UTAFITI: Wanawake wanapenda harusi kuliko ndoa

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Jun 23, 2022
227
333
Je, umeoa au kuolewa, shughuli yako ya harusi ilikuwaje na nani alikuwa msuka mipango wewe au mume wako?

Nàam suala la kuoa na kuolewa limekuwa gumzo na muda mwingine kuleta mtazamo tofauti katika jamii.

Sio mara moja au mbili umesikia kuwa wachumba wameshindwa kuoana kwa sababu familia moja ya mwanamke au mwanaume kukomalia lazima ndoa iende na harusi.

Wazazi ama walezi au mtoto mwenyewe anae enda kuoa ama kuoelewa anaweza kukomaa kuwa hawezi kuingia kwenye ndoa pasipo sherehe ya ndoa yaani harusi lasivyo ataachana na mchumba na kutafuta mwingine ambae yupo tayari kufanya hivyo.

Kuna uchumba huvunjika kwa sababu mmoja wapo hayupo tayari kushiriki katika ndoa kwa mtindo wa sherehe ya harusi kwa sababu za Kiuchumi.

Muhusika au familia yake inaweza kuweka ugumu kuwa haiwezi kumudu gharama za sherehe ya harusi hivyo mwanao atafute mchumba mwingine ambae yupo tayari kuingia kwenye ndoa pasipo sherehe ya harusi.

Katika utafiti wa visa Kama hivi imebainika kuwa wanawake ndio hupenda kushiriki ndoa kwa mtindo wa harusi kuliko wanaume.

Utafiti unaonyesha kuwa wanawake huvutiwa zaidi na sherehe za harusi kabla ya ndoa yenyewe yaani maisha baada ya sherehe.

Kwa mujibu wa mtandao wa The Star Kenya unabainisha kuwa wanawake wengi hupenda ufahari wa kuonekana hivyo kutamani harusi kuliko wanaume.

Pia unabainisha kuwa wanawake hupendezwa na mipango ya harusi kuliko wanaume hivyo huchukua nafasi kubwa katika maandalizi ya shughuli mwanzo hadi mwisho.

Mavazi ya kupendeza, viatu vya bei ghali huwavutia zaidi wanawake kutaka harusi wakipata wachumba kuliko kufikiria mambo ya ndani ya ndoa yatakuwaje.

Bila shaka umeona mara nyingi harusi hufanyika kwa gharama kubwa yenye kupendeza lakini ndoa isidumu hata mwaka wanaachana?

Yote haya ni matokeo ya wanawake kutowaza maisha ya ndoa kipindi cha uchumba kwa kuangalia zaidi harusi pasipo kufikiria mapungufu na uimara wa wenza wao wanaotarajia kuingia nao kwenye ndoa.

Kwa mujibu wa utafiti Wanaume wengi hushiriki sherehe za harusi kwa ushawishi wa wanawake ni asilimia chache sana wanao amua wao wenyewe kwa hiari.

Hata wakishiriki hupenda kufanya mambo kwa urahisi mno jambo ambalo ni kinyume na matakwa ya wanawake.

Utafiti unagusa pia katika mafundisho ya ndoa kuwa wanawake wengi hukosa hamasa ya kuudhuria mafundisho ya ndoa na kuelekeza akili zao katika kufikiria Sherehe ya harusi itakuwaje, ni namna gani itasisimua jamii na kuonekana ni ya tofauti.

Matokeo ya utafiti huu yanaangazia mitazamo ya wanawake walioingia kwenye ndoa kwa mtindo wa harusi na uimara wa ndoa zao, utafiti unabaini kuwa wengi wao hawakupata maandalizi ya Kutosha kuhusu ndoa yenyewe.

Utafiti unabainisha kuwa wanawake wengine hulazimisha wenza wao kushiriki sherehe ya harusi ili kuwa Kama kifungo cha ndoa hiyo na kuweka uhakika wa wao kudumu Katika ndoa licha ya madhaifu yao kwakua sherehe hurasimisha uwepo wao katika ndoa husika na jamii nzima hujua hivyo.

Aidha jamii inatazamwa kubadili utamaduni wa kuwafunda watoto wao kuhusu ndoa na kuelekeza nguvu katika kushindana kuandaa sherehe za harusi za kifahari jambo ambalo halina maana kwenye ndoa husika iwapo wenza hawajui namna ya kuishi katika hali inayotakiwa.

Picha: Mtandao
Peter Mwaihola

Screenshot_20220824-083202.jpg
 
Nina jamaa yangu aligoma kbs kufanya sherehe mke mtarajiwa akavunja uchumba. Sasa hivi jamaa kaoa tena ndoa ya kanisani no sherehe zaidi ya kupata chakula cha jioni na kinywaji kwa watu wasiozidi 100. Mtaka sherehe bibie yupo kuhangaika kutafuta mtu wa kumuoa. Mimi napinga sana ndoa za sherehe ambazo ni kuumizana tu, fanya kitu kwa uwezo wako.
 
Nina jamaa yangu aligoma kbs kufanya sherehe mke mtarajiwa akavunja uchumba. Sasa hivi jamaa kaoa tena ndoa ya kanisani no sherehe zaidi ya kupata chakula cha jioni na kinywaji kwa watu wasiozidi 100. Mtaka sherehe bibie yupo kuhangaika kutafuta mtu wa kumuoa. Mimi napinga sana ndoa za sherehe ambazo ni kuumizana tu, fanya kitu kwa uwezo wako.
Kweli kabisa
 
Back
Top Bottom