#COVID19 Kuna siku Watanzania watapanga foleni za kilomita kadhaa ili kuchanja

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,206
12,703
Kwa hali ninavyoiona ya hii Korona kuondoka na watu, kuna siku watanzania watapanga foleni za kilomita kadhaa ili wapate chanjo.

Nilienda kupata chanjo siku ya jumanne. Nilikuwa niko peke yangu na mtoa chanjo. Tulizungumza mambo kirefu sana. Nilikaa pale kama nusu saa hivi. Mbaya zaidi wafanyakazi wa afya wengi sana nao wanakwepa kuchanja. Jamaa fulani alinipa uchambuzi kuwa wafanyakazi wengi wa afya kinachowafanya wasichanje ni uoga wa sindano!!

Kingine nilichokiona, unapewa cheti cha mkononi na kingine unaweza download. Inaonekana kama umedhamiria kutochanja ila unataka upate cheti, unaweza 'ukachonga' na mtoa chanjo ukapata cheti.

Mbaya zaidi serikali nayo imechukulia mzaha hili suala. Gwajima, Dr anaenda kumpa Steve Nyerere ubalozi wa chanjo. Ataelimisha nini watu juu ya chanjo?

Siku inakuja watu watapanga foleni za kilomita kadhaa ili kupata chanjo
 
Mi nimechanja lakini kitoto changu kichanga sitaki kichanjwe! Kuna nesi hapa amenivuta sikio niwe makini.

Naona hakuna muitikio wa chanjo kwa watu wazima wanaamua kuipunguzia kwa vitoto huko leba
Sema kwa muda mrefu ilionekana hakuna umuhimu sana kwa watoto kuchanja sababu walionekana hawako kwenye risk. Sijui kama imebadilika. Na wanachanjaje watoto bila consent ya mzazi?
 
Nikuulize, hiyo chanjo ni kwa ajili ya variant ipi ya Corona, na kikija variant mpya je?

Nikuulize, ukishachanja, unaacha kuvaa barakoa, unaweza kujichanganya na watu, unakuwa huwezi kuambukizwa, kuambuzi wengine , kuugua na kufariki kwa Corona?

Side effects za muda mfupi, wa kati ma mida mrefu wa hizo chanjo ni zipi?
 
Variants ni nyingi. Ikitokea variants ambayo haisikii hii chanjo ya J&J ntaenda tena kuchanja. Na ntaendelea kujikinga na Corona sababu kuna variants zingine na chanjo siyo 100%
 
Maneno kama hayo ya vitisho yalikuwepo kabla hata chanjo hazijaja kwa sababu ya kutochukua tahadhari za kujikinga na corona na kutishana kwamba itafika muda kuja kushtuka itakuwa too late sijui hospitali zitajaa wagonjwa mara tutatengwa na dunia n.k, ila naona sasa kitisho kipya ni chanjo.
 
Kungekuwa hakuna haja ya kusema, "wanaangamia kwa kukosa maarifa." Ukosa maarifa ndiyo ujinga. Ujinga unaua, chukua tahadhari.
Nasema hivi tukizungumzia kifo kama kifo hakujawahi kuwa na kifo kisicho cha ujinga, vifo vyote vinatokana na ujinga fulani sidhani kama kuna kifo ambacho si cha ujinga.

Wewe unaweza kuona kufa kwa corona hali ya kuwa chanjo zipo ni ujinga ila ukafa kwa maradhi mengine ambayo ni ujinga tu ndio uliyokufanya uyapate na pengine kwa ujinga ukakosa tiba yake.
 
Maneno kama hayo ya vitisho yalikuwepo kabla hata chanjo hazijaja kwa sababu ya kutochukua tahadhari za kujikinga na corona na kutishana kwamba itafika muda kuja kushtuka itakuwa too late sijui hospitali zitajaa wagonjwa mara tutatengwa na dunia n.k, ila naona sasa kitisho kipya ni chanjo.
Watu wanakufa balaa.
 
"Ujinga unaua, chukua tahadhari."
Nakwambia hivi si ajabu hilo maana watu hawajaanza kufa leo kwa ujinga, huko hospitali kuna watu wamelazwa kwa maradhi ambayo sababu ni ujinga tu. Tunasumbuliwa na maradhi mengi sana na husababisha vifo vingi ila yote hayo sababu ni ujinga tu, kama tungejielewa hayo maradhi tusingapata na tungeepusha vifo.

Sasa mimi nakushangaa wewe unaona ujinga kwenye corona tu!
 
Mi nataka nikachanjwe but nafikiria maumivu ya hile sindano, halafu naiona kama ni ndefu Sana tofauti na sindano zingine
 
Nikuulize, hiyo chanjo ni kwa ajili ya variant ipi ya Corona, na kikija variant mpya je?

Nikuulize, ukishachanja, unaacha kuvaa barakoa, unaweza kujichanganya na watu, unakuwa huwezi kuambukizwa, kuambuzi wengine , kuugua na kufariki kwa Corona?

Side effects za muda mfupi, wa kati ma mida mrefu wa hizo chanjo ni zipi?
Ukiumwa malaria ukatibiwa na kupona huwa hutumii tena neti eh?
 
Back
Top Bottom