Kayinga junior
Senior Member
- Feb 19, 2012
- 152
- 7
msiige ndoa zakina chuma ulete
Aisee!
Ukweli huu unauma sana!
Bahati yangu nilioa zamani sana, na niliolea kijijini ambapo gharama nyingi za hapo juu zilijifuta automatically!
Kwa hiyo hela si naweza nikafungua kampuni yangu ndogo hapo.Kwa hali hiyo bado niponipo sana..
Leo tupumzike na habari za siasa na habari zinazowahusu watu tuangalie mtu unapojianda kuowa
Kuna thread moja inahusu michango ya harusi imenikumbusha mbali. Hivi
jamani, mnazijua gharama anazoingia bwana harusi hadi anapooa? Katika hali
ya kawaida kabisa, kama wewe ni mwanaume na unataka kuoa, jiandae kwa mambo
haya:
1. Kujitambulisha ukweni. Hapo utatakiwa uende kijijini alikozaliwa mkeo
mtarajiwa ukajitambulishe huko. Kama mfano mkeo anatokea Mwanza, na mnaishi
Dar, andaa nauli ya watu wawili, malazi kwa siku mbili, na utagharamia
shug​huli hiyo ya utambulisho. We tenga 500,000. Hapo tuna assume mkeo
atajitegemea. Otherwise 800,000 itakutoka.
2. Kumtambulisha mkeo kwenu. Kama nyie nyumbani ni Arusha, utatakiwa
umpeleke huko Ngarenanyuki. Sio umlete hapo Tabata mlipopanga. Hapo sio
kwenu! Andaa nauli yako na atakaekusindikiza, nauli ya binti na mwenzie, na
gharama za vinywaji na chakula siku hiyo. Utahitaji kama 700,000
3. Kifuatacho ITV ni kuwaalika wakwe zako nyumbani. Uwatoe watu kama nane
Mwanza, uwalete Arusha. Wale, walale, wajisaidie, kwa gharama zako. We acha
ubishi, tenga 800,000 tu.
4. Kwani we wazazi wako wanajua unakooa? Sasa je? Wasafirishe kwenda
Mwanza! Watu watano. Utahitaji kuwa na 500,000. Beba pia ATM card yako, kuna
imejensi.
5. MAHARI ndio topic inayofuata sasa. Ukiwa mjanja, unganishia kwenye
hiyo safari hapo juu uue ndege wawili. Pamoja na hayo, itabidi ubebe
2,000,000.
6. Sasa kijana unaweza kumvisha mchumba wako pete. Nunua ya kawaida
kabisa ya dhahabu. 350,000. Tukio lenyewe la kumvisha pete unaweza ita
marafiki wawili watatu ukatumia 200,000. Au fanya sherehe kabisa. Mi simo
7. Oke, sasa unaweza kuitisha vikao vya harusi. Tengeneza kadi za mwaliko
wa kamati kwa 200,000, kikao cha kwanza gharama zote ni juu yako. Andaa
500,000. Swali la kwanza kwenye kikao: "We una shing ngapi?" Sema 1,000,000.
8. Utahitaji 100,000 ya sms na simu kukumbushia michango. (Shukuru Mungu
kuna cheka time)
9. Wakati vikao vinaendelea, utatuma 200,000 kwa m-pesa ili mambo ya
kimila yaendelee kule nyumbani. We unaelewa
10. "Darling, sasa mi kwenye kitchen party ntavaa nini?" 300,000!
11. "Darling, kuna mahali nimeona gauni zuri la send." 400,000!
12. "Baby, rafiki yangu alinunua gauni la harusi China yani lilimpende..."
700,000!
13. Wakati huo wewe mwenyewe hujajua utavaa nini, hujanunua pete za
harusi, hujamvalisha best man na mkewe. Tuseme unahitaji kama 1,500,000
maana utalia lia sana. Kumbuka, gharama hizi huchangiwi na kamati. Wala
hutarudishiwa.
14. Siku ya send off lazma uende Mwanza. Utaenda mwenyewe? Ndugu wawili
watatu na mshenga 600,000. Kwenye send off utatakiwa kutoa sijui blanketi la
bibi, vitenge vya mashangazi, na vikorokoro kibao. Nunua hivyo vitu 300,000
uende navyo ili kupunguza gharama. Beba 200,000 za wale mashangazi
watakaoibuka ghafla!
15. Mshonee baba mkwe suti 100,000 mama mkwe yeye atavaa gauni la 50,000.
16. Fotokopi hiyo hapo juu (namba 15) kwa wazazi wako. 150,000
17. Watu watakaopenda kuvaa sare wajitegemee! Mimi sina hela! Ila
utavishonea nguo vile vitoto kwa 80,000.
