Kuna siri gani ya mafanikio ya ghafla kwa wafanyabiashara ya kuuza smartphones?

NetMaster

JF-Expert Member
Sep 12, 2022
1,454
4,853
Wengi huwa ni vijana wadogo tu wapo kwenye 20s hasa wahitimu wa degree na diploma.

ni tabaka tofauti na wauza simu wengine, wao hujitofautisha kwa kuuza simu zenye brand zinazotrend ulaya na marekani tu kama iphone, samsung na google pixel... Simu za kichina na vitochi hawauzi.

Simu hizo bei huwa zimechangamka kwahio wengi wapo kwenye majiji yenye watu wenye vipato vya juu wanaoweza zimudu kama Dar (maduka yao yamejaa Makumbusho, Mwenge na kariakoo), Mwanza, Arusha.

kwa macho yangu nimeweza kuwa observe kwa miaka kama miwili hawa vijana na nimeona wengi biashara imebadili maisha yao ghafla.

  • vijana wanaonekana smart sana, wanatupia pamba na hawapo nyuma kwenye fashion.
  • kwenye usafiri nako si haba, kijana mwenye 20s kumiliki crown, subaru, bmw yupo juu huyo.
  • kwakuwa wanazijua simu na wanazifatilia, wengi wanamiliki simu za gharama za kisasa
  • kwenye sekta ya kula bata, hawana shughuli ndogo, uwanja huu wanafanya kweli japo kwa level za kibongo.
  • wanaishi sehemu smart, wapo waliopanga apartment nzuri, wapo waliopanga nyumba nzima, n.k huku wakiendelea na ujenzi
  • ni ngumu sana kugombaniana mwanamke, binti mwenye simu ya kichina ya laki 2 iliyochoka anahongwa hata iphone ya laki 5 yenye wateja wachache, binti kapewa tu hio iphone ashazuzuka bila kujali ya mwaka gani
 
1672570243456.png
 
Mie naona hizi biashara za simu ni kama kazi ya ziada au kuficha chanzo kikuu cha income yao. Ila ni kweli hawa vijana wanaonekana smart sana na inaonekana wana mkwanja mrefu na usafiri mzuri. ila nakua siamini kama hiyo biashara ya simu pekee ndiyo inawatoa. Kuna kitu nyuma ya pazia
 
hizi simu kwa jumla wanachukulia wapi
Hizi simu zipo dubai, ulaya au china na zinakuja kama used as new au certified refurbished. Kwa hiyo ukinunua kwa jumla bei inakuwa ndogo. Ukija kuuza kwa bei elekezi inakuja na faida nzuri. Kwa hiyo hawa wanachuo hutumika kama madalali kupata wateja kuliko kukaa na simu dukani.
 
Wengi huwa ni vijana wadogo tu wapo kwenye 20s wakiwemo wahitimu wa vyuo wenye degree/diploma, hupendelea kuuza simu zenye brand zinazotrend ulaya na marekani hususani iphone, samsung na google pixel... Simu za kichina hawauzi ama ni nadra.

Simu wanazouza ni bei kali hivyo wengi wapo kwenye majiji yenye watu weye vipato vya juu wanaoweza zimudu kama Dar (maduka yao yamejaa Makumbusho, Mwenge na kariakoo), Mwanza, Arusha.

Kiukweli kwa macho yangu nimeweza kuwa obsetve kwa miaka kama miwili hawa vijana na nimeona wengi hasa wanaomaliza vyuo wakiingiia hii biashara maisha yao yanabadilika ghafla kwenye suala la mkwanja.

Wengi naowajua hawakosi usafiri wa maana unaopendwa na vijana wa rika zao za 20s na early 30s, crown, subaru, bmw, wanamiliki simu za kisasa za gharama sanasana iphone matoleo mapya bei huwa milioni 2+.

Suala zima la kutupia pamba wapo byee, wanawakilisha vema vijana wenye 20s kwenye sekta ya kula bata, hawana shughuli ndogo uwanja huu wanafanya kweli japo kwa level za kibongo.
Changamoto ya hizo simu nyingi zinarudishwa na wateja, hivyo uwe aware na hilo.
Maana katika piece 10 utakazouza zitakazoenda kulalamikiwa na wateja na hatimaye kuja kubadilisha ni 50/50
So wengine wanavumilia wengine inabidi ubebe lawama wengine uwabadilishie.
Matatizo ni mengi kwakweli.
Nipo kwa hii field so nafahamu risk zake na changamoto tunakutana nazo sokoni
 
Hehehe wamefikiwa na kwa uchache wao. Nobody understands kwanini hawa vijana wana hela hivi😂😂😂
 
Changamoto ya hizo simu nyingi zinarudishwa na wateja, hivyo uwe aware na hilo.
Maana katika piece 10 utakazouza zitakazoenda kulalamikiwa na wateja na hatimaye kuja kubadilisha ni 50/50
So wengine wanavumilia wengine inabidi ubebe lawama wengine uwabadilishie.
Matatizo ni mengi kwakweli.
Nipo kwa hii field so nafahamu risk zake na changamoto tunakutana nazo sokoni
huo utafiti labda umeufanya kwa wauza simu wa mchongo, ni nadra sana mtu karudisha simu mbovu kwenye duka alilonunua labda wawe wapiga dili. binafsi hadi sasa nishanunua simu zaidi ya 10 zikiwemo efurbished 3 na hakuna hata moja nimewahi kurudisha.
 
Mie naona hizi biashara za simu ni kama kazi ya ziada au kuficha chanzo kikuu cha income yao. Ila ni kweli hawa vijana wanaonekana smart sana na inaonekana wana mkwanja mrefu na usafiri mzuri. ila nakua siamini kama hiyo biashara ya simu pekee ndiyo inawatoa. Kuna kitu nyuma ya pazia
Exactly
 
Back
Top Bottom