Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,488
- 13,608
Mwaka jana ukame ulikuwa wa kutisha kanda ya kaskazini nzima. Basi linasimama pale Bombo na ukitazama wauza matunda hali ni mbaya ya kile wanachokiuza. Nakumbuka niliuziwa machungwa ya kuvundikwa hakukuwa na matunda mengine zaidi. Mwezi kama huu mwaka jana.
Hali naiona haina tofauti sana na mwaka huu, Jua linachomoza saa kumi na moja kasoro usiku na joto kali linaanza mapema kabla hata ya saa nne asubuhi. Ni muendelezo wa mwaka mwingine wenye ukame, mito inakauka na hali ya kijani inapotea. Madhara ya ukame tunayaona kwenye masuala ya maji. Mgao umekuwa ni mkali na umeme unaelekea huko huko.
Miaka ya nyuma tulizoea kumsikia Kiongozi wa Nchi akihamasisha viongozi wa dini wajitokeze ili waombee mvua. Imekuwa ni desturi iliyozoeleka haswa pale Jangwani au mnazi mmoja kuwaona viongozi wa kiislam na kikristo wakimuomba Mungu kwa nguvu kubwa ili ashushe maji yake yenye baraka.
Naona mwaka huu unapita kimya kimya na kiangazi kikali kinaendelea kutesa mtaani. Haiwezekani viongozi wa dini wakaanzisha wao hoja ya kuombea mvua?. Mtandao wao unaozoeleka katika masuala mbalimbali nyeti kusikika ukikemea au kutoa mwongozo naona upo kimya tu!, kama vile kuombea mvua sio suala nyeti.
Au kunakuwa na siasa za bahasha kutoka kwa wenye mamlaka ya kuongoza nchi kuelekea zilipo akaunti za benki za Mababa Askofu?. Pengine tunapowaona wakiitikia hoja za kiserikali nyuma ya pazia kunakuwa na mshiko maalum unaotolewa, nimesema pengine nikiwa sina uhakika na kauli ninayoisema.
Mungu anapoibariki Tanzania kwa kuipa kila aina ya maliasili anakuwa akitushangaa sana tunapomuomba atudondoshee maji yake maalum!, tungekuwa tunawasiliana nae moja kwa moja hakika angetuuliza maswali mengi sana ya msingi.
Lakini siku zote ni mwenye huruma kwa waja wake, hata anapokosewa saba mara sabini humpokea mja wake anayekuja akiwa anafanya toba ya kutoka ndani kabisa ya moyo wake. Huu ukimya wa sasa wakati kinamama na kinadada wanaonekana mitaani na ndoo vichwani unaleta mashaka.