Aliewahi kuwa housegirl anaingiza zaidi ya milioni 1 kila mwezi, walioenda vyuo kuna haja ya kufanya kazi sehemu binafsi kwa mishahara ya laki 3?

R-K-O

JF-Expert Member
Jun 27, 2023
482
2,138
Ni binti naemjua kabisa alikuwa house girl akiwa na umri wa miaka 16 alitolewa huko Iringa aje kusaidia kazi, baada ya miaka sita familia ikaamua wampeleke sehemu ajifunze kushona, alipomaliza akarudi kwao kijijini wakampa cherehani na milioni 1 na nusu ya shukrani.

Binti hakukaa sana huko kwao akarudi mjini, alikuwa anasaidia kupika mgahawa flani wa mtaani kwa miezi miwili hivi ila ni mbali na sehemu aliyoishi akiwa house girl, watu wa mtaa moja tulioishi nae walidhani labda alifukuzwa wengine tuliomjua kasomeshwa cherehani, kapewa chereani na kapewa milioni na nusu tulihisi labda katapeliwa kila kitu na ndugu zake.

Muda si mrefu nae akafungua sehemu kwenye frem za kawaida hizi, sio uswazi sana anapika chakula cha mchana na jioni. wali, maharage, pilau na nyama.

Navyoongea sasa hivi ile sehemu ya mwanzo wapo mabinti wawili kawaacha hapo, yeye alishafungua sehemu nyingine na wateja wapo.

Ilinishawishi nimfatilie zaidi, hajanipa mchoro mzima ila aliniambia ile miezi miwili alikuwa anapitia training na kuijua biashara, ndipo nilipoelewa kwamba hakutapeliwa kama nilivyodhani mwanzo.

Kwa haraka haraka kwenye mgahawa moja anaweza kupata elf 30 faida, kwa migahawa miwili kwa mwezi ?

Nachohofia tu pengine akipata mario ampe mimba inaweza kumtikisa

Kwa upande mwengine nikianza kutafakari hawa wadogo zetu wengine ambao wamemaliza vyuo wapo ajira zenye mishahara ya laki na nusu hadi 5 tena ni private nafadhaika sana, wengi huona aibu kufanya baadhi ya shughuli kama kupika mitaani.
 
Basi utajipendekeza upeleke umarioo wako, binti wa watu afilisike.
Ntakuwa mstari wa mbele ikitokea nisikie kuna mbwiga anataka kumuharibia.

Binti anatoa funidisho kubwa hata kwa wengine, kuna wengine wanaona aibu kupika mtaani wameridhika na ajira za laki na nusu
 
Kila Biashara ni nzuri ukisimuliwa^
Ni kwamba wasomi wengi hawapo tayari kufanya baadhi ya biashara wakipata vyeti, hii imekwamisha wengi sana wawe watumwa wa mishahara ya laki 3

Mtu kamaliza chuo hataki kusikia mambo ya kuchoma mahindi, umama ntilie, kuchoma mishkaki, n.k. fursa zinampita
 
Kila ambae ameingia mtaani mapema ...baada ya miaka 10 yupo mbali...
Hata walioanza kama vibarua kkoo wakiwa Wana miaka 15...walipofikisha miaka 25 walikuwa na stable income
35 walikuwa mbali Sana ...

Mimi namjua mtu amejenga ghorofa na anaendesha mkokoteni sokoni ...Kwa miaka mingi....sana...

Karibu matajiri Wengi hawana elimu ya chuo kikuu....


Shida ya kusoma Sana unakuwa unajikosoa Sana kabla ya hata kuingia mtaani...mwisho unasita
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom