DOKEZO Moshi: Mwalimu anayehisiwa Kufichua Maovu ya Afisa Elimu wa Manispaa awekwa LOCKUP na Afisa Elimu huyo (Ndg. Ngonyani)

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
YAH:- MWALIMU CALVIN TWARILA WA KIBO AACHIWE HURU ANAONEWA!!

NAWEKA USHAHIDI WA MAOVU YOTE YA NGONYANI!!

Somo tajwa hapo juu lahusika.

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa viongozi wote waliolisimamia suala letu walimu!Nianze na ofisi ya Rais, Wizara ya Elimu Tamisemi, Ofisi ya Takukuru, Usalama wa Taifa, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Wilaya! Ukaguzi kanda na Dawati la jinsia na watoto kwa kazi kubwa mliyoifanya! Kweli serikali yetu ipo makini na inajali wananchi wake kwa kutatua kero zao kwa haraka!! Asanteni sana!

Niliwaaga ila kwa haya yanayoendelea nimeona nirudi kuwajuza wakuu wangu! Mtanisamehe sana kwa haya nitakayoongea, ni katika kuiweka Manispaa ya Moshi sehemu salama kutoka katika uzembe, unyanyasaji, ukatili na dhulumu wanazofanyiwa watumishi wa umma!

Viongozi wangu imeniuma sana walimu baadhi wasiohisiwa katika kutoa maandishi haya wanawekwa lockup bila sababu na kutishiwa kuuawa!Kwahiyo kusema ukweli ni kosa la jinai!sasa leo nitaweka wazi kila kitu..!

1: Afisa Elimu huyu anakamata ovyo walimu na kuwaweka ndani kupitia marafiki zake ambao ni maaskari; haki ipo wapi? Yeye angesubiri ukweli ubainike! Amemuweka ndani Mwalimu wa Kibo anaitwa Calvin Twarila leo ni siku ya sita kwa kumhisi tu kuwa ametoa tamko! Yeye ndiye alitakiwa awepo lockup muda huu na sio walimu wasiojua kitu!

2: Ameenda kusafisha bastola yake kwamba atakapombaini mhusika amuue! Huyu jamaa yupo sawa kweli? Anaita walimu ofisini kwake na kuwahoji pia kuwatisha kuwa ataua mtu!! Hivi anajua sheria za nchi? Kutishia ni kosa kisheria! Anachokikwepa ni nini wakati walimu wamesema ya moyoni na ukweli wote utabainika kupitia dodoso zilizotoka TAMISEMI.

3: Anajisifu kwamba yeye hawezi kuondoka Manispaa ya Moshi na hakuna wa kumtoa wala kumgusa! Anadai kuondoka kwake hapo ni kupanda cheo! (na rekodi ipo aliyorekodiwa akitoa matamshi hayo tutaweka hadharani)!

4: Ushahidi upo wa yote niliyoyabainisha upo wazi naweka baadhi ya shahidi zangu zisizokuwa na shaka hadharani: Handeni amejenga nyumba nne(4) kwenye compound moja kwa ndani ya muda mfupi na kununua magari manne ya gharama! Je, yeye mtumishi wa umma katoa wapi fedha hizo kama sio za wizi na utapeli wa miradi na kuomba walimu wakuu na waratibu (wachukue miamala yake ya 2021-2023).

5: Mkuu wa shule ya Msingi Magereza Aniseth Kileo alikamatwa na mkuu wa gereza la Karanga akihamisha mali ya umma ikiwepo mabati, saruju, mbao na vifaa vya ujenzi; alipoulizwa akasema kaelekezwa na huyo fisadi mdogo Ngonyani. Akaulizwe, taarifa zipo pale! Mali za shule unahamisha unapeleka wapi? Hata walimu wa shule ya msingi Magereza wanalijua hilo!

5: Kuna fedha zilipelekwa shule ya msingi Magereza za miradi za shule ya msingi Njoro EP4R ..why fedha hizo zipelekwe Magereza ilhali hata shule ya Msingi Njoro ina Akaunti? Nawaambia ukweli ni katika upigaji wa hizo fedha! Eti ukitaka kununua vifaa anayesaini ni mkuu wa shule ya Magereza ambaye ni rafiki mkubwa wa Ngonyani. Fuatilieni miradi ya Magereza vs Njoro. Lile lilikuwa lango kuu la wizi wa fedha za umma..!

