Kuoa kwa harusi au bila harusi kipi bora?

Kuoa kwa harusi au bila harusi kipi bora?

Vema tu.Ila ieleweke kuwa kutoa mahari siyo adhabu au faini.Ni kutoa shukrani,kukubali undugu mpya na kuonesha uimara wa kubeba jukumu la kuwa kiongozi wa familia tarajiwa.
ukipewa lift nauli ya nini? kikubwa kuwa mpole mpaka michepuko au kifo kitakapo watenganisha!
 
Jambo jema linalofanywa kimya kimya au mahali pa siri ndo huwa na dhawabu(mibaraka) toka kwa MOLA ila kama ukiamua kulifanya adharan kwenye macho ya walimwengu utapokea dhawabu za walimwengu (wivu, chuki, masengenyo, vicheko, husda na mengineyo mengi)
 
ukipewa lift nauli ya nini? kikubwa kuwa mpole mpaka michepuko au kifo kitakapo watenganisha!
Lift ina gharama zake.Gari likipata pancha utapewa jeki utoe tairi.Rejeta ikileta rabsha unapewa gudulia ukachote maji na mpo Mikumi mbugani.Na ukiomba lift ukakuta mbele wamejaa(pick ups) ukubali kudandia kwenye bodi na mvua inanyesha.Tafakari
 
Jambo jema linalofanywa kimya kimya au mahali pa siri ndo huwa na dhawabu(mibaraka) toka kwa MOLA ila kama ukiamua kulifanya adharan kwenye macho ya walimwengu utapokea dhawabu za walimwengu (wivu, chuki, masengenyo, vicheko, husda na mengineyo mengi)
Mkuu kuna kitu umenifungua hapa....kwanini nikishirikisha mambo yangu mazuri marafiki na hata ndugu zangu huwa yanaharibika/ yanatibuka??

Ila nikifanya kimya kimya natoboa[emoji15]

Ngoja nizidi kuwa msiri Dadeeki
 
Jambo jema linalofanywa kimya kimya au mahali pa siri ndo huwa na dhawabu(mibaraka) toka kwa MOLA ila kama ukiamua kulifanya adharan kwenye macho ya walimwengu utapokea dhawabu za walimwengu (wivu, chuki, masengenyo, vicheko, husda na mengineyo mengi)
Dawa ni moja:Kama ni mkristu RC ndoa ya asubuhi saa kumi na mbili ingeswihi zaidi.Au kwa muislamu ita sheikh akufungisheni nyumbani.Mnapata "mpunga" wenu na jamaa kiasi maisha yanasonga.Stress free harusi.Burdaaaniiii!
 
Lift ina gharama zake.Gari likipata pancha utapewa jeki utoe tairi.Rejeta ikileta rabsha unapewa gudulia ukachote maji na mpo Mikumi mbugani.Na ukiomba lift ukakuta mbele wamejaa(pick ups) ukubali kudandia kwenye bodi na mvua inanyesha.Tafakari
tambua hata kuoa bila mahali pia kunagharama zake maana kunakipindi ataumwa, matatizo kwao yatatokea etc. kwaiyo wakikupa bure kubali kikubwa unampenda!
 
Mke wangu mtarajiwa amekataa sherehe kasema tufunge ndoa turudi nyumbani tuendelee na ratiba kama kawaida....
 
Umeleta dukuduku,kisha ukatuachia na jibu lako.
Nadhani kichwa cha uzi kingebadilishwa Maudhui.
 
Nimewahi kuwa meneja wa kumbi za harusi kubwa tu hapa mjini.

Sherehe zote zinazo karibisha ndoa, harusi, send off , kitchen party na nyinginezo asilimia kubwa 85% ni michango ya watu. Matatizo hutokea kwenye michango, na mara nyingi ma bifu na viburi huibuka. Mtu asipo changa ndio mwanzo wa kutosalimiana na mahusiano huweza isha.

Wengi wa bwana harusi na bibi harusi asilimia kubwa unakuta mmoja wao ndie mwenye kipato cha wastani au mwajiriwa.

Tatizo linatokea pale ambapo Bwana harusi na bi harusi huingiza ela nyingi kutoka mifukonu mwao ili kufanikisha shughuli hizo kwa kukopa bank, jamaa nk

Kiufupi ni kwamba asilimia kubwa ya ninao wafaham na niliokutana nao wanaishi maisha ya tabu sana na huwezi amini ni huyu ndie alifunga harusi ya 40M. Wengi wao baada ya mazungumzo hujuta sanaa. Tukio la siku moja linakugharimu miaka 2-3 kwa kuishu kwa tabu sanaa.

Niliapa kabisa kamwe sita kuja fanya michezo hii ya kuigiza kama sina kipato kikubwa cha kuchezeaa. Mimi kama nitafunga harusi sinta mchangisha mtu yoyote hata sumni.
Pili harusi yangu haita zidi watu 50.

Asilimia kubwa ya wanao alikwa kwenye harusi ni wachangiaji, na wengi hutaka kuona ela yao waliochanga wanaifaidi vipi. Ikitokea tofauti kile anachokiona mezani hakiendani na ela aliyotoa majungu ndo huzalishwa hapa.

Harusi nyingi zina majungu, mara bi harusi hajapendeza, mara bi harusi sijui kabila gani, mara bi harusi kanunaa, mara harusi imepoaa, yanii ukumbini ni kuchoranaa tupuuuu.

Kwa ushauri wangu, vijana tusipende fame ya muda mfupi. Tusipende kufurahisha watu kwa muda mfupi alafu muda mrefu unagharamika wewe. Tusipende kuigaiga.

Kama huna uwezo wa hizi mambo, achana nazo, zinagharama sana, kuanzia kifedha hadi kisaikolojiaa.
 
Umeleta dukuduku,kisha ukatuachia na jibu lako.
Nadhani kichwa cha uzi kingebadilishwa Maudhui.
Haiwezekani kwenye mazungumzo kusitokee mabadiliko.Ilianza gharama za ndoa na sherehe yake sasa tunaipanua hoja kwa nakshi za hoja zingine.Hii ni tabia ya fasihi hasa ya uandishi na kuongea.
 
Haiwezekani kwenye mazungumzo kusitokee mabadiliko.Ilianza gharama za ndoa na sherehe yake sasa tunaipanua hoja kwa nakshi za hoja zingine.Hii ni tabia ya fasihi hasa ya uandishi na kuongea.
Sina shaka na hilo kaka,
Kichwa cha mada kinaonekana anatafuta majibu kutoka kwa wanajamvi, lakini pia wakati huo huo yeye katoa jibu la swali hilo hilo.
Ndio maana nasema kuna haja kichwa kubadilika ili kuchukua maana kamili ya mada..mfano: Harusi ipi ni bora kwako!?
Kwa kichwa hiki yeye anaweza toa jibu la swali lakini pia nafasi kwa wengine ikiendelea kuwepo kutoa majibu yao.
Tuko pamoja mkuu.
 
Back
Top Bottom