Kwa mujibu wa sheria ukifanya mambo haya haihesabiki kama umefanya uchochezi

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Kwa mujibu wa kifungu cha 55(2) cha Kanuni za Adhabu Sura ya 16, kitendo hakiwezi kuhesabiwa kama kufanya uchochezi ikiwa umefanya mambo haya;

(a) Kuonyesha kwamba serikali imepotoka au imekosea katika mwenendo wake wowote;

(b) Kuonyesha makosa au mapungufu katika serikali au Katiba ya Jamhuri ya Muungano au kama ilivyowekwa na sheria, au katika usimamiaji utoaji wa haki kwa lengo kurekebisha makosa hayo au upungufu huo;

(c) Kuwashawishi wakati wowote wakazi wa Jamhuri ya Muungano kujaribu kwa njia ya halali kuleta megeuzo ya jambo lolote katika Jamhuri ya Muungano kama ilivyowekwa kwa sheria;

(d) Kuonyesha, kwa nia ya kuvifuta, mambo yoyote yanayoleta au yenye mwelekeo wa kujenga hisia za nia mbaya na uadui baina ya aina mbali mbali za watu wa Jamhuri ya Muungano.

Kesi za uchochezi wananzopewa watu sasa hivi zinazingatia kifungu hiki kweli?
 
Back
Top Bottom