Kuoa kwa harusi au bila harusi kipi bora?

Kuoa kwa harusi au bila harusi kipi bora?

Unakuta jamaa hana kiwanja wala biashara ya kueleweka halaf anakuletea kadi ya mchango wa harusi ya laki moja ukihoji anakwambia bajeti ya harusi ni milion 10
Jaman vijana wenzengu hebu tufanye harusi kwa kadri ya uwezo wetu na tuache huu ulimbukeni
 
Siku hizi mtu akitaka kuoa kuna kuwa na event nyingi mara utasikia kutangaza uchumba, pete ya uchumba, kitchen part [wakati muolewaji ameishawah ishi na mwanaume mwingine kwenye sogea tuish miaka saba] mara ndo send off then harusi!!!! baada ya harusi jamaa anabaki hana kitu hadi vyombo vya ndani vya kuunga unga! mi naona Bora kuoana bila harusi ili fedha ya sherehe nifanyie mambo mengine!!!
Bila harusi
 
Sherehe kama hizo huwa hazirudiwi kama birthday ni mara moja mtu kufanya sherehe yenye uwezo wake sio mbaya , kwangu mie
 
Wanaume tunaweza lakini wanawake hawawezi kwakuwa wanawake wanapenda sana sherehe na sifa kwa iyo ugumu ndio upo hapo
 
Kama haipo kwenye uwezo wako bora usifanye ni hasara sana, ila siku hizi wanawake wanapenda sherehe kuliko ndoa yenyewe
 
Unakuta jamaa hana kiwanja wala biashara ya kueleweka halaf anakuletea kadi ya mchango wa harusi ya laki moja ukihoji anakwambia bajeti ya harusi ni milion 10
Jaman vijana wenzengu hebu tufanye harusi kwa kadri ya uwezo wetu na tuache huu ulimbukeni
😂uzuri ukipeleka kadi yako pia atachanga
 
Back
Top Bottom