 
Hebu mkafufue mtu wenu wa chato basi ili tupumzike na hizi kufuru zenu.
Kwanini umesema huyo wa chato?
Mie sijalinganisha mtu au uongozi.
Bali nimezungumzia hali ilivyo!
Kama tutaendelea kuweka ulinganishi na ushabiki wa kiongozi, tutashindwa kutatua changamoto zinazojitokeza kwa sasa.

Kuna kijana mmoja aliwahi kusema,baada ya kifo cha jpm, angetamani kiongozi fulani wa jeshi naye angefariki.

Nilipomuuliza sababu, akasema wameua watu wengi sana na kwamba kuna akina mama wamebaki wajane.

Kwahiyo nikagundua kwamba baadhi ya vijana waliogopa kufanya uhalifu kwasababu waliaminishwa kwamba wakikamatwa basi watauawa. Jambo ambalo hadi leo nalitafakari pasipo majibu sahihi hasa kwa kuhusianisha na hali ya sasa!
 
Kiukweli matukio ya wizi yameongezeka kwa kasi sana bora Mama angelifumua hili jeshi la polisi.
 
Back
Top Bottom