Kuna wanajeshi Watanzania Iraq?

Jasusi

Badala ya kusema tusiweke conclusions za kuwa huyo ni Mtazania. Hebu tupe japo idea zako kidogo kwa nini huyu jamaa amevaa bendera yetu???

Wengi hapa tupo open minded, ila tuna hamu sana ya kupata vielelezo vyenye mashiko.

Maandishi yana nafasi ndogo sana kulinganisha na picha.

Yebo Yebo,
Hiyo patch nilikuwa sijaiona. I take it back.
 
Folks,
Let us not jump to conclusions. Unless wamemtaja kuwa ni Mtanzania nijuavyo mimi Mu7
alipeleka wanajeshi wake kule kuungana na coalition of the willing.

Ni kweli mkuu.unajua siku hizi heading zikisomwa tu tayari mtu anajadili mada akiwa katika mood za conclussion.Hilo ni tatizo kubwa.

Pia,kama kweli kuna mwanajeshi hata mmoja mtanazania yuko huko basi serikali inabidi iwajibike
 
Katika swali la msingi ndani yake kuna swali jingine ambalo naamini linapaswa kuulizwa na ambalo laweza kutoa jibu:

a. Je kuna mwanajeshi yeyote wa Marekani mwenye asili ya Tanzania anayepigana Iraq? Jibu la swali hilo kwa kadiri ninavyojua ni ndiyo. Wapo vijana wachache wa Kitanzania waliojiunga na jeshi la Marekani na sasa hivi/wamewahi kupigana Iraq. Hawa sasa hivi ni Wamarekani au wako mbioni kuupata uraia wa huku (Kumbuka kujiunga na jeshi la Marekani siyo lazima uwe raia, unahitaji kuwa na Permanent Residence). Je yawezekana huyo ni mmoja wao?

b. Je kuna askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ambaye anashiriki mapigano Iraq chini ya Jeshi la Marekani au pamoja na Jeshi la Marekani? Nina majibu mawili. Inawezekana, chini ya mamlaka ya Kikatiba ya Rais ambayo tumempa nguvu ya kumuamuru mwanajeshi yeyote kutekeleza majukumu fulani ndani au nje ya nchi. Katika nguvu hiyo ya Kikatiba Rais halazimishwi kulijulisha Bunge deployments ya troops wetu.

Jibu la pini ni hapana kwani kwa kadiri ninavyofahamu Tanzania haina mkataba wa kusaidiana vitani kijeshi na Marekani. Kama mkataba huo upo ni lazima Bunge lingepaswa kujua. Kwa vile Dr. Slaa yuko kwenye mtandao anaweza kuuliza swali hili siku ya Alhamisi kwa Waziri Mkuu.
 
Mimi naona nyote hamjui vizuri bendera ya nchi....hivi wapi kuna mstari mwekundu katika bendera yetu hebu angalieni picha vizuri ni rangi tu zinafanana lakini huo mstari mwekundu ndio unatofautisha na bendera yetu.
 
This is news to me!!!

Nimejaribu ku-search for details about our military uniform na nimegundua kwa kawaida sisi hatutumii flag patch na iwapo tungetumia flag patch ingefanan hivi kutokana na toleo ya Equestrade group ambayo ina toa huduma ya military acessories
flag_tanzania_gb_large.jpg


ila sasa it is still questionable maana nao pia wanatoa flag patches kwa nchi zingine amabzo hazina jina la nchi kama vile tulivyoona kwenye picha.

Marekani huwa wanaweka flag patches kwenye uniforms zao. Kwa kuwa ni vita vya kimataifa lazima allies wao wawe na flag patches for identification purposes. It amazes me kuona watanzania tunapigana huko na mbaya zaidi tunaitwa waIraq?? It does not make sense. Tafadhali tupewe majibu hapa
 
Mimi naona nyote hamjui vizuri bendera ya nchi....hivi wapi kuna mstari mwekundu katika bendera yetu hebu angalieni picha vizuri ni rangi tu zinafanana lakini huo mstari mwekundu ndio unatofautisha na bendera yetu.

Nimejaribu kuikuza picha hiyo lakini ikashindikana naona pia kuna issues ya pixels. Ila nahisi hiyo rangi unayosema ni vumbi. ngoja nirudie tena kuitazama upya.
 
Mimi naona nyote hamjui vizuri bendera ya nchi....hivi wapi kuna mstari mwekundu katika bendera yetu hebu angalieni picha vizuri ni rangi tu zinafanana lakini huo mstari mwekundu ndio unatofautisha na bendera yetu.

Hiyo haiko clear kama ni nyekundu au nyeusi iliyopigwa na jua, nyekundu ingekuwa inaonekana hivyo zaidi.

Inawezekana Wa Iraq wanavaa bendera za unit zao, inawezekana hii inafanana na ya Tanzania.Inawezekana Photoshop.
 
