Kuna umuhimu gani wa kujiunga na JKT kwa Mujibu wa Sheria na asipojiunga nini kitatokea?

Kujiunga na Jeshi si Vibaya Maana Kule Unajifunza UZALENDO,Ukakamavu,Kumbuka ni JKT (Jeshi la Kujenga Taifa) Means Yapo Mengi Utajifunza Unapokuwa Kule.
Pia Utajifunza Baadhi ya Mbinu za Kijeshi,Gwaride,Uzalishaji Mali,Kujitegemea,Ushirikiano,Pia Utaijua Silaha na Kuitumia Na Mengine Mengi.
Binafsi Nilipangiwa Mwaka 2014 Mtabila KJ.
Nilijifunza Mengi Mno,Pia Waweza Pata Chance Ukiwa Kule Ukajikuta Umeingia Kwenye System.

Ni Maamuzi Yako Kuongeza CV au Kuacha.
Ningekushauri Ujiunge.
Na nisipo jiunga kuna tatizo ??
 
Usipoenda jkt utakosa kazi za ulinzi maana it's such a shame kwa Bongo hizo ndio type za kazi wanakuuliza kama umepitia ulinzi, nenda JKT ukitoka karibu tukalinde usalama wakulipia.
 
Ilishapitisha bila cheti cha jkt form six ukienda kuomba kazi baada ya kumaliza kama huna no kazi
Kakuongopea nani? Unajua Kada zipi zinataka kigezo cha JKT ni just added advantage kwa Mtu ambaye ataomba nafasi ya Security officer wa Taasisi fulani and not otherwise.
 
Acha uoga nenda karipoti bana mbona madem wanaenda na wanarudi sembuse we kidume msee.

Kunafaida za kwenda jeshi,
jeshi litakujengea patience, confidence na uzalendo, pia unakutana na watu wengi na kwa muda mchache unatengeneza marafiki .....

2018, kanda yetu ilikua ni kanda ya usaili wa vijana kuingia chomboni, washkaji weng wa PCB, PCM na PGM na CBG walichukuliwa kujiunga na jeshi, weng ni wanajesh now na baadhi yao wako Russia, na nchi zingine wanasomea officer cardet.

Huwez jua labda kanda ya kati ulopangiwa inaweza kuwa kanda ya usaili mwaka huu

Lkn kama unaishu ya maana ya kufanya mtaani ya HELA INAYOELEWEKA usiende Ila kama hauna cha kufanya mtaani nenda KUNAFAIDA SANA.

2018 mpaka tarehe 17/6/ nilikua nimekataaa kwenda Ila baada ya kwenda sometimes huwa napakumbuka.
Acha kuogopa mwanang nenda afu makutopora hamna tifu kivile.
 
Wadau nipo mbele yenu

Mwanangu kamaliza form 6 mwaka huu kachaguliwa ahudhurie mafunzooo ya jeshi kwa mujibu, lakini mwanangu hataki jeshi.

Je, asipohudhuria hayo mafunzo kuna madhara gani atapata au atakosa chuo au atakosa Kazi?
 
Wadau nipo mbele yenu wana FB .mwanangu kamaliza form 6 mwaka huu kachaguliwa ahudhurie mafunzooo ya jeshi kwa mujibu ..lakini mwanangu hataki jeshi...
Je asipohudhuria hayo mafunzooo kuna madhara gani atapata au atakosa chuo au atakosa Kaz ???
Hakuna madhara zaidi ya kuendelea kuwa mvivu.
 
Nenda Mkuu hata baadaye ukiamua kuwa muasi haitosumbua sana. Binafsi najuta kwanini sikwenda Kwa kuwa Kwa sasa nafikiria sana kuasi
Nalog off
 
Kujiunga na Jeshi si Vibaya Maana Kule Unajifunza UZALENDO,Ukakamavu,Kumbuka ni JKT (Jeshi la Kujenga Taifa) Means Yapo Mengi Utajifunza Unapokuwa Kule.
Pia Utajifunza Baadhi ya Mbinu za Kijeshi,Gwaride,Uzalishaji Mali,Kujitegemea,Ushirikiano,Pia Utaijua Silaha na Kuitumia Na Mengine Mengi.
Binafsi Nilipangiwa Mwaka 2014 Mtabila KJ.
Nilijifunza Mengi Mno,Pia Waweza Pata Chance Ukiwa Kule Ukajikuta Umeingia Kwenye System.

Ni Maamuzi Yako Kuongeza CV au Kuacha.
Ningekushauri Ujiunge.
Uzalendo in dhana pana huwezi jifunza uzalendo kwa miezi mitatu,
Hii ni long term behavioral change process ambayo inabidi ianzie kwenye ngazi ya familia na siyo vinginevyo.
 
Jeshi ni kama added Cv. Binafsi nilikuwa naogopa sana kwenda jkt lakini baada ya kutoka pale hakika niliikumbuka Maramba Jkt kijana kama umechaguliwa kujiunga na jkt usipoteze hiyo fursa. Na km wakiume alafu unaogopa na wakati huna kazi ya kufanya nyumbani nadhani ww ni fala tu
 
Uzalendo in dhana pana huwezi jifunza uzalendo kwa miezi mitatu,
Hii ni long term behavioral change process ambayo inabidi ianzie kwenye ngazi ya familia na siyo vinginevyo.
Uko Sahihi,Ila Nimesema "Utajifunza" Meant Kashajifunza Ps Level & Sc Level JKT ni Mwendelezo!
 
Back
Top Bottom