Kuoa si jambo dogo, unatakiwa uwe umejiandaa

Kuoa si jambo dogo, unatakiwa uwe umejiandaa

Tunakokwenda,sherehe za harusi zitafanywa na wenye uwezo wa kifedha tu.

Kwangu mie,harusi sitofanya ila nitaenda kufunga ndoa tu kanisani tena ile ya saa 12:30 asbh,tukitoka hapo ni kuendelea na Kazi tu
 
Harusi yangu na process zote za kupata mke hazitazidi 5 milioni tshs, ntafanya harusi based on my fantasy na sitochangisha hata kumi. Ntaalika few and very important family members, friends ni wale wa shida yako shida yangu jana, leo na kesho. Waliobaki katika ndugu na rafiki watapewaga recorded video waangalie.

Nafanya harusi kwa hela ya mfukoni mwangu ili:-
  • niwe na sauti na maamuzi magumu katika ndoa yangu maana hata ndugu hatathubutu kutia neno kwani hajatoa hata kumi kwa mahusiano yangu.
  • sitaki familia za watu ziishi kwa kujibana ili wanichangie mie.
  • natoa hela ya mfukoni mwangu ili yeyote ataesema tuchange nimwambie wewe changisha ila hela yenu itakuwa mtaji wa projects zangu ambazo zitanipa cash flow na sio sherehe ya kupoteza hela na wakati hata forbes hawanijui.
Ifike mahala tuishi kama wazungu ama zile familia za kitajiri zisizotaka umaarufu. Oa kwa jinsi mfuko wako unavyoruhusu na sio unataka kuoa kwa hesabu za mifuko ya watu.
 
Namba 23 hiyo peas ndogo sana , maana kuna usafiri, kula na mambo ya hapa na pale zaidi ya 2mil na zaidi tena Kama usafiri ni ndege
 
Back
Top Bottom