#COVID19 Kuna siku Watanzania watapanga foleni za kilomita kadhaa ili kuchanja

WENGI WANAOONDOKA NI WALE WALIOCHANJA SASA KAMA KWELI UMECHANJA MZEE JIANDAE SAFARI INAKUJA
Kwa hali ninavyoiona ya hii Korona kuondoka na watu, kuna siku watanzania watapanga foleni za kilomita kadhaa ili wapate chanjo.

Nilienda kupata chanjo siku ya jumanne. Nilikuwa niko peke yangu na mtoa chanjo. Tulizungumza mambo kirefu sana. Nilikaa pale kama nusu saa hivi. Mbaya zaidi wafanyakazi wa afya wengi sana nao wanakwepa kuchanja. Jamaa fulani alinipa uchambuzi kuwa wafanyakazi wengi wa afya kinachowafanya wasichanje ni uoga wa sindano!!

Kingine nilichokiona, unapewa cheti cha mkononi na kingine unaweza download. Inaonekana kama umedhamiria kutochanja ila unataka upate cheti, unaweza 'ukachonga' na mtoa chanjo ukapata cheti.

Mbaya zaidi serikali nayo imechukulia mzaha hili suala. Gwajima, Dr anaenda kumpa Steve Nyerere ubalozi wa chanjo. Ataelimisha nini watu juu ya chanjo?

Siku inakuja watu watapanga foleni za kilomita kadhaa ili kupata chanjo
 
Back
Top Bottom