Inasikitisha; Uwajibikaji wa viongozi wetu umeshuka mno

Vyamavingi

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
5,745
5,446
Kuna mambo yanaumiza sana, yanaathiri uchumi na maisha ya Watanzania wengi kutokana na uwajibikaji duni wa viongozi wetu na setikali.bKwa sasa tunarudi nyuma kwa kasi wakati tulishakuwa na matumaini kuwa tunasonga mbele.

Matatizo tunayosikia kutoka kwa wananchi katika ziara za Makonda, dhidi ya polisi na mambo mengine yanadhihirisha jinsi uwajibikaji wa viongozi ulivyopungua. Inafikia mahali Makonda anasema , kama ingekuwa enzi za utawala uliopita wangenikoma!

Hebu tafakari haya; maji na umeme katika miji na majiji kama Dar kwa sasa limekuwa tatizo! Haya matatizo tulishayasahau, ukame ulikuwepo na mvua hazikutosha lakini maji na umeme tulipata!

Leo Dar maji yamekuwa tatizo, viongozi wako kimya, DAWASA wako kimya wakati mvua iko bwelele, mito imejaa na kufurika! Hakuna maelezo lakini kuna mgawo usio rasmi wa maji, DAWASA hawasemi, Wazi wa Maji naye yuko kimya!

Umeme nao tatizo limeanza upya, mgawo si mgawao, hakuna umeme! TANESCO wako kimya, Naibu Waziri Mkuu/Waziri wa Nishati anatupatia sababu zisizo na mashiko, ati wizi wa transformer 80! Transforma 80 ndio zinafanya jiji zima kuwa na mgawo! Mwanzo walituambia upungufu wa maji kwenye mabwawa ya kuzalisha umeme, mara miundombinu imechoka, haikuwa inafanyiwa matengenezo kwa miaka 7 ya JPM! Uongo mtupu, yaani JPM alikuwa na mkatab na Mungu, kuwa mvua hazikupungua kwa miaka 7! TANESCO wana miundombinu gani yenye uwezo wa kuhimili uchakavu kwa miaka 7?

Ukweli ni kuwa uwajibikaji wa viongozi wetu umeporomoka sana, viwango vya serikali kujali watu wake na usitawi wao vimedorora sana.

Vv
 
WAKUBWA WANACHEPUSHA MAJI YA CONGO BASIN MAKUSUDI YASIINGIE KWENYE MTERA HEP.

LENGO
1. KUJA NA KAMPUNI TANZU ZA KUZALISHA UMEME, IPTL NK

2. KUUZA GENERATORS, SORAL WIND VANE NK.

MASIKINI TANZANIA YANGU
 
Kuna mambo yanaumiza sana, yanaathiri uchumi na maisha ya Watanzania wengi kutokana na uwajibikaji duni wa viongozi wetu na setikali.bKwa sasa tunarudi nyuma kwa kasi wakati tulishakuwa na matumaini kuwa tunasonga mbele.

Matatizo tunayosikia kutoka kwa wananchi katika ziara za Makonda, dhidi ya polisi na mambo mengine yanadhihirisha jinsi uwajibikaji wa viongozi ulivyopungua. Inafikia mahali Makonda anasema , kama ingekuwa enzi za utawala uliopita wangenikoma!

Hebu tafakari haya; maji na umeme katika miji na majiji kama Dar kwa sasa limekuwa tatizo! Haya matatizo tulishayasahau, ukame ulikuwepo na mvua hazikutosha lakini maji na umeme tulipata!

Leo Dar maji yamekuwa tatizo, viongozi wako kimya, DAWASA wako kimya wakati mvua iko bwelele, mito imejaa na kufurika! Hakuna maelezo lakini kuna mgawo usio rasmi wa maji, DAWASA hawasemi, Wazi wa Maji naye yuko kimya!

Umeme nao tatizo limeanza upya, mgawo si mgawao, hakuna umeme! TANESCO wako kimya, Naibu Waziri Mkuu/Waziri wa Nishati anatupatia sababu zisizo na mashiko, ati wizi wa transformer 80! Transforma 80 ndio zinafanya jiji zima kuwa na mgawo! Mwanzo walituambia upungufu wa maji kwenye mabwawa ya kuzalisha umeme, mara miundombinu imechoka, haikuwa inafanyiwa matengenezo kwa miaka 7 ya JPM! Uongo mtupu, yaani JPM alikuwa na mkatab na Mungu, kuwa mvua hazikupungua kwa miaka 7! TANESCO wana miundombinu gani yenye uwezo wa kuhimili uchakavu kwa miaka 7?

Ukweli ni kuwa uwajibikaji wa viongozi wetu umeporomoka sana, viwango vya serikali kujali watu wake na usitawi wao vimedorora sana.

Vv
Kwamba Tzn yote hii matatizo yaliisha si ndio? Kwa hiyo yamekuja si ndio unataka kutuambia?
 
Kwahiyo wewe hauoni au upo wapi au upo kolomije?

Kama upo Dar mtafute kinyozi wa saluni alafu muulize kipindi hiki Cha mama ni kile Cha Magu ni kipindi kipi kigumu kwake

Nimekupa njia rahisi ya kupata jibu maana wewe unaonekana ni kilaza
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom