Kundi la mapedeshee watatu waliotamba enzi za Kikwete!

("Wapi kizaizai")("wapi mpakanjia ")(" wapi George Mayenga")
=============
Wanamziki na wasanii mbalimbali hawakuacha kutamka maneno hayo!
Maneno hayo ni majina ya matajili marafiki watatu waliokuwa wanapenda sifa kupindukia!
Katika hao watatu, sijawahi kuona mtu aliyekuwa anapenda sifa kama KIZAIZAI....
Kwanza huyu jamaa miaka yote hakuwahi kumaliza ujenzi Wa nyumba yake zaidi ya kujenga na kubomoa halafu anajenga tena! (Ili Mradi tu aonyeshe anazo)
KIZAIZAI alikuwa akijenga nyumba hadi inakamilika halafu anaibomoa na kujenga tena. (Na Fundi aliyejitia kiherehere cha kumshauri kwamba wasivunje alijibiwa nafanya hivi ili nyinyi mpate kura! Nawalipa Pesa ya kujenga na kubomoa na kujenga tena)

KIZAIZAI Aliwahi kujaribu kubadilisha jina la mtaa mzima uitwe jina lake (KIZAIZAI STREET)
Aliagiza order ya ndoo za rangi toka kiwandani zipakwe kila nyumba mtaa mzima, Kwa madai kwamba mtaa mzima ufanane na hadhi yake kutokana na wageni wanaomtembelea, pia aliweza kupendekeza mtaa mzima upandwe miti mirefu miashoki!
KIZAIZAI hakupenda kukaa na gari aina moja Kwa siku tatu anabadilisha!
KIZAIZAI alikuwa akigawa fedha hususa bandi na wanamziki walipompaisha! Na wale wote walioshangilia walipata fedha!
KIZAIZAI Alipatwa hadi kuimbwa na Diamond katika wimbo wake Wa "kizaizai"
KIZAIZAI sasa kamaliza UJENZI Wa Nyumba yake awamu hii na hataki kubomoa tena!!
View attachment 645110
Mwabie abomoe ajenge Tena.!!!!?
 
sasa kama unawafahamu wanapiga dili haramu si uende ukatoe taarifa polisi kama raia mwema..
Musofe yuko nje, Ndama yuko nje, Kizaizai yuko nje, Muzamir yuko nje, Jack pemba yuko nje, Masawe yuko nje na wengine weeengi wako nje sasa utatuambiaji wanapiga dili haramu wakati hata mahakama imewaachia huru ndama na Musofe...
Siyo kila aliyeko nje ni raia mwema na si kila aliyeko ndani ana hatia...
Wanaopigwa wenyewe wakitoa taarifa hawasaidiwi.
Haijapita hata miezi sita kapigwa mzungu flani mmoja wa wahusika kakamatwa kawekwa ndani kawatembezea mlungura wa mls 80, kaachiwa kaondoka yuko nje now.
Mzungu anabaki analialia tu we unasema polisis.
Huyo mhusika walimtoa kwenye gazeti la mwananchi alipokamatwa lakini alipoachiwa hawakutoa habari zake, kanyoa upara na ndevu kubadiri mwonekano kasepa zake ukizingatia naye hakuwa mtz
 
Kizaizai kasinyori mwenyewe lbda utawala mwengine ndio anaweza rejea kwenye tambo zake.
 
Kuna yule aliekua anasimamisha hummer lake jeusi pale K/koo nahisi papaa faru dume hivi yupo wap? Na huyu jamaa Ndama mutoto ya Ng'ombe si alikua na ile pesa ya utakatishaji? Vp alichomoa?.
Son of cow alilipa fine akachomoka.. Hela sio kuzuri
 
Safi sana, ilikuwa shida mtaani, mwenye hela halali hatesi kihivyo, mifano ipo...
Wako tuli kama maji ya mtungini...
2a728131ced4755aaab9f517f98cb8f7.jpg
 
Back
Top Bottom