ALLIANCE GLOBAL: Kampuni ya kitapeli inayoendelea kuliza wasomi wengi nchini

Undava King

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
3,205
5,333
"Kama kuna jambo linauma basi ni kuteketeza karo shuleni kumsomesha mwanao kisha wajanja wachache watumie nafasi hiyo hiyo ya usomi wake kukutapeli kama mzazi kwa kigezo cha kumpatia ajira"

Nikiwa njiani kuelekea mjini kwenye miangaiko pembeni yangu (kwenye daladala) kaketi dada mmoja aliyevalia nadhifu kimwonekano ni kama mfanyakazi anayewahi kazini na amekwisha chelewa tiyari kwa maana mara kwa mara anapigiwa simu inaonekana kama ni za maagizo au maelekezo fulani.

"Samahani kaka eti hili gari linafika mpaka kirumba?"

Hapo nikujua moja kwa moja kumbe ni mgeni.."hapana linaelekea Buhongwa labda ukifika Natta ushuke"

Baada ya hapo ndipo ukawa mwanzo wa mazungumzo ambayo hitimisho lake ilikuwa ni kwa dada wa watu kughairi safari yake na ikambidi harudi alikotoka huku akibwaga machozi sijui ni ya furaha ama simanzi, akinishukuru kwa kumwokoa na huo mtego wa kampuni uchwara kwa jina la Alliance Global.

Labda wengi hawafahamu lakini kuna wale ambao walishaibiwa wakajifunza na kuna wale ambao wamepata uzoefu na matukio ya kitapeli ya makampuni ya namna hii yanayojinadi kufanya biashara ya Mtandaoni kuuza bidhaa za virutubisho lishe (hasa toka Marekani na Ufilipino) huku wakijinadi kutengeneza kiasi kikubwa cha pesa kupitia biashara hii kiasi cha kuvutia hisia za walio wengi hasa wasomi na wahitimu wa sekondari na vyuo vikuu kudhania hii ni njia bora zaidi ya mafanikio ya haraka.

Chondechonde Mzazi au Kijana wa form 4, form 6 na Chuo Kikuu (hasa wa vijijini mnaoamini moja kwa moja taarifa mnazopokea kwa ndugu zenu walioko mijini)nyie ndiyo walengwa wa hawa manyang'au, pindi unapopokea simu au taarifa juu ya uwepo wa ajira isiyo na masharti magumu ya kikazi yaani ni bora tu mwanao awe amehitimu au anajua kompyuta na ya kwamba wao shughuli zao za kibiashara ufanyikia ndani (kwa maana ya kwenye kompyuta kwa njia ya mtandao) na haziusishi uvujaji wa jasho juani kama wafanyavyo machinga, Shtuka.

Usikubali kutoa pesa hili uajiriwe (utaambiwa kazi ipo ila lazima uje na kiingilio cha TSh.30,000/= na pesa ya malazi ambayo haiainishwi wazi (watatoa huduma ya hosteli)na kazini kufika ni saa 1 kamili hili mradi utoe pesa ya accomodations ila chakula hawahusiki nacho hiyo gharama ni juu yako (hii ni kwa Mwanza sijui kwingine huko)

Baada ya kufika eneo la tukio utapewa Account ya Benki (sitoitaja) ukawawekee Laki sita (TSh.600,000/=) hili upewe hivyo virutubisho lishe ukaangaike navyo kutapeli wazee wastaafu na watu wenye matatizo sugu ya kiafya na wenye ufahamu duni kuhusiana na bidhaa hizo, kisha kiasi utakachouza unawarudishia wao na wewe utalipwa kwa commission na kiasi kisichozidi Tsh.150,000-180,000 kwa mwezi ikiwa na wewe utawaingiza kundini washiriki wengine wawili ambao nao watatoa ada kama hiyo (mtaji) ya kiingilio, huu ni mtego usiingie.

Dalili/Ishara kuwa ni wao hata kama jina la Kampuni ni lingine na si hili nililolitaja:-

1. Uambiwi pointi rasmi ya mahali ofisi yenyewe ilipo, unachotakiwa ni kufika na kujionea.

2. Utapigiwa simu na tapeli mmoja kukupa guidance ya namna ya kuwafikia mahali walipo lakini utaambulia kuelekezwa kama mshamba, mfano halisi kwa Mwanza "..ukifika shukia daraja la samaki" Umeshashuka? "Njoo mpaka usawa wa viwanja vya Furahisha", Umeshafika? unaiona hiyo gari ya bluu mbele yako? Nimemtuma kijana mmoja kavalia black suti anakuja kukupokea, kisha mguu moja kwa moja mpaka "VILLA PARK HALL" mahali walipo hivi sasa wakati naandika uzi huu.

3. Kama ulivyotaraji sivyo badala ya ofisi utakutana na bonge la ukumbi na wanajua kuselekti mno location lazima liwe ni jengo moja kubwa la kukodi lenye geti au hoteli mahali ambapo si rahisi kushtukiwa.

