#COVID19 Kuna siku Watanzania watapanga foleni za kilomita kadhaa ili kuchanja

Nakwambia hivi wanaokufa ni wachache kuliko wanaopona ila muda wote vinazungumziwa vifo tu,ndio maana ilifikia watu kutabiri kuwa huu ugonjwa ukija afrika tutaokota maiti barabarani na ni kweli kwa kipindi kile ilikuwa halali kusema vile.
Kwa hiyo vifo vya 3% kwa aiborne disease unaona si kitu. Pengine labda sijui lengo lako. Wewe unapinga chanjo sababu ugonjwa umekuzwa?
 
Kwa hali ninavyoiona ya hii Korona kuondoka na watu, kuna siku watanzania watapanga foleni za kilomita kadhaa ili wapate chanjo.

Nilienda kupata chanjo siku ya jumanne. Nilikuwa niko peke yangu na mtoa chanjo. Tulizungumza mambo kirefu sana. Nilikaa pale kama nusu saa hivi. Mbaya zaidi wafanyakazi wa afya wengi sana nao wanakwepa kuchanja. Jamaa fulani alinipa uchambuzi kuwa wafanyakazi wengi wa afya kinachowafanya wasichanje ni uoga wa sindano!!

Kingine nilichokiona, unapewa cheti cha mkononi na kingine unaweza download. Inaonekana kama umedhamiria kutochanja ila unataka upate cheti, unaweza 'ukachonga' na mtoa chanjo ukapata cheti.

Mbaya zaidi serikali nayo imechukulia mzaha hili suala. Gwajima, Dr anaenda kumpa Steve Nyerere ubalozi wa chanjo. Ataelimisha nini watu juu ya chanjo?

Siku inakuja watu watapanga foleni za kilomita kadhaa ili kupata chanjo

Lazima, hata tungechanja wote hiyo siku Itafika
 
Kuna kesi kadhaa zimetokea Mtaani kwetu, walikwenda kuchanja na haijaisha hata miezi mitatu, wamechapa mwendo. Hospital walipochunguzwa ikabainika kuna shida ilikuwa inajitokeza kwenye damu(Damu Kuganda). Mnaokwenda kuchanja nyie nendeni tu.
Utungaji huu, wengi wameanzisha uzushi kama huu. Mtaani kwetu hivi, kule vile. Umesikia chanjo inaweza sababisha kuganda damu unaamua kutunga "mtaani kwetu."
 
Kuna kesi kadhaa zimetokea Mtaani kwetu, walikwenda kuchanja na haijaisha hata miezi mitatu, wamechapa mwendo. Hospital walipochunguzwa ikabainika kuna shida ilikuwa inajitokeza kwenye damu(Damu Kuganda). Mnaokwenda kuchanja nyie nendeni tu.
Na visa hivyo havifuatiliwi na kutangazwa ila wenyewe wanasema ni watu wachache tu ndio wanaoganda damu, hata huku napokaa kipo kisa cha aina hiyo. Na nasikia kuna wengine wanaparalyze.
 
Kifo hakikimbiwi na wala hakina chanjo ukiona hujafa Basi haujafa kwaajili ya kinga ya chango ila haujafa kwasababu siku hazijafika.

We chanja mi sichanji
 
Kifo hakikimbiwi na wala hakina chanjo ukiona hujafa Basi haujafa kwaajili ya kinga ya chango ila haujafa kwasababu siku hazijafika
We chanja mi sichanji
Kama ni hivyo kungekuwa hakuja haja ya kuchanja chanjo zile utotoni. Wala kutumia dawa. Wala kuwa na hospitali.
 
Utungaji huu, wengi wameanzisha uzushi kama huu. Mtaani kwetu hivi, kule vile. Umesikia chanjo inaweza sababisha kuganda damu unaamua kutunga "mtaani kwetu."
Tumekuwa na Tatizo Kuu la kutaka Kusikia Unachokitaka au Kuona na Kifanywe Unachokitaka Mhusika na sio Uhalisia. Wewe ukitaka kukubali kubali, usipotaka acha. Juzi nipo ofisini, kuna jirani yangu hakuwa amefungua ofisi yake, nikampigia kumuuliza kama atakuja akaniambia hana uhakika sababu walikuwa kwenye mazishi ya jirani yao.

Picha nzima ikapatikana jana, kumbe aliyefariki aliwahi kuchanjwa! Baada ya muda maradhi yakawa yanapishana pishana hayamkauki, Jumanne hali ikawa tata akaaga dunia. Hapo Jeshi la Wokovu tena Kurasini nikakutana na same stori ukiachana na za huku mtaani kwetu. Wewe endelea kubisha, hakuna wa kubishana na wewe.
 
Na visa hivyo havifuatiliwi na kutangazwa ila wenyewe wanasema ni watu wachache tu ndio wanaoganda damu, hata huku napokaa kipo kisa cha aina hiyo. Na nasikia kuna wengine wanaparalyze.
Hizo side effects ndizo alizokuwa anazihoji Gwajiboy akaishiwa kupopolewa mawe, watu bado wanaona ni jambo dogo ila muda utasema tu. Mdudu ni kweli yupo na anaua ila hii chanjo inaua pia. Dizonga nako nasikia wameanza kukiamsha barabarani kupinga chanjo.
 
Mi nimechanja lakini kitoto changu kichanga sitaki kichanjwe! Kuna nesi hapa amenivuta sikio niwe makini.

Naona hakuna muitikio wa chanjo kwa watu wazima wanaamua kuipunguzia kwa vitoto huko leba
Mkuu unamaanisha manesi wanawachoma watoto?
 
Back
Top Bottom