Kuoa kwa harusi au bila harusi kipi bora?

La maana sana,maana ukichangiwa na watu elfu moja nawe utawachingia watakapo oa au kuolewa aka wao au jamaa wa karibu.....
 
Mi nitapiga ndoa ya mkeka,yani wahusika tu (wazazi pande zote mbili na wafungishaji ndoa). Wengine waendelee na majukumu yao ya kila siku, sitak kuwaona. Hapo nitakua nimetumia bajet chini ya sh.50,000/=
 
Mie ndoa inafungwa saa 12 alfajiri baada ya swala ya asubuhi afta zati ni gahwa na tende hapo hapo msikitini kisha nasepa na maiwafu honeymoon.naacha sherehe ya nyumbani inaendelea hakuna kadi wala kiingilio anakaribishwa kila mtu ndugu jirani,marafiki na hata watu wa mtaani wanakula na kunywa inakuwa kama sadaka,ntapita tu wan taim kuwasalimu wageni na kufinya cha mtume kisha tunasepa no kuuzishana sura,nashuhuli nitafanya nayoimudu sitachangisha mtu,watakaojitolea wenyewe bila shuruti nitapokea.mambo ya ukumbini nawaachia wanaoyaelewa,the fairytale wedding industrial complex
 
Mkuu usinisahau kwenye gahwa.Nitakuja tuinogeshe kwa stori za hapa na pale ili kuvuta uradi!
 
Mkuu unataka kumuudhi mleta uzi?Yeye anataka kuoa kininja tu.Anataka kumtwaa bibie kama anaokota mapera porini.
duhhh!!! siku akionana na wazazi wake atakutana na mvua ya faini kabla ya kuongea mahari. Na ikatokea matatizo ya kiafya maana ya mungu mengi atapata tabu sana.
 
Nimewahi kuwa meneja wa kumbi za harusi kubwa tu hapa mjini.

Sherehe zote zinazo karibisha ndoa, harusi, send off , kitchen party na nyinginezo asilimia kubwa 85% ni michango ya watu. Matatizo hutokea kwenye michango, na mara nyingi ma bifu na viburi huibuka. Mtu asipo changa ndio mwanzo wa kutosalimiana na mahusiano huweza isha.

Wengi wa bwana harusi na bibi harusi asilimia kubwa unakuta mmoja wao ndie mwenye kipato cha wastani au mwajiriwa.

Tatizo linatokea pale ambapo Bwana harusi na bi harusi huingiza ela nyingi kutoka mifukonu mwao ili kufanikisha shughuli hizo kwa kukopa bank, jamaa nk

Kiufupi ni kwamba asilimia kubwa ya ninao wafaham na niliokutana nao wanaishi maisha ya tabu sana na huwezi amini ni huyu ndie alifunga harusi ya 40M. Wengi wao baada ya mazungumzo hujuta sanaa. Tukio la siku moja linakugharimu miaka 2-3 kwa kuishu kwa tabu sanaa.

Niliapa kabisa kamwe sita kuja fanya michezo hii ya kuigiza kama sina kipato kikubwa cha kuchezeaa. Mimi kama nitafunga harusi sinta mchangisha mtu yoyote hata sumni.
Pili harusi yangu haita zidi watu 50.

Asilimia kubwa ya wanao alikwa kwenye harusi ni wachangiaji, na wengi hutaka kuona ela yao waliochanga wanaifaidi vipi. Ikitokea tofauti kile anachokiona mezani hakiendani na ela aliyotoa majungu ndo huzalishwa hapa.

Harusi nyingi zina majungu, mara bi harusi hajapendeza, mara bi harusi sijui kabila gani, mara bi harusi kanunaa, mara harusi imepoaa, yanii ukumbini ni kuchoranaa tupuuuu.

Kwa ushauri wangu, vijana tusipende fame ya muda mfupi. Tusipende kufurahisha watu kwa muda mfupi alafu muda mrefu unagharamika wewe. Tusipende kuigaiga.

Kama huna uwezo wa hizi mambo, achana nazo, zinagharama sana, kuanzia kifedha hadi kisaikolojiaa.
Fact tupu umeongea
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom