Kuna watu wana hela jamani!!

Huyo atakuwa na Mgodi wa Almas
 
Wakati napiha zangu A level pale aza boys nilikuwa na goma langu la kiarabu pale kariakoo, kwao wana House girls watatu, wawili wanakuja na kuondoka mmoja anakaa pale pale, ukiangalia sasa familia yenyewe kuna mama, baba tayari r.i.p, kaka zake wawili, mmoja ana mke na yeye binti!! Nikastaajabu kidogo.. Miaka imesonga mbele tuliachana baada ya mimi kumtia mimba binti mwingine ye kwa hasira akaolewa tukaja kupatana km washikaji tu, akanialika kwake yupo yeye na mwanae mume wameshakorofishana,lakin ana mabeki3 wawili.

Nikikumbuka familia zetu kuna baba, mama watoto 8, mjomba, sijui babu, bibi mzaa baba, bibi mzaa mama. Na beki 3 hamna au sana sana yupo mmoja kama roho..
Hahaa!! Maisha hayako sawa kabisa.
Mie nazaliwa kwa mtogole, au zamani kurasini maji machafu mmoja anazaliwa kwenye shortcut kwa bakhresa, mtoto wa miaka 2 ana account ina soma m mia kadhaa, mimi na miaka yangu 50 kasoro nina akaunti ya mpesa, benki nina kadi ya ushahidi wa benki!! Ikiingia pesa haikai inapitiliza..
 
Hao jamaa ni wafanya biashara wa nini hapa bongo mana wanaonekana kwa siku hawakosi milion angalu 50
 
Pumbavu kabsaa sasa Si najenga yangu hela zote hizo??
 
kuna watu ukisimulia maisha yao unaweza onekana unaongeza chumvi..kuna watu wana kufuru hiii DUNIA acheni kabisa
 
Unafika kwa mtu unaogopa mpaka pakukaa utachafua..

Bongo hii hii kuna watu wanaishi maisha ya kufuru mkuu
nakubaliana na wewe kabisa...nilishaingia Nyumba unakaa kwenye kochi umeshakaa lakini unajiona kama uko hewani unaning'inia bado...nilitegea wenyeji wameniacha kidogo Nikainuka tena nikakaaa..Bwana weeeeee yale sio masofa ila ni Kufuru sjawahi yaona popote walai...

Hamna hata kitu kimoja humo ndani ya nyumba nimewahi kukiona popote tv Jina lake silijui yani Mzeee Tanzania anaesemaga ni nchi maskini Ajifikirie sana sana na hajazunguka vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…