Vijana waliopita JKT kwa mujibu wa sheria wote kupigwa chini?

Jan 30, 2023
89
284
RUNGU lilianza wiki iliyopita pale vijana wa JKT walipoenda kwenye Usaili wa Magereza. Ikumbukwe kuna makundi mawili ya vijana wa JKT,la kwanza ni wale walioenda JKT kwa KUJITOLEA (hawa wengi huwa Kidato cha Nne).Kundi la pili ni wale walioenda JKT KWA MUJIBU WA SHERIA (hawa huwa ni Kidato cha Sita).

Wiki iliyopita vijana walioitwa kufanya Usaili wa Kujiunga na Magereza walitangaziwa kwamba kuna MUONGOZO kwamba wote waliopita JKT KWA MUJIBU WA SHERIA wasifanye Usaili huo na hawakufanya wakafurushwa.Wale waliopita JKT KWA KUJITOLEA ndio waliofanya Usaili.

Za ndani ni kwamba hata Vijana waliofanya Usaili Jeshi la Polisi na kwenye Vyombo vingine RUNGU hili nalo litawadondokea.
 
Hata hao waliofanya usahili ambao walikuwa JKT kwa kujitolea wamepigiwa chini Kama ulikuwa na div.three na four za mwanzo!!, waliochukuliwa ni wale wenye div four ya 28 tu!!
 
Duh ! Ila hii nchi hii , huwa sielewi hii logic kabisa ,kwamba four ya 28 ndio inafaa zaidi jeshini au sio ?
wanadai kwamba ukiwa na hio four huwez kuendelea kusoma koo miaka yote utabakia kazini tu kwa sababu hata elimu huwez kujiendeleza
 
wanadai kwamba ukiwa na hio four huwez kuendelea kusoma koo miaka yote utabakia kazini tu kwa sababu hata elimu huwez kujiendeleza
Kweli kabisa mkuu, Pia wanaogopa kuajiri waliofaulu kwa sababu baada ya muda ataanza kudai mda kwenda kusoma.
 
Angalia nafasi zingine mkuu, pengine kuna nafsi nzuri zaidi kwa ajili yako
Mkuu inakata sana aisee jwtz ile form six cardet nimepiga usaili fresh nikapigwa chini niliumia sana nikaona hamna niende tu chuo nimekomaa nimetoka na GPA Kali nikapiga saili za tutorial assistant nikapigwa chini wakabeba wrote wanaojitolea pale chuoni nikaona huenda riziki ipo polisi napo nimepgwa chini aisee mkuu asikuambie mtu imeniuma vibaya mno na bado mbeleni sjui inakuaje japo Nina ufaulu mzuri sana chuoni
 
Mkuu inakata sana aisee jwtz ile form six cardet nimepiga usaili fresh nikapigwa chini niliumia sana nikaona hamna niende tu chuo nimekomaa nimetoka na GPA Kali nikapiga saili za tutorial assistant nikapigwa chini wakabeba wrote wanaojitolea pale chuoni nikaona huenda riziki ipo polisi napo nimepgwa chini aisee mkuu asikuambie mtu imeniuma vibaya mno na bado mbeleni sjui inakuaje japo Nina ufaulu mzuri sana chu
 
RUNGU lilianza wiki iliyopita pale vijana wa JKT walipoenda kwenye Usaili wa Magereza. Ikumbukwe kuna makundi mawili ya vijana wa JKT,la kwanza ni wale walioenda JKT kwa KUJITOLEA (hawa wengi huwa Kidato cha Nne).Kundi la pili ni wale walioenda JKT KWA MUJIBU WA SHERIA (hawa huwa ni Kidato cha Sita).

Wiki iliyopita vijana walioitwa kufanya Usaili wa Kujiunga na Magereza walitangaziwa kwamba kuna MUONGOZO kwamba wote waliopita JKT KWA MUJIBU WA SHERIA wasifanye Usaili huo na hawakufanya wakafurushwa.Wale waliopita JKT KWA KUJITOLEA ndio waliofanya Usaili.

Za ndani ni kwamba hata Vijana waliofanya Usaili Jeshi la Polisi na kwenye Vyombo vingine RUNGU hili nalo litawadondokea.
Maisha yamebadilika sana hii leo wasomi wanatafuta kazi za ajabu ajabu kama hizi na hawapati ?
 
JKT iwe ni added advantage na sio kigezo cha kuajiriwa huku ni kuwanyima haki vijana wasiopita JKT kwa sababu mbalimbali
 
Back
Top Bottom