18. Siku mbili kabla ya harusi, utaanza kupokea wageni. Unatakiwa
uwatafutie malazi na chakula. Kwa ujumla utahitaji kama 500,000
19. Jioni watoe auti mashemeji zako ambao hawajawahi kufika Dar
ukawanunulie bia ili wakuone wa maana. 200,000
20. Siku ya harusi bibi harusi na mwenzie na watoto na ma maids watatakiwa
wakapambwe saluni. 200,000
21. We na mwenzio mtaenda kunyoa hapo kwa nanii. Ndevu na nywele na black
kibishi 40,000
22. Siku ya harusi beba sadaka 10,000. Wakati huo umeshamtuma kijana
akakulipie hoteli mtakayofikia baada ya harusi. Kamati haitoi hela hiyo, so
utalipa malazi ya siku mbili 200,000
23. Kama mtaenda honeymoon sehemu yoyote nzuri nzuri nje ya mji, si chini
ya 800,000 kwa angalau siku 5.
24. Wakati uko huko honeymoon, huna hata kumi, mwanakamati mmoja ambae
hakuchanga anakupigia simu " Sasa tunavunja lini kamati?" Pesa yote
iliyochangwa ilitumika kwenye harusi, sasa gharama za kuvunja kamati ni za
nani?? 500,000!
25. SASA MNAANZA MAISHA YA UNYUMBA. 14,180,000 poorer.
KAZI KWENU MSIOOA/MTAKAOOA TENA.KAM VIPI JIWEKE MAPEMA HAAA HAAAAAA HAAAAAA
chanzo. Allen Mazoko mazokoallen@yahoo.com
Hiyo nadhani itakuwa inawahusu watoto wa kishua zaidi si choka haituhusu kabisa anamtundika binti mimba wazazi wakileta mdomo unawaambia nikabidhini mzigo wangu unachukua mzigo anaweka ndani kiumbe kikizaliwa baadae ndio mnaanza harakati za kubariki ndoa
Mlolongo woooote mi wala haunitishi kwani wapo wanao oa kwa 100000/ na akaondoka na mkewe! Yani swala la gharama sio issue kabisa wala haisababishi wanaume kutokuoa kabisa! Hayo yanafanyika kutokana na uwezo wa muhusika mwenyewe
Lipo jamboajingine ambalo hufanya wanaume wawe wagumu kutoa maamuzi ya kuoa! Unamuana mke wa jirani yako anatenbea na jamaa fulani,rafiki yako anatembea na mke wa mtu, wewe nae giril friend wako kaolewa kwakua labda mambo yako yalikua badobado na akajitokeza jamaa kafika jumlala.haya baby wako kaolewa lakini akipata nafasi mkikutana mnnapeana libeneke!
Sasa chukulia kijana ambae hajaoa anayaona yote hayo huo uamuzi wa kuoa atautoa wapi? Na hasa akijiuliza hizo gharama? Wataishia kuishi kinyumba bila ndoa! Na wadada nao jiingize king uoe harakaharaka ukae ukijua mkeo hamuachi last boyfriend wake kabla ya wewe kama ulivyo wewe na last girlfriend wako kabla hajaolewa mnavyoliendeleza libeneke mkikutana!
Siku hizi imebaki NDOA ZA UKUMBINI KUTIMIZA WAJIBU baada ya ukumbini nyumbani kero tu
Mlolongo woooote mi wala haunitishi kwani wapo wanao oa kwa 100000/ na akaondoka na mkewe! Yani swala la gharama sio issue kabisa wala haisababishi wanaume kutokuoa kabisa! Hayo yanafanyika kutokana na uwezo wa muhusika mwenyewe
Lipo jamboajingine ambalo hufanya wanaume wawe wagumu kutoa maamuzi ya kuoa! Unamuana mke wa jirani yako anatenbea na jamaa fulani,rafiki yako anatembea na mke wa mtu, wewe nae giril friend wako kaolewa kwakua labda mambo yako yalikua badobado na akajitokeza jamaa kafika jumlala.haya baby wako kaolewa lakini akipata nafasi mkikutana mnnapeana libeneke!
Sasa chukulia kijana ambae hajaoa anayaona yote hayo huo uamuzi wa kuoa atautoa wapi? Na hasa akijiuliza hizo gharama? Wataishia kuishi kinyumba bila ndoa! Na wadada nao jiingize king uoe harakaharaka ukae ukijua mkeo hamuachi last boyfriend wake kabla ya wewe kama ulivyo wewe na last girlfriend wako kabla hajaolewa mnavyoliendeleza libeneke mkikutana!
Siku hizi imebaki NDOA ZA UKUMBINI KUTIMIZA WAJIBU baada ya ukumbini nyumbani kero tu