Mbwa dume
JF-Expert Member
- Jan 15, 2014
- 5,530
- 9,062
Nina girlfriend wangu ambaye tumedumu miezi kadhaa na tumepanga kuoana pindi uchaguzi utakapomalizika!
Amehitimu chuo cha biashara tangu mwaka Jana na mpaka sasa hajafanikiwa kupata ajira!
Nafahamika kwa wazazi wake nae anajulikana kwetu.
Sasa jana alisherehekea siku yake ya kuzaliwa
sherehe ilifanyika nyumbani kwao mida ya saa 1 jioni.
Wiki moja kabla ya sherehe hiyo nilikuwa safarini nikamuahidi kumnunulia zawadi nzuri kwa ajili ya birthday yake.
Sasa hiyo jana alikuwa na shauku ya kutaka kujua nimemletea zawadi gani !
Mda ulipowadia nilienda taratibu kumkumbatia kipenzi changu na kumzawadia cherehani mpya aina ya butterfly pamoja na kuahidi mbele ya umati kuwa nitatoa gharama zote za mafunzo ya kozi ya miezi mitatu ya ushonaji ili baada ya kumaliza mafunzo aweze kujiajiri.
Lakini cha ajabu mpenzi wangu alionyesha hakufurahishwa na zawadi hiyo!
Jana usiku kanisms kwamba "umenichukuliaje mimi lakn?"
Nikampigia akasema eti alitegemea ningemnunulia zawadi ya maana kumbe hovyo!
Leo nimemtumia ujumbe tuonane hakunijibu nimejaribu kumpigia mda wote hapokei simu yangu!
Naomba mnishauri eti hiyo zawadi ina ubaya gani au ningemnunulia nini ikiwa sina uwezo wa kununua gari?!