#COVID19 Tujadili na kushauri Serikali kuhusu chanjo za Covid -19 na ukusanyaji wa takwimu zinazotakiwa na WHO

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
4,954
4,326
Jana rais wetu ameagiza kuundwa task force ya watalaam kuchambua kwa makini masuala haya ya covid 19 na kuishauri serikali hatua sahihi za kuchukua. Pressing issues hapa ni hasa msimamo wetu kuhusu chanjo za covid na utoaji wa takwimu zinazohitajika WHO kila siku. Tujadili faida na hasara au mapungufu yake. Hii inaweza kusaidia task force hii kutoa ushauri mzuri kwa serikali yetu.

1. Kuhusu chanjo za covid 19:
Lengo kuu la chanjo ni kupata herd immunity ya angalao ya 60% ya population kupitia chanjo ili ku cut off transmission (Ro) ya mlipuko wa gonjwa hili. Kwa Tanzania ambayo population yake ni million 60 hii ina maana kuwa kupitia chanjo hizi inapaswa tuwe na watu wasiopungua million 36 walio na immunity against kirusi hiki cha cov -2.

Bahati mbaya kwenye field hakuna chanjo yenye 100% efficacy. Chanjo nyingi zina efficacy ya takribani 70% tu. Hii ina maana kuwa kati ya watu 100 wanaopata chanjo hizi kikamilifu (2 doses), ni watu 70 tu ndiyo miili yao inafanikiwa kujenga hiyo immunity against cov-2, hao 30 waliobaki huwa wanaambulia tupu.

Hivyo ili kupata hao watu milioni 36 wenye immunity kama chanjo yetu ina efficacy ya 70% tunahitaji kuchanja watu million 51.5 kwa mahesabu rahisi ya cross multiplication.

Kwa kuwa chanjo hizi zinahitaji dose mbili kwa kila mtu, hivyo tutahitaji doses million 102.9 kuchanja hao watu million 51.5.
Bei ya dose moja ni Tsh 35,000 (USD 15). Kwa hiyo chanjo hizo zitatugharimu Tsh 3.6 trillion. Hapo hatujajumlisha gharama za kuzisafirisha kwenye vituo mbali mbali nchi nzima, gharama za wachanjaji, gharama za utunzaji na logistics zingine. Hatutapewa bure bali tunaweza kukopeshwa kwa riba fulani. Tutapewa kiasi kidogo bure cha kuanzia - actually cha majaribio.

Kwa mchanganuo huo tu utaona kwamba kitu hiki hakiwezekani kwa nchi nyingi zetu hizi za Afrika. Itatuchukua miaka kadhaa kuchanja watu wote hao ili kupata herd immunity kupitia chanjo hizi. Hata huko kwenye nchi zilizoendelea ambazo chanjo hizi wameanza tangia mwezi January 2021 hadi sasa wengi wao hawajafikisha 20% full vaccination ya watu wao, wanategemea itawachukua mwaka mmoja kufikisha hilo lengo la herd immunity kupitia chanjo.

Zaidi ya hapo ni kwamba chanjo zinazotumia genetic engineering ya vinasaba zina changamoto zake. Haziruhusiwi kutolewa kwa wenye umri wa chini ya miaka 16. Sasa kwa nchi za Afika kundi hili la wenye umri huu ni karibu asilimia 30% ya population. Maana yake ni kuwa ukilitoa kundi hili hilo kundi linalobaki hata ukilichanja lote hutafikia hiyo 60% herd immunity inayotakiwa kukata transmission ya mlipuko. Chanjo zote isipokuwa za Uchina zinatumia tekinolojia ya genetic engineering.

Isitoshe muda wa kinga unaopatikana kupitia chanjo hizi hauzidi mwaka mmoja. Hii ina maana kwamba inabidi kila mwaka watu wachanjwe tena. Yaani zoezi hili la kuchanja ni la kudumu hadi pale itakapopatikana chanjo inayotoa permanent immunity against cov-2.

Halafu kinachochanganya vichwa ni kwamba mtu hata kama ameshapata full vaccination bado anatakiwa kuendelea kuvaa barakoa, social distancing, lockdown etc sawa na yule ambaye hajapata hizo chanjo. Na nchi nyingi ambazo zimechanja badala ya ugonjwa huu kupungua kwenye nchi hizo tumeshuhudia ukiongezeka. Kuna wimbi jipya la mlipuko kutokana na virusi hivi kubadilika badilika na hivyo kuwa na uwezekano wa kukwepa hizi chanjo.

Wanasema wamegundua kwamba virusi vya corona kutoka Tanzania vina genetical mutations za mara kumi. Wanasema hii imetokana na watanzania kutozingatia masharti ya kujikinga. Bado wanachunguza kama aina hii ya virusi vya Tanzania makali yake yamepungua au yameongezeka kutokana na hizo ten genetical mutations.