4. Kama ulihisi kwa mujibu wa wito kuwa unaripoti katika ofisi fulani ya kampuni ndugu yangu umewaka, hii ni zaidi ya kampuni kwani inawafanyakazi (nyie mnaoingia kwenye ajira hii ya mchongo) kati ya vijana 600 hadi zaidi ya 1000 ambao wamekaa kimakundi makundi ndani ya ukumbi mmoja wakipokea mafundisho na maelekezo toka kwa motivation speakers waliovalia vazi rasmi la suti.

Wito wangu kwa walengwa/waathirika wa mambo haya ambao mpaka hivi sasa ninapoandika uzi huu wapo benchi wakipangwa na wengine wakiendelea na mikakati ya kulipa ada na viingilio shtukeni na mwachane na mipango hiyo ya kilaghai ondokeni mahali hapo mnadhalilisha usomi na utu wenu.

Pili mnajitia umasikini bure, ikiwa umejitafuta mpaka ukapata laki 6 na ikiwa hekari 1 ya shamba la mahindi au viazi vitamu kijijini maandalizi hadi kuivisha ni laki 1 kwanini kama wasomi msiungane katika kilimo cha pamoja na muunde vikundi huku mkijihakikishia mikopo serikalini na katika mabenki/wafadhili, bahati njema wameshawaleta pamoja na mmekutana kwa wale ambao bado hamjaingia mtegoni sanuaneni msepe mkachape kazi kiufupi hakuna mafanikio rahisi duniani.

Tatu, Kujiamini na Kujitambua ni pamoja na kujisimamia na kutambua haki yako na ya wengine wanapoonewa, kukandamizwa, kudhulumiwa n.k na kusimama mstari wa mbele kuwapigania na kuhakikisha kuwa wanapata haki zao, tafadhali kama wasomi (wale mlioshtuka kabla ya kuwapa pesa) washtueni wenzenu waliokwisha kutapeliwa kuwa mahali mlipo siyo sahihi na fuateni misingi ya haki na sheria kudai kilicho chenu kabla hamjachelewa.
 
Haaaah! Hivi hawa jamaa bado wapo??

Nawakumbuka hawa kwenye season ya Corona

ILIVYOANZA

Mwaka juzi kuna dada mmoja mtaani naheshimiana naye sana akaniomba siku ya jumamosi nikahudhurie semina.

Ni mtu ambaye namheshimu sana na aliponiambia hivyo hata sikuwa na wasiwasi nikasema sawa basi nitamwambia na rafiki yangu ili twende wote.

Kweli ilipofika jumamosi tukachomoka wote watatu mpaka pale mwenge kwenye stand ya daladala kuna ki ghorofa fulani ambacho floor ya juu kuna ukumbi.

Basi tukafika pale kwanza kila mtu naye muona pale kama ni mwanaume basi amegonga suti afu na funguo zina hang kwenye lux ya suruali.

Kulikuwa na baadhi ya watu ambao walivaa kawaida ambao baadaye hao ndio nilikuja kufahamu kuwa ni wageni kama sisi wamekuja hapo kwa ajili ya kusikiliza hiyo semina.

Ilikuwa majira ya saa 7 ndio semina inaanza, akaoita jamaa mmoja mbele akiwa na projector akatusalimia "Helloooo" akifuatia na Good morning japo ilikuwa ni mida ya mchana.
 
JINSI WANAVYOANZA KUTENGENEZA UAMINIFU

Mara jamaa akaanza kujiongelesha. "Unajua mimi nilikuwa ni mwanafunzi wa chuo na nikiwa mwaka wa tatu chuoni niliamua kuacha chuo nikajiunga na hii Organization"

Akawasha projector akawa anatuonesha picha zake akiwa nyuma ya magari ya kifahari.

Kwanza akaanza kuweka defense "unajua hii ni kampuni halali na imesajiliwa na ina vibali vyote. Hivyo kama una wasiwasi na ukweli wa haya mafanikio basi anza tu kufikiria kiasi kilichotumika ku register hii kampuni"

"Ukumbi huu tumeukodi kwa muda wa wiki moja. Fikiria tu hizo gharama zake, je kuna dalili yeyote ya uongo hapo?"

"Na je Serikali inawezaje kutupa kibali cha kuruhusu tufanye utapeli?"

Akatoka kwenye defense akaja kwenye kupanda mbegu ya utapeli kichwani mwetu

"unajua hii Alliance Global Movement inafanywa na watu wengi mashuhuri ila kutokana na mafanikio yake kuwa rahisi watu wamekuwa wakifanya siri"

Akaweka picha akiwa na mzee mmoja wa Kifilipino, mara wakiwa Club, kwenye boti, airport.

Aliongea mengi sana ya kuonesha kuwa ni rahisi sana kuwa milionea.
 
MWISHO AKAJA KWENYE POINT


AKasema wamekuja na bidhaa ambayo ni package ya dawa lakini ni virutubisho. Wakasema wamefanya hivyo ili kuwasaidia watu hususani vijana watumie product hiyo kujikomboa kwenye umasikini.


Mchanganuo wa hiyo product sasa.

