Kuombea wanaume ruhusa

Kuombea wanaume ruhusa

Mm mke wangu kajua kuwa tbc wanaonyesha..kalipia king'amuzi miezi miwili...imekula kwangu.

Khaaa, huyu shemeji yetu ni noumer, sipati picha kama angekua mcheza mpira and then kocha akamuweka nafasi ya senta hafu ingekuaje, asingekua anapita mtu hapoa aise!
 
mimi na mume wangu huwa tunaangalia wote ukitegemea tbc 1 wanaonyesha haendi mtu bandani
 
hakuna kuombeana ruhusa kwanza nyinyi na mpira sijui mmelogezewa? eti
 
Napenda kuwaombea ruhusa wanaume wote kuwa kuanzia tarehe 12 Juni 2014, mashindano ya kombe la dunia yataanza pale Brazil. Hivyo wewe mama, ukiambiwa na mwenzi wako kuwa anakwenda kuangalia mpira basi isiwe tabu.

Kwa kuwa litakuwa linachezwa usiku sana hata akirudi asubuhi jua alikuwa kwenye mechi.Tafadhali muache akina baba nao waburudike ndio wakati wao huu. Kijiwe cha umbea kwao nikuangalia mpira.

Natumaini hamtatuangusha akina MAMA/DADA MCHEPUKO SIO DILI BAKI NJIA KUU, kuangalia mpira sio mchepuko, lakini na nyie madada/ wamama, msitumie huo mwanya kuchepuka.

Ruhusa ya nini wakati kitu kitamwagwa live bila chenga TBC, TBC lazima wafanye juu chini watuonyeshe mechi hizo maana si wanatumia kodi zetu.Bora wasionyeshe the comedy (bunge) waonyeshe kombe la dunia
 
Kumbe wengi mmeoa eeh!! Mada zingine naona mpo singo, lol
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom