Kuna siri gani ambayo Jenerali Venance Mabeyo anataka kumpa Rais Samia Suluhu?

Afande MABEYO naomba nikukumbushe katika dokezo lako kwa muheshimiwa raisi usiwasahau vijana wa JKT walio katika miradi mbalimbali ya kitaifa

Kwa kumbukumbu zangu ndogo kwa sasa watakuepo oparesheni MERERANI wakijenga ikulu DODOMA wakiwa 2000+

PIA Lipo kundi dogo la vijana 300 katika bwawa la NYERERE vijana hawa na kama mmewasahau hawaongelewi kabisa.. hawa ni miaka miwili sasa hawajatoka katika lile pori, hawana likizo na hawajui kitu mjini....

Baada ya kundi kubwa mkataba wao kuisha na kurudi nyumbani hawa walibaki na mara kadhaa HAYATI MAGUFULI alikisikikika akiahidi kuwaajiri...

Makundi haya yamefiwa na hawajui nini kinaendelea....

Nikuombe AFANDE MABAYO kama itakupendeza fikisha salamu za vijana hawa kwa muheshiwa Raisi.

Vijana msikate tamaa..... POPOTE MLIPO
TUPAMBANE MPAKA MWISHO
Maneno mazuri sana, i wish afande ayaone

Sent from my Android using JamiiForums mobile app
 
by the way kwanini mkuu wa majeshi anahutubia?
ili iweje?
Jeshi limeingizwa kwenye siasa . Hata ile habari kwamba kuna kitu Mabeyo anataka kumwambia Rais Hassan ni siasa.

Mabeyo hakosi muda wa kuongea na rais privately, pale alikuwa anatangaza kwa umma.

Kuna power struggle kubwa sana huko kati ya wafuasi wa Magufuli na watu wa makundi mengine ye CCM.

Kuna watu walitaka hata Samia Suluhu Hassan asiwe rais, Mabeyo na wenzake wakasema katiba ni lazima ifuatwe.

Ndiyo maana umeona Mkuu wa Majeshi katoa hotuba, halafu katika msiba, sehemu ambayo ungetegemea hotuba za tazia za rais aliyefariki, mkuu wa majeshi katumia muda mwingi sana kuongea jeshi ilivyo nyuma ya rais mpya na karudia rudia sana kwamba linamuunga mkono na litamlinda. Hii ni kuweka watu wote jeshini wajue kwamba hakuna muda wa kuwa na makundi jeshini, jeshi lipo nyuma ya rais mpya.
 
Watu wana mipango na mikakati ya mbali mkuu

Kumbuka wakati huu kila mmoja anataka kujiweka kwenye nafasi ya kuaminika kwenye awamu ya sita...

Kwa nafasi yake nafasi ya kumuona Rais anayo na anaweza kumweleza jambo lolote wakati wowote, hapakua na haja ya kulisema hili hadharani.

Aidha kwa upande mwingine, inawezakua kuna ujumbe anautuma kwa watu flani.
CDF sio mtu mdogo. Na wala haitaki kujikomba kwa yeyote.
 
Mabeyo hakuwa na ulazima wa kulisema hadharani...
Think beyond, amesema hadharani Sababu alikuwa anatuma ujumbe kwa kikundi flani...lazima alitaka hicho kikundi kijue kwamba kama kuna issue aliambia na Rais kabla mauti hayajamkuta basi anayo na atamfikishia ujumbe Rais.
 
Watu wana mipango na mikakati ya mbali mkuu

Kumbuka wakati huu kila mmoja anataka kujiweka kwenye nafasi ya kuaminika kwenye awamu ya sita...

Kwa nafasi yake nafasi ya kumuona Rais anayo na anaweza kumweleza jambo lolote wakati wowote, hapakua na haja ya kulisema hili hadharani.

Aidha kwa upande mwingine, inawezakua kuna ujumbe anautuma kwa watu flani.
Hata hivyo ikumbukwe tupo kwenye msiba kwahiyo kujikwaaa ulimi kwa namna hii tutarajie kupo kikubwa ni kuvumiliana tu
 
JE KULIKUWA NA UMUHIMU GANI WA MKUU WA MAJESHI KUTOA KAULI HIYO? Je, haoni kwamba kwa nafasi yake kutoa kauli kama hiyo kunaweza kuzua taharuki kwenye jamii juu ya usalama wa nchi au Mh. Rais?
Taharuki hiyo wataipata wenye mipango yao miovu.Why trembling kama uko clean?!.
 
Anataka kujiosha tu mi nataka awaeleze ndugu zetu wa JWTZ zile tiriol za kutosha zilizokutwa kwenye account ya mke wake zilitoka wapi?

Na pili ile bima anayoikata kwa kila mshahara halafu hakuna faida inayopatikana kwa askari nazo anapeleka wapi? Mi ni hayo tu.
Kama bunge tu halijadil mambo yao wewe ni nani mpaka uambiwe
 
Majeshi yetu ya Ulinzi yakae nje ya Politics
Yalinde mipaka haswa huko kusini
So yakubali tu hata kama nchi inaporwa na wanasiasa? Unajua waafrika tuna akili fupi sana? No wonder bado ni masikini. Tunapenda vitu rahisi sana...wizi wizi, mambo mepesi mepesi..siasa kama BIASHARA
 
So yakubali tu hata kama nchi inaporwa na wanasiasa? Unajua waafrika tuna akili fupi sana? No wonder bado ni masikini. Tunapenda vitu rahisi sana...wizi wizi, mambo mepesi mepesi..siasa kama BIASHARA
Nchi zinazotawaliwa na Wanajeshi nazo huporwa na Wanajeshi
 
Watu wana mipango na mikakati ya mbali mkuu

Kumbuka wakati huu kila mmoja anataka kujiweka kwenye nafasi ya kuaminika kwenye awamu ya sita...

Kwa nafasi yake nafasi ya kumuona Rais anayo na anaweza kumweleza jambo lolote wakati wowote, hapakua na haja ya kulisema hili hadharani.

Aidha kwa upande mwingine, inawezakua kuna ujumbe anautuma kwa watu flani.

Huyu kamanda nimemkubali. Kwanza tumejua ziko siri za jeshi ambazo anajua CDF na Amiri basi. Lakini kulikuwa na katensioni flani hivi. Ndungai sijui ni majonzi au nini alikuwa ana kitu kina msumbua ,CDF was very sereous.
 
Back
Top Bottom