Kuna nini kinaendelea CCM?

Nsumba-ntale

Member
Joined
May 24, 2026
Posts
15
Reaction score
80
Inavyoonekana, ni kama vile CCM kuna ombwe la ki Uongozi.

Asha-rose Migiro hatoshi na hana sifa za kuendelea kuwa Katibu Mkuu hata kwa siku moja mbele! Ni Katibu Mkuu asiye na ushawishi wala hasikilizwi na yeyote. Yupo kimya kama vile alilazimishwa awe hapo alipo.

Mbaya zaidi, pesa za Chama zinatumiwa na wajanja waliopo Serikalini kwa maelekezo. Ki ujumla, Chama hakina pesa na ndiyo maana hata mishahara ya Watendaji na Watumishi ndani ya Chama, mishahara hawalipwi.


Namba mbili naye hayupo sawa na namba moja wake kwa sababu ya uchonganishi wa Mtendaji mkuu wa siri-kali!

Fukuto ni kubwa na la haja! Ni suala la mda tu fito zitagawanwa.
 
Nasubiri kuona moshi mweusi unafuka ndani ya chama hiki dhalimu kabisa.
 
Tulikuwepo sisi watetezi kinda kinda wa CCM mitandaoni.
Lakini baada ya Okt29 chama kinanuka uvundo mzito.
Nafikiri hata kina Asha Rose wanajionea heri kukaa kimya kuliko kutetea uozo uliopo.
 
Nani anayetakiwa kuwepo walau kwa siku moja?
Tulikuwepo sisi watetezi kinda kinda wa CCM.mitandaoni.
Lakini baada ya Okt29 chama kinanuka uvundo mcito.
Nsfikiri hata kina Asha Rose wanajionea heri kukaa kimya kuliko kutetea uozo uliopo.
Huu ndio ukweli.
 
Mimi nawaombea kwa Mungu wafilisike kabisa ili nchi yetu ipone
 
CCM Inawakati mgumu kuliko wakati wowote uliopita
wao kwa wao hawaminiani bado muda waanze kuuana wao kwa wao na chama kufutika ktk uso wa dunia
 
relax gentleman, na bado 🤣
 
 
CV yake na yaliyotokea Oct.29 vinakinzana!

Sidhani kama anamsukumo wa kukipigania chama.
 
Na iwe hivyo🙏
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…