6: Huyo huyo mkuu wa shule ya magereza akishirikiana na boss wake wamezimiliki nyumba za shule mbili za shule ya msingi Magereza wakishirikiana kuwahamisha walimu waliokuwa wanakaa hapo na hizo nyumba moja kufanya danguro ambapo Mkuu huyo wa shule amemuweka kimada wake Mwalimu Elizabeth na huyo boss wake Ngonyani akipata Mwanamke hapo ndipo guest yao! (Abanwe huyu mkuu siri zote anazijua! Waulizeni Mwalimu Marygorate M. wa uhuru na Jackline M. wa Shaurimoyo kilichowakuta shule ya Magereza. Tena kuna walimu wengine waligomea kuhama! Walimuhamisha mama wa watu anaitwa Irene C. na kumpeleka shule ya Shirimatunda ili aachie nyumba lakini mama huyo alichoka uonevu akaenda kupiga kelele pale Manispaa akiwa na baba yake mgonjwa aliyefariki baadae kwa manyanyaso hayo (mtafuteni huyu mama).

7: Atafutwe Mwalimu mkuu wa Chemchem anaitwa Mashauri awaeleze anachopitia sasa baada ya kunyimwa mradi wa Covid 19 wa madarasa manne kwa kukataa kutoa mlungula alioombwa na huyu Ngonyani! Alitaka milioni mbili lakini Mwalimu Mashauri akatoa elfu ishirini, matokeo yake mradi wa covid haukupelekwa shuleni kwake ukapelekwa shule ya Msingi Langoni! Nendeni Langoni mtajionea

8: Lile jengo la SACCOS ambalo lipo katika eneo la shule ya msingi Uhuru, afisa elimu Ngonyani na timu yake wamechukua mkataba wa milioni mia mbili (200Mil) na kukabidhi eneo la shule kwa Saccos ili wajenge ofisi zao. Je, hii ni haki kuuza sehemu ya Shule? Na je hizo pesa zimeingizwa wapi? Kwenye akaunti ipi?

9: Kuna miradi imepelekwa shule ya Msingi Uhuru ya kujenga Ukumbi wa starehe! Jamani hivi hizo pesa kuna upungufu mkubwa wa madarasa wao wanaenda kujenga kumbi za starehe kweliiii? Tunakwamisha kwa makusudi Mama yetu Mpendwa Samia Suluhu Hassan katika jitihada zake za kuondoa uhaba wa madarasa wao wanajenga kumbi!!walimu walipohoji wakahamishwa mmoja kapelekwa shule ya Shirimatunda wafuatilieni walimu hao!!

10: Kuna walimu wamenyanyasika sana! Mwalimu Mkuu wa Njoro aliyehamishwa kwenda Pasua anaitwa Brigeti. Kuna Mwalimu Hando mpaka leo anapokea nusu mshahara mwaka wa tatu sasa!alitengenezewa zengwe la Mwalimu mkaidi baada ya kuchoka kuhamishwa hamishwa na kukataa ufisadi wa huyu boss Ngonyani wa kutaka kugawana fedha za uhamisho! Pia aliwahi kutolewa vyombo vyake nje kwenye nyumba ya shule pale Shirimatunda na vyombo kupelekwa bohari la serikali. Huu ni unyanyasaji mkubwa sana! Afisa Elimu Kata Theodora kisa katofautiana na boss akahamishwa. Kuna Mwalimu Jackline, Mwalimu Mary, Mwl Kiwale wa Kibo, huyu sasa mpaka leo kanyimwa mshahara kwa miezi mitano sasa kisa ana bifu na Ngonyani na wana mpango wa kumfukuza kazi kabisa! Wakati kuna walimu walevi kupindukia, watoro waliokithiri wengine walipoteaga miaka mpaka mitatu na wapo kazini why huyu !walimu? Wabakaji kama yule wa shule ya Msingi Muungano aliyebaka mwanafunzi pale shule akakutwa matokeo yake akahamishwa kwenda Msandaka au Msaranga kama sikosei wameachwa sasa wanataka wamfukuze kazi huyu Mwl Kiwale wakati alipata matatizo ya mirathi ya baba yake yeye akiwa kama msimamizi. Taarifa zote tunazo hakuna Mwalimu wa Moshi asiyejua hili tatizo la Afisa Elimu na huyu Mwalimu..walimu hawa watafutwe

11: Atafutwe dereva aliyekuwa anamuendesha huyu Afisa Elimu na aseme kilichomfanya akamkataa huyu boss! Haiwezekani wewe ulitumie gari la ofisi kufanyia ngono humo ndani na kumuamrisha dereva asubiri nje mpaka umalize haja zako! Je, ni sahihi kwa mtu mzima kama yule kupeperushwa? Ilifika wakati alichoka akakataa kuendesha hilo gari na kupelekea kumuweka mtu wake ambaye ndipo wakaenda kuliangusha gari la Serikali likapotelea huko mpaka leo.

12: Atafutwe Afisa Elimu Taaluma anaitwa Urasa amekuwa mhanga wa haya matatizo ya unyanyasaji! Yule boss wetu Mungu amlinde, amekuwa akijitoa sana kutafuta haki za walimu na hata kuipaisha taaluma lakini ndio kawa chungu ya boss na kutaka kumng'oa hapo ofisini.. Boss Ngonyani ameshaandika notice nyingi TAMISEMI kutaka aondolewe lakini busara za viongozi wetu wa TAMISEMI zilitumika.

13: Huyu Boss Ngonyani anashiriki kuwabadilishia walimu home of domicile ili kupunguza fedha wanazolipwa kwaajili ya nauli..sasa cha kuchekesha katika mafaili inaonyesha ile ya awali lkn mwalimu anapewa barua isiyo rasmi ya kubadilishiwa..hapo kuna upigaji wa fedha za walimu za nauli kwa kutumia janja hiyo!!kagueni malipo ya nauli mwaka huu na mwaka jana walimu wengi wameumizwa hapo !!je ni sahihi mwalimu kubadilishiwa home of domicile bila kumshirikisha??ushahidi upo wa walimu hao!!

14: Kuna wanafunzi walilawitiwa wakiwa tisa (9) shule ya Msingi Chemchem na mtu anaitwa babu Yahaya, kesi ilisimamiwa vizuri na Mwenyekiti wa Mtaa wa Sokoni na Mratibu kata wa kipindi hicho bwana Kiwale wakamkamata mhusika na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria na mpaka kesi ikaenda mahakamani, walilisimamia mpaka saa nane usiku majibu yakatolewa na watoto wanne wakathibitika kuingiliwa na kulawitiwa! Lakini huyu boss alipokea rushwa ya shilingi milioni tano na kesi ikaishia hapo na Huyu Mwalimu Kiwale ambaye alikuwa afisa elimu kata akatengenezewa zengwe na kushushwa cheo na kwenda kufundisha shule ya Kibo! Fuatilieni hii kesi mtuhumiwa yupo mtaani anaendelea kuharibu watoto wa watu.

Kwa leo nawashukuru sana naomba Mungu awatangulie na pia Mwalimu Calvin aachiwe huru kabla hatua zingine hazijachukuliwa.

Ameen amani ya Bwana itawale katika anga ya Moshi Manispaa!

Mwalimu Mazalendo.
 
Tumekusikia tutamchukulia hatua kali za kinidhamu ikidhibitiika ni kweli ni swala la muda tu
 
Why I hate ajira?

Ukitishiwa unaogopa na huwezi jisemea ukakimbilia humu, mie bwana sijawahi tishiwa, najua haki zangu, na ugali wangu siupati kwa afisa elimu...

Poleni sana, ajira na mazingira ya walimu wetu ni mateso sana, watafanyaje na lazima wale? Jishughulisheni na tu miradi tutawapa kujiamini.
 