Ni kwamba kwanza unatakiwa uelewe kuwa hiyo product haitolewi bure. Ni package inayouzwa Shilingi 500,000.

Ndani yake kuna mchanganyiko wa dawa zenye kutibu magonjwa mengi ikiwemo kisukari, ugonjwa wa moyo, na Covid.

Lakini pia package hiyo unaweza kuitumia kama virutubisho tu hata kama sio mgonjwa.

Akatuwekea na picha ya mfumo wa ndani wa mwili wa binadamu ambao unatisha. Akatutajia jina la ugonjwa akisema ndio sababu iliyofanya mfumo wa ndani uwe na muonekano wa kutisha.

Baadaye akaweka picha nyingine inayoonesha mfumo wa ndani wa mwili wa binadamu upo clean.

Akatoa maelezo kuwa hapo ni baada ya mgonjwa kutumia product yao ndio ikaenda kufanya uponyaji.

Hivyo unachotakiwa kufanya ni kutengeneza pair. Ukinunua hiyo package utafunguliwa account na kiasi fulani cha pesa utawekewa kama kianzio ambacho ni 50,000.

Halafu ukimleta mtu mwingine hapa akanunua tena package yetu maana yake utapata shilingi 50,000 ambayo nayo itaingia kwenye account yako iliyotengenezwa.

KWa hiyo naye huyo mtu akileta mtu mwingine ndivyo utavyozidi kutengeneza hela kupitia pair.

MASWALI NILIYOWAULIZA

Niliponyoosha mkono kutaka kuuliza swali akaniruhusu.

SWali lilikuwa ni hili

Ikiwa kama kweli nyinyi mmeamua kumsaidia kijana ajitoe kwenye umasikini kwanini muweke gharama kubwa ya kununua hiyo bidhaa?

Je ni kweli mna amini mtu anayeweza kuwa na laki 5 ni mtu ambaye anahitaji kusaidiwa kuepukana na umasikini?

NImesikia kuna watu humu mnamiliki majumba na utajiri wa kifahari. Mwingine kasema ana
miliki 150M. Sasa akitoa 10M akatununulia hiyo product atakuwa amesaidia watu wangapi kuwainua kiuchumi?
 
hata universisty abroad ya mtu anaitwa Tonny ya kupeleka wanafunzi nje ya nchi ni matapeli kuliko matapeli wote duniani mshenzi sana huyo TONNY na genge lake ofisini
Uje na ushuhuda kuhusu huyu jamaa! Nilikuwa namuoma ni mtu smart sana kila nilipokuwa nikimtazama kwenye TV akihamasisha vijana kusoma nje ya nchi kupitia university abroad!

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
hata universisty abroad ya mtu anaitwa Tonny ya kupeleka wanafunzi nje ya nchi ni matapeli kuliko matapeli wote duniani mshenzi sana huyo TONNY na genge lake ofisini
Waanike na maovu yao mkuu usisite kusanua juu ya shughuli za hawa mbwa mwitu hapa ndipo mahala pake uwezi jua utakuwa umesaidia wangapi kwa taarifa yako.
 
MWISHO AKAJA KWENYE POINT


AKasema wamekuja na bidhaa ambayo ni package ya dawa lakini ni virutubisho. Wakasema wamefanya hivyo ili kuwasaidia watu hususani vijana watumie product hiyo kujikomboa kwenye umasikini.


Mchanganuo wa hiyo product sasa.

Ni kwamba kwanza unatakiwa uelewe kuwa hiyo product haitolewi bure. Ni package inayouzwa Shilingi 500,000.

Ndani yake kuna mchanganyiko wa dawa zenye kutibu magonjwa mengi ikiwemo kisukari, ugonjwa wa moyo, na Covid.

Hivyo unachotakiwa kufanya ni kutengeneza pair. Ukinunua hiyo package utafunguliwa account na kiasi fulani cha pesa utawekewa.

HAlafu ukimleta mtu mwingine hapa akanunua tena package yetu maana yake utapata shilingi 50,000 ambayo nayo itaingia kwenye account yako iliyotengenezwa.

KWa hiyo naye huyo mtu akileta mtu mwingine ndivyo utavyozidi kutengeneza hela kupitia pair.

MASWALI NILIYOWAULIZA

Niliponyoosha mkono kutaka kuuliza swali akaniruhusu.

SWali lilikuwa ni hili

Ikiwa kama kweli nyinyi mmeamua kumsaidia kijana ajitoe kwenye umasikini kwanini muweke gharama kubwa ya kununua hiyo bidhaa?

Je ni kweli mna amini mtu anayeweza kuwa na laki 5 ni mtu ambaye anahitaji kusaidiwa kuepukana na umasikini?

NImesikia kuna watu humu mnamiliki majumba na utajiri wa kifahari. Mwingine kasema ana
miliki 150M. Sasa akitoa 10M akatununulia hiyo product atakuwa amesaidia watu wangapi kuwainua kiuchumi?
Eheee, wakakupa jibu gani?
 
Back
Top Bottom