Wameukuza sana huu ugonjwa sasa uhalisia unapoonesha tofauti ndipo watu wengine husema hakuna ugonjwa kabisa.Nafikiri ubishani ulioibuka juu ya huu ugonjwa ndio unaouvumisha zaidi.
Kwa hiyo vifo vya 3% kwa aiborne disease unaona si kitu. Pengine labda sijui lengo lako. Wewe unapinga chanjo sababu ugonjwa umekuzwa?Nakwambia hivi wanaokufa ni wachache kuliko wanaopona ila muda wote vinazungumziwa vifo tu,ndio maana ilifikia watu kutabiri kuwa huu ugonjwa ukija afrika tutaokota maiti barabarani na ni kweli kwa kipindi kile ilikuwa halali kusema vile.
Chanjo hiari ni siasa. Kama unazuiwa kuingia uwanjani au kusafiri nje bila kuchanja kuna hiari hapo?Kwani si tulikubaliana chanjo ni hiari, kifo ni lazima!!!
Kwa hali ninavyoiona ya hii Korona kuondoka na watu, kuna siku watanzania watapanga foleni za kilomita kadhaa ili wapate chanjo.
Nilienda kupata chanjo siku ya jumanne. Nilikuwa niko peke yangu na mtoa chanjo. Tulizungumza mambo kirefu sana. Nilikaa pale kama nusu saa hivi. Mbaya zaidi wafanyakazi wa afya wengi sana nao wanakwepa kuchanja. Jamaa fulani alinipa uchambuzi kuwa wafanyakazi wengi wa afya kinachowafanya wasichanje ni uoga wa sindano!!
Kingine nilichokiona, unapewa cheti cha mkononi na kingine unaweza download. Inaonekana kama umedhamiria kutochanja ila unataka upate cheti, unaweza 'ukachonga' na mtoa chanjo ukapata cheti.
Mbaya zaidi serikali nayo imechukulia mzaha hili suala. Gwajima, Dr anaenda kumpa Steve Nyerere ubalozi wa chanjo. Ataelimisha nini watu juu ya chanjo?
Siku inakuja watu watapanga foleni za kilomita kadhaa ili kupata chanjo
Utungaji huu, wengi wameanzisha uzushi kama huu. Mtaani kwetu hivi, kule vile. Umesikia chanjo inaweza sababisha kuganda damu unaamua kutunga "mtaani kwetu."Kuna kesi kadhaa zimetokea Mtaani kwetu, walikwenda kuchanja na haijaisha hata miezi mitatu, wamechapa mwendo. Hospital walipochunguzwa ikabainika kuna shida ilikuwa inajitokeza kwenye damu(Damu Kuganda). Mnaokwenda kuchanja nyie nendeni tu.
Na visa hivyo havifuatiliwi na kutangazwa ila wenyewe wanasema ni watu wachache tu ndio wanaoganda damu, hata huku napokaa kipo kisa cha aina hiyo. Na nasikia kuna wengine wanaparalyze.Kuna kesi kadhaa zimetokea Mtaani kwetu, walikwenda kuchanja na haijaisha hata miezi mitatu, wamechapa mwendo. Hospital walipochunguzwa ikabainika kuna shida ilikuwa inajitokeza kwenye damu(Damu Kuganda). Mnaokwenda kuchanja nyie nendeni tu.
Hata malaria kila unapoumwa unapiga dawa.Kirusi kikibadilika unachanjwa tena na tena hadi utakapokufa
Kama ni hivyo kungekuwa hakuja haja ya kuchanja chanjo zile utotoni. Wala kutumia dawa. Wala kuwa na hospitali.Kifo hakikimbiwi na wala hakina chanjo ukiona hujafa Basi haujafa kwaajili ya kinga ya chango ila haujafa kwasababu siku hazijafika
We chanja mi sichanji
Kila mtu awe na uhuru wake anaechanja achanje asie chanja aachweKama ni hivyo kungekuwa hakuja haja ya kuchanja chanjo zile utotoni. Wala kutumia dawa. Wala kuwa na hospitali.
Yap. Ila kumbuka hiari hiyo ni siasa tu.Kila mtu awe na uhuru wake anaechanja achanje asie chanja aachwe
Tumekuwa na Tatizo Kuu la kutaka Kusikia Unachokitaka au Kuona na Kifanywe Unachokitaka Mhusika na sio Uhalisia. Wewe ukitaka kukubali kubali, usipotaka acha. Juzi nipo ofisini, kuna jirani yangu hakuwa amefungua ofisi yake, nikampigia kumuuliza kama atakuja akaniambia hana uhakika sababu walikuwa kwenye mazishi ya jirani yao.Utungaji huu, wengi wameanzisha uzushi kama huu. Mtaani kwetu hivi, kule vile. Umesikia chanjo inaweza sababisha kuganda damu unaamua kutunga "mtaani kwetu."
Kila mtu afanye maamuzi yake anaepiga campaign za chanjo aachwe na anaepiga campaign za kukataa chanjo aachweYap. Ila kumbuka hiari hiyo ni siasa tu.
Hizo side effects ndizo alizokuwa anazihoji Gwajiboy akaishiwa kupopolewa mawe, watu bado wanaona ni jambo dogo ila muda utasema tu. Mdudu ni kweli yupo na anaua ila hii chanjo inaua pia. Dizonga nako nasikia wameanza kukiamsha barabarani kupinga chanjo.Na visa hivyo havifuatiliwi na kutangazwa ila wenyewe wanasema ni watu wachache tu ndio wanaoganda damu, hata huku napokaa kipo kisa cha aina hiyo. Na nasikia kuna wengine wanaparalyze.
Mkuu unamaanisha manesi wanawachoma watoto?Mi nimechanja lakini kitoto changu kichanga sitaki kichanjwe! Kuna nesi hapa amenivuta sikio niwe makini.
Naona hakuna muitikio wa chanjo kwa watu wazima wanaamua kuipunguzia kwa vitoto huko leba
Wana chanja ili kujiepusha na kufa kwa corona na athari zake zingine au?Kuchanja au kutochanja haimaanishi kuwa hautakufa.