Kuombea mvua wakati ni huu viongozi wa dini sauti zenu zisikike

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,489
13,608
Mwaka jana ukame ulikuwa wa kutisha kanda ya kaskazini nzima. Basi linasimama pale Bombo na ukitazama wauza matunda hali ni mbaya ya kile wanachokiuza. Nakumbuka niliuziwa machungwa ya kuvundikwa hakukuwa na matunda mengine zaidi. Mwezi kama huu mwaka jana.

Hali naiona haina tofauti sana na mwaka huu, Jua linachomoza saa kumi na moja kasoro usiku na joto kali linaanza mapema kabla hata ya saa nne asubuhi. Ni muendelezo wa mwaka mwingine wenye ukame, mito inakauka na hali ya kijani inapotea. Madhara ya ukame tunayaona kwenye masuala ya maji. Mgao umekuwa ni mkali na umeme unaelekea huko huko.

Miaka ya nyuma tulizoea kumsikia Kiongozi wa Nchi akihamasisha viongozi wa dini wajitokeze ili waombee mvua. Imekuwa ni desturi iliyozoeleka haswa pale Jangwani au mnazi mmoja kuwaona viongozi wa kiislam na kikristo wakimuomba Mungu kwa nguvu kubwa ili ashushe maji yake yenye baraka.

Naona mwaka huu unapita kimya kimya na kiangazi kikali kinaendelea kutesa mtaani. Haiwezekani viongozi wa dini wakaanzisha wao hoja ya kuombea mvua?. Mtandao wao unaozoeleka katika masuala mbalimbali nyeti kusikika ukikemea au kutoa mwongozo naona upo kimya tu!, kama vile kuombea mvua sio suala nyeti.

Au kunakuwa na siasa za bahasha kutoka kwa wenye mamlaka ya kuongoza nchi kuelekea zilipo akaunti za benki za Mababa Askofu?. Pengine tunapowaona wakiitikia hoja za kiserikali nyuma ya pazia kunakuwa na mshiko maalum unaotolewa, nimesema pengine nikiwa sina uhakika na kauli ninayoisema.

Mungu anapoibariki Tanzania kwa kuipa kila aina ya maliasili anakuwa akitushangaa sana tunapomuomba atudondoshee maji yake maalum!, tungekuwa tunawasiliana nae moja kwa moja hakika angetuuliza maswali mengi sana ya msingi.

Lakini siku zote ni mwenye huruma kwa waja wake, hata anapokosewa saba mara sabini humpokea mja wake anayekuja akiwa anafanya toba ya kutoka ndani kabisa ya moyo wake. Huu ukimya wa sasa wakati kinamama na kinadada wanaonekana mitaani na ndoo vichwani unaleta mashaka.
 
Imani ina mambo yake, katika vitu sijawahi kuamini ni hayo maombi ya mvua sijui toka kwa viongozi wa dini. Kama mvua hainyeshi ni kwasababu za mabadiliko ya tabia nchi, na sioni kiongozi yoyote wa dini akifanya lolote la kuleta mvua kwa the so called maombi. Tuchimbe mabwawa na kuvuna maji wakati wa mvua nyingi. Tuache kumjaribu Mungu kwa uzembe wetu. Hakuna kiongozi wa dini anaweza kuomba mvua ije.
 
Kwanini tusikasirikiwe na Ngai?
francis.png
 
Mwaka jana ukame ulikuwa wa kutisha kanda ya kaskazini nzima. Basi linasimama pale Bombo na ukitazama wauza matunda hali ni mbaya ya kile wanachokiuza. Nakumbuka niliuziwa machungwa ya kuvundikwa hakukuwa na matunda mengine zaidi. Mwezi kama huu mwaka jana.

Hali naiona haina tofauti sana na mwaka huu, Jua linachomoza saa kumi na moja kasoro usiku na joto kali linaanza mapema kabla hata ya saa nne asubuhi. Ni muendelezo wa mwaka mwingine wenye ukame, mito inakauka na hali ya kijani inapotea. Madhara ya ukame tunayaona kwenye masuala ya maji. Mgao umekuwa ni mkali na umeme unaelekea huko huko.