Tatizo la watanzania wajinga ni wengi mtu katoa vielelezo vyoote anakuja mpumbavu kamaliza secondar ana simu touch anatoa comment eti majungu hayo, mwingine stupit anasema. DED yupo, ofisa usalama yupo, sijui nani yupo. shubamit, kwani wakiwa hao woote wapo uonevu haufanyiki akiwa je ni washikaji wake si anafanya upumbavu wowote?

Kwani Magufuli alivyokuwa akipita njiani watu walikuwa wakimlalamikia shida zao na alikuwa anawaita wote hao uliowataja na kuwailiza mbona mnashindwa kutatuwa kero za wananchi wakawa wanatumbua macho kodo
 
Mmmmmm waalimu tena! Nchi imejaa vituko hii yaani Afisa Elimu ana uwezo wa kumweka mtu ndani?nchi hii nani mwenye jukumu la to arrrest a suspect?,wapi ile sheria ya kutumweka mtu ndani bila ya docket?,vipi kuhusu zile 48hrs zikipita ni lazima suspect afikishwe kwa court of law au aachiliwe?

Why waalimu wote wanashindwa kufanya push back against one guy? Na matokeo yake ni kulalama ndani ya JF, pls mtoa hoja haki haiji in a golden plate, haki inakuja kwa ku fight back ili kudai haki, ni LAZIMA watu wengine wafe ili haki ipatikane kinyume cha hapo utaishia kulalama,binafsi pia ni mwalimu wa kusomea ila nilishasema NO kuwa mwalimu.

Ninakushauri jiendeleze kielimu hata ukiwa na Bachelors na tafuta passport, kajilipue Namibia, Botswana, Lesotho ualimu unalipa kule au far east ukafundishe English, good luck
 
Kwani Afisa elimu ndio hatua ha mwisho ya mwisho ya maamuzi?

Nyie walimu wenzetu wa idara ya msingi mnatuangusha sana walimu.Afisa elimu sio muajiri wako.Hata DED akizingua kuna mamlaka za juu yake.shuda yenu huwa mnawaona maafisa elimu kama miungu wangu.ushauri kwa walimu walioonewa:

1. Waende kwa TSC
2. Kama Tsc hawatatia ushirikiano waende kwa DED
3. Kama DED hatatoa ushirikiano waende TAMISEMI
 
Hapo CWT wapo na wanayaona hayo yote ila wamejiziba masikio halafu eti kinajiita chama cha kutetea walimu,

Halafu kama hayo yanayosemwa ni kweli afisa elimu anapata wapi mamlaka ya kumuweka ndani mtumishi wa umma?
Exactly mkuu hasa hiyo paragraph yako ya mwisho, ni POLICE tu mwenye arresting power, tuamke watanzania
 
Mmmmmm waalimu tena!nchi imejaa vituko hii yaani Afisa Elimu ana uwezo wa kumweka mtu ndani?nchi hii nani mwenye jukumu la to arrrest a suspect?,wapi ile sheria ya kutumweka mtu ndani bila ya docket?,vipi kuhusu zile 48hrs zikipita ni lazima suspect afikishwe kwa court of law au aachiliwe?,why waalimu wote wanashindwa kufanya push back against one guy?na matokeo yake ni kulalama ndani ya JF, pls mtoa hoja haki haiji in a golden plate, haki inakuja kwa ku fight back ili kudai haki, ni LAZIMA watu wengine wafe ili haki ipatikane kinyume cha hapo utaishia kulalama,binafsi pia ni mwalimu wa kusomea ila nilishasema NO kuwa mwalimu, ninakushauri jiendeleze kielimu hata ukiwa na Bachelors na tafuta passport, kajilipue Namibia, Botswana, Lesotho ualimu unalipa kule au far east ukafundishe English, good luck
Tatizo jeshi letu la polisi lina njaa sana hivyo ni rahisi tuu huyo afisa elimu kuhonga askari na askari wakamtengenezea kesi huyo mwalimu wakamkamata na kumuweka ndani maana sheria zetu ni kandamizi sana kwa raia
 
Back
Top Bottom