Kwa nini nisiamini hii imekuwa photoshoped?
Ina maana watu wa yahoo ndio wame-photoshop hii picha?? Na kwa nini waamue ku-photoshop bendera ya Tanzania na sio Kenya au Uganda. Hii sio photoshop.
 
attachment.php

Ukiingalia nembo ina kivuli na hii haijawa photoshop kabisa tunawaomba waheshimiwa Hamad Rashid na Slaa waandae hoja mapema leo kesho waiwasilishe bungeni wananchi tupate maelezo ya kina wanajeshi wetu wamefikaje Iraq (pesa bwana zitatumaliza)

Tunakupa pole kamanda kwa hiyo ajali
 
Mimi naona nyote hamjui vizuri bendera ya nchi....hivi wapi kuna mstari mwekundu katika bendera yetu hebu angalieni picha vizuri ni rangi tu zinafanana lakini huo mstari mwekundu ndio unatofautisha na bendera yetu.

Fidel ndugu yangu, Kamuone daktari haraka iwezekanavyo maana hiyo rangi nyekundu ndugu yangu haipo. Au labda uliruka darasa la kupaka rangi nursery school. Maana niiangalia elimu ya chekechea ya nyumbani, crayons hamna tunabaki kuimba namba na imla kutwa!
 
Huu uzee nao sasa unatuchanganya, macho hata hayaoni sawasawa. Hii katikati ni nyekundu au nyeusi?
 
attachment.php

Ukiingalia nembo ina kivuli na hii haijawa photoshop kabisa tunawaomba waheshimiwa Hamad Rashid na Slaa waandae hoja mapema leo kesho waiwasilishe bungeni wananchi tupate maelezo ya kina wanajeshi wetu wamefikaje Iraq (pesa bwana zitatumaliza)

Tunakupa pole kamanda kwa hiyo ajali

kuna wairaq ma blacks?
i can see the guy is black japokuwa anavumbi sana
 
web page ya yahoo inayobeba hiyo picha inaonekana kama hivi ifuatavyo!!
je ni photoshop hii?
 

Attachments

  • Doc1.doc
    355 KB · Views: 76
Hiyo ni photoshoped na nitawaeleza kama nilivyowaeleza kuhusu ile picha ya Mwanamama wa CUF alionekana kulala bungeni ,ila hapa inataka uone tofauti ya kivuli ,kitu ambacho wengi ya wanaotumia photoshop huwa wamejawa na jazba na factor hii ya kivuli huwaumbulisha vibaya sana.Nimegundua kuna kivuli kwa chini ya bendera kitu ambacho kisingekuwepo kwani huwa bendera imeganda na si yakutoa kivuli,vilevile ukitazama juu ya bega kuna kikoti ambacho kwa jinsi ya kivuli cha bendera kilivyoangukia basi na lile pango la kikoti ambalo ni kubwa nalo lingetoa kivuli kilichokaribia nje kabisa lakini kinaonekana kivuli chake hakipo kimemezwa kwa ndani.
Jengine huyo jamaa ni mzungu kutoka kikosi cha mizinga au kwenye magari ya deraya na ukitaka kumuona uzuri ,copy the properties of the picture .itaonekana kama inavyofuata bila ya mabano { http://www.} jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=1967&d=1218536045
na paste kwenye bar halafu kama unatumia explore 7 and above unaweza kuikuza picha mpaka kwenye 400% chini mkono wa kulia wa browser yako kipo kinakuwepo kitendea kazi hiyo ,unauona upande wa uso wa huyo jamaa kuwa ni mzungu na si mwafrika japo wapo waafrika weupe.
Rangi zetu nyeusi zinafanana na kivuli hivyo kusingetokea alama yeyote ya uso kama sikio na rangi nyeupe kwenye sehemu za mashavu au shingo ambayo imejifichaficha,halafu sidhani kama wabunge watauvaa mkenge wa kwenda kuuliza suala hilo itakuwa nao hawana muelekeo wanakotomezwa ndio huko huko.
 
Kwanza kwa nini uamini au usiamini? Wewe si hukubali haya mambo ya 'imani'....?


Nilishakwambia kuhusu kuamini katika kuamini, au kutoamini katika kuamini na kutoamini katika kutoamini au kuamini katika kutoamini au hata kutokuwa katika kuamini katika kuamini au kutoamini katika kuamini pamoja na kutoamini katika kutoamini na kuamini katika kuamini ukasema yaishe.

Sikukwambia kwamba naamini au siamini, nimeuliza kwa nini nisiamini, which in reverse is kwa nini niamini.

Ndiyo maana nikakupa majibu kibao, inaweza kuwa hii au ile au ile, speculations tu hapa, hamna facts.Mimi siamini katika kuamini, na siamini katika kutoamini.Nataka kujua. However this is a typical Selassian illusion, an ideal to be pursued, but never attained.
 
Back
Top Bottom