Miaka ya nyuma tulizoea kumsikia Kiongozi wa Nchi akihamasisha viongozi wa dini wajitokeze ili waombee mvua. Imekuwa ni desturi iliyozoeleka haswa pale Jangwani au mnazi mmoja kuwaona viongozi wa kiislam na kikristo wakimuomba Mungu kwa nguvu kubwa ili ashushe maji yake yenye baraka.

Naona mwaka huu unapita kimya kimya na kiangazi kikali kinaendelea kutesa mtaani. Haiwezekani viongozi wa dini wakaanzisha wao hoja ya kuombea mvua?. Mtandao wao unaozoeleka katika masuala mbalimbali nyeti kusikika ukikemea au kutoa mwongozo naona upo kimya tu!, kama vile kuombea mvua sio suala nyeti.

Au kunakuwa na siasa za bahasha kutoka kwa wenye mamlaka ya kuongoza nchi kuelekea zilipo akaunti za benki za Mababa Askofu?. Pengine tunapowaona wakiitikia hoja za kiserikali nyuma ya pazia kunakuwa na mshiko maalum unaotolewa, nimesema pengine nikiwa sina uhakika na kauli ninayoisema.

Mungu anapoibariki Tanzania kwa kuipa kila aina ya maliasili anakuwa akitushangaa sana tunapomuomba atudondoshee maji yake maalum!, tungekuwa tunawasiliana nae moja kwa moja hakika angetuuliza maswali mengi sana ya msingi.

Lakini siku zote ni mwenye huruma kwa waja wake, hata anapokosewa saba mara sabini humpokea mja wake anayekuja akiwa anafanya toba ya kutoka ndani kabisa ya moyo wake. Huu ukimya wa sasa wakati kinamama na kinadada wanaonekana mitaani na ndoo vichwani unaleta mashaka.
Mnaharibu mazingira na vyanzo vya maji halafu mnataka huyo huyo Mungu afanye miujiza gani !?
 
Askofu Dr Shoo ameshatangaza maombi ya nchi nzima

Amesema ukame huu siyo wa kawaida

Amefanya hivyo kwa mazoea tu, na kwakuwa anajua bado watu wanaimani na mambo ya maombi, basi naye anawatembezea humo humo. Lakini ki ukweli hakuna kiongozi yoyote wa dini anaweza kuomba mvua na ikanyesha. Hata ikinyesha sio kwa ajili ya maombi, bali ni lazima ingenyesha tu.
 
Hello, love u
 
Tayari utabiri ushatolewa, mvua itanyesha lini. sije wakaomba siku moja kqbla wakachukua credit

Hao viongozi wa dini wanataka kuchukua pointi za mezani. Mvua itanyesha hivi karibuni bila hata maombi yao. Hao viongozi wa dini wafanye mambo mengine yenye tija, sio kucheza na beat za wanasiasa.
 
Africa tamu sana mnabomoa kiwanda mnakigeuza nyumba ya ibada kisha mnaitumia kumwomba Mungu awape ajira
Mnakata miti milion karibia 3, kisha mnarudi kwa Mungu kumwomba mvua
 
Bila ya wanatuongoza kukumbuka walisahau wapi, lini na kwa nini? kumtaja na kumuweka Mungu wa Mbinguni Kwanza kabla ya yote, hali hii ya mambo itaendelea kuwa ngumu. Mfalme Ahabu alishindwa kula hata chakula wakati wa dhiki ile ya kiangazi kile kilicho itishwa na Nabii Eliya.

Hivi kweli Tanzania tumerudia tena ile dhiki ya awamu ya 4 ya kuzungumzia mgao wa umeme na kero za kelele ya majenerata kila upande wa nchi?!. Kweli???!!!
 
Askofu Dr Shoo ameshatangaza maombi ya nchi nzima

Amesema ukame huu siyo wa kawaida
Ahimize waumini wake kutunza mazingira kwa kupanda miti mingi. Katika dayosis, sharika na nyumba za waumini wake waonyeshe mfano kwa kupanda miti na kutunza mazingira wakati huo maombi yaendelee
 
Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom