UTAFITI: Wanawake wanapenda harusi kuliko ndoa

Princep

JF-Expert Member
Nov 25, 2016
565
792
Suala la kuoa na kuolewa limekuwa gumzo na muda mwingine kuleta mtazamo tofauti katika jamii.

Sio mara moja au mbili umesikia kuwa wachumba wameshindwa kuoana kwa sababu familia moja ya mwanamke au mwanaume kukomalia lazima ndoa ifanyike na harusi.

Wazazi ama walezi au mtoto mwenyewe anayeenda kuoa ama kuoelewa anaweza kukomaa kuwa hawezi kuingia kwenye ndoa pasipo sherehe ya ndoa yaani harusi lasivyo ataachana na mchumba na kutafuta mwingine ambae yupo tayari kufanya hivyo.

Katika utafiti wa visa kama hivi imebainika kuwa wanawake ndio hupenda kushiriki ndoa kwa mtindo wa harusi kuliko wanaume.

Utafiti unaonyesha kuwa wanawake huvutiwa zaidi na sherehe za harusi kabla ya ndoa yenyewe. Kwa mujibu wa mtandao wa The Star Kenya unabainisha kuwa wanawake wengi hupenda ufahari wa kuonekana hivyo kutamani harusi kuliko wanaume.

Mwanamke/binti akipata mchumba mavazi ya kupendeza, viatu vya bei ghali humvutia zaidi kichwani mwake na kumsukuma kutaka harusi zaidi kuliko kufikiria mambo ya ndoa yatakuwaje.

Bila shaka umeona mara nyingi harusi hufanyika kwa gharama kubwa yenye kupendeza lakini ndoa isidumu hata mwaka wanaachana? Yote haya ni matokeo ya wanawake kutowaza maisha ya ndoa kipindi cha uchumba kwa kuangalia zaidi harusi pasipo kufikiria mapungufu na uimara wa wenza wao wanaotarajia kuingia nao kwenye ndoa.

Kwa mujibu wa utafiti Wanaume wengi hushiriki sherehe za harusi kwa ushawishi wa wanawake ni asilimia chache sana wanaoamua wao wenyewe kwa hiari.

Utafiti unagusa pia katika mafundisho ya ndoa kuwa wanawake wengi hukosa hamasa ya kuudhuria mafundisho ya ndoa na kuelekeza akili zao katika kufikiria Sherehe ya harusi itakuwaje, ni namna gani itasisimua jamii na kuonekana ni ya tofauti.

Matokeo ya utafiti huu yanaangazia mitazamo ya wanawake walioingia kwenye ndoa kwa mtindo wa harusi na uimara wa ndoa zao, utafiti unabaini kuwa wengi wao hawakupata maandalizi ya Kutosha kuhusu ndoa yenyewe.

Aidha jamii imeaswa kubadili mitazamo kuhusu suala ndoa kwa kuacha kuelekeza nguvu nyingi katika kushindana kuandaa sherehe za harusi za kifahari jambo ambalo halina maana kwenye ndoa.

Source: gospomedia
 
Back
Top Bottom