Kuombea wanaume ruhusa

bnf

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
218
Reaction score
79
Napenda kuwaombea ruhusa wanaume wote kuwa kuanzia tarehe 12 Juni 2014, mashindano ya kombe la dunia yataanza pale Brazil. Hivyo wewe mama, ukiambiwa na mwenzi wako kuwa anakwenda kuangalia mpira basi isiwe tabu.

Kwa kuwa litakuwa linachezwa usiku sana hata akirudi asubuhi jua alikuwa kwenye mechi.Tafadhali muache akina baba nao waburudike ndio wakati wao huu. Kijiwe cha umbea kwao nikuangalia mpira.

Natumaini hamtatuangusha akina MAMA/DADA MCHEPUKO SIO DILI BAKI NJIA KUU, kuangalia mpira sio mchepuko, lakini na nyie madada/ wamama, msitumie huo mwanya kuchepuka.
 
mbona na wadada wengi huwa kombe la dunia wanaangalia?
 
Naomba uniombee ruhusa na mimi aisee, tutabanana hapa hapa kwenye world cup
 
Mke wangu ameanza kupenda mpira ghafla.

Anawafahamu wachezaji wote kuanzia timu za taifa hadi vilabu wanavyotokea.

Kasema tutaenda nae kila mechi.
 
mbona na wadada wengi huwa kombe la dunia wanaangalia?

wengi kwa viwango gani? je idadi yao inalingana na wanaume? na labda nikukumbushe pia kuna baadhi ya wanaume hawaangalii ila ni wachache ukilinganisha na wanaongalia, hivyo hata kama kuna wanawake wanaangalia idadi yao ni ndogo ukilinganisha na wasio angalia....
 

lengo langu ni kusema tu kwamba kuna wadada wanapenda kuangalia kombe la dunia tu lakini idadi yao siwezi kuisemea
 
muda wa kuangali tamthilia na movie si ndo huu sasa
 
Mm mke wangu kajua kuwa tbc wanaonyesha..kalipia king'amuzi miezi miwili...imekula kwangu.
 
Kwani Dstv si wanaonyesha, bora muangalizie nyumbani....ili wachezaji wakizingua mcheze yenu.
 
Ndio maana my wife kila siku ananiuliza, kombe la dunia mara hii litachezwa saa ngapi
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…