Ukweli ni kuwa makali ya gonjwa hili kwa waafrika chini ya jangwa la sahara ukitoa Afrika kusini, ni madogo sana ukilinganisha na nchi kama za ulaya, amerika na brazil. Hivyo ingalifaa tuendelee kuwa na subira kuhusu chanjo. Tujikite zaidi kwenye manunuzi ya vifaa tiba vinavyohitajika kuwatibu hao wachache wanaopata changamoto la upumuuaji. Ventilators zinunuliwe za kutosha pamoja na vifaa vy kuwakinga watoa huduma za afya zikiwemo PPE za kutosha.

2. Ukusanyaji wa takwimu zinazohitajiwa na WHO kila siku:
Takwimu hizi zimejikita kwenye upimaji (PCR testing) wa watu wengi iwezekanavyo kila siku hasa walio kwenye high transmission areas na wale waliokutana na watu wenye virusi vya corona (contact tracing).

Lengo kuu ni kuwapata watu walio na virusi hivi vya cov-2 ( wengi hawana dalili za ugonjwa) na kuwatenga (isolate or lockdown) kwa siku 14 au hadi watakapokuwa negative ili wasiambukize wenzao hasa wazee na walio kwenye high risk ya kupata ugonjwa mkali wakiambukizwa. Hivyo takwimu hizi za WHO zimejikita kwenye mkakati huu wa testing, testing, testing and isolate or lockdown. Kila nchi inapewa minimum number ya watu huko mitaani ambao inatakiwa kwenda kuwachukukua sample za njiti puani kwa ajili ya kipimo cha PCR kila siku kutoka sentinel sites mbali mbali nchi nzima. Pia kwa wale wenye dalili za ugonjwa wanaofika kwenye vituo vya tiba. Wote wenye dalili za ugonjwa na wale ambao hawana dalili ili mradi pua zao zimeonekana kuwa na antigen za cov-2 huhesabika kama wagonjwa (New cases).

Kipimo kimoja cha PCR ni sh 120,000/ Kama tunatakiwa kufanya angalao vipimo 100,000 kwa siku hii itatugharimu Tsh 12 billion. Kwa mwaka ni sawa na Tsh 4.4 trillion. Pesa hizi tunapewa kwa mkopo wenye riba.

Ukweli ni kuwa nchi nyingi hasa za Afrika zinafanya usanii tu na kutoa takwimu feki. Si kazi rahisi kusaka watu mitaani walio na coronavirus lakini ni wazima. Bila kutumia nguvu za polisi hakuna atakayekubali kuchokonolewa pua yake wakati yeye ni mzima. Na hakuna atakayekubali kuwa isolated bila nguvu za polisi. Hii kitu haiwezekani kwa mazingira yetu licha ya kuwa na gharama kubwa.

Ukweli ni kuwa nchi zilizotekeleza (kwa usanii) masharti hayo hazina uahueni wo wote wa gonjwa hili ukilinganisha na sisi.
 
Hadi sasa hizi genetically engineered chanjo hasa zinazotumia DNA viral vectors zinaonesha kuwa hatari sana kwa uhai wa binadamu hususani kuganda kwa kwa damu iliyomo kwenye ubongo (cerebral sinus thrombosis). Hadi sasa zimethibitika kusababisha mwili kutengeneza antibodies against platelets na hivyo autoimmune thrombocytopenia.

Matatizo haya ukiyapata kwenye nchi masikini kama za Africa ni 100% fatal. Hata huko kwao ni 60% to 70% fatal. Matatizo haya wanayapata hasa vijana na hasa wanawake wenye umri wa chini ya miaka 60 ambao kwa kawaida wana 99.9
% chances za ku survive gonjwa la corona wakilipata.

Chanjo zilizobainika kuwa na immeadiate side effects hizo ni AstraZeneca na Johnson & Johnson vaccine. Madhara ya muda mrefu bado tunayasubiri muda wake utakapofika. Nchi nyingi za ulaya na amerika zimesitisha chanjo hizo huku mlipuko wa covid 19 ukiongezeka. Hata huku Afika nchi kadhaa zimesitisha chanjo hizo eg Afrika kusini, DRC Cameroon nk. India, Australia nk.

Hivyo ni vyema tukaendelea kuvuta subira hadi kitakapoeleweka. After all nchi nyingi zilizokimbilia kuchanjana sana hadi sasa mlipuko wa gonjwa hili umeongezeka badala ya kupungua.

 
Huku kwetu kuwatambua (diagnose) watu wanaopta ugonjwa kama wa cerebral sinus thrombosis siyo rahisi, hatuna vifaa na ujuzi wa kutuwezesha kufanya hivyo kwenye vituo vyetu vingi vya afya. Kwanza wagonjwa wetu wengi hawaendi kutibiwa kwenye hospitali zetu ambazo gharama zake wanashindwa kuzimudu. Hata wakienda mgonjwa wa cerebral sinus thrombosis atakuwa diagnosed malaria (kwani dalili yake kubwa ni kuumwa kichwa, ikiambatana na kupoteza fahamu basi itakuwa cerebral malaria), UTI au typhoid. Marafiiki zetu wa nchi jirani wanatuambia matatizo hayo wanayapata wengi baada ya kuchanjwa ila serikali yao inayafumbia macho kuyachunguza (of course hawana uwezo wa kuyachunguza).
 
Back
Top Bottom