Kuna karatasi yako moja muhimu hutaiona!

giphy.gif
 
Dunia ya makaratasi.. Ndivyo ninavyoweza kusema. Makaratasi yaitwayo nyaraka ndio yanaiongoza dunia

Makaratasi ya vibali mbalimbali
Makaratasi ya vyeti mbalimbali
Makaratasi ya pesa mbalimbali
Makaratasi ya mikataba mbalimbali
Makaratasi ya hati za kusafiria
Makaratasi ya utambuzi nknk

Tangu kuzaliwa mpaka kufa ni makaratasi ndio yanatuongoza, kuanzia nyumbani, makazini, michezoni, kwenye biashara, sanaa, ubunifu, mahusiano, viwango vya elimu nknk.! Bila makaratasi hutambuliki kwa chochote kile, huaminiki wala hujulikani.

Karatasi ndio zitakutambulisha siku na mahali pa kuzaliwa na mwaka pia
Karatasi ndio zitatambulisha viwango vyako vya elimu
Karatasi ndio zitatambulisha mahusiano yako kisheria
Makaratasi ndio yatatambulisha vitu na mali unazomiliki
Makaratasi ndio yataamua kiwango cha ukwasi ama ufukara wako

Hivyo basi daima sisi ni watu wa makaratasi na tunayatunza kweli kweli. Ni karatasi hiyo hiyo inayotengenezwa kutokana na miti ndio tunaitumia hiyo hiyo kuhimiza watu wasikate miti

Kwenye makabati yetu tunayo makaratasi mengi tu tumeyatunza vema na yakipotea tunapata tabu kweli LAKINI kuna karatasi moja tu linalokuhusu sana wewe pekeyako ambalo hutakaa ulione.. Nalo ni katarasi litakaloandikwa kuthibitisha mwisho wako.

Linaitwa HATI YA KIFO. Hili watabaki nalo utakaowaacha na ndio litakuwa MUHIMU kuliko yale yote uliyoyatunza maisha yako yote.

giphy.gif
Hata huko mbinguni nasikia kuna kitabu kimeandikwa majina yetu na vingine majina ya watu watakaoenda motoni . Karatasi kila mahala.
 
Ni zaidi ya hayo... Kuna vyeti vya vifo licha ya kuandikwa sababu za kifo lakini huongezewa alama maalum ya kimataifa (ICD)International Classification of Disease!] kutambulisha asili ya tatizo kama TB, Polio nknk na vingine hutambulisha kama ugonjwa uliomchukua marehemu ni kizalia au wa kuambukiza
Lakini kwa kesi ya corona sio coded number ni mhuriView attachment 1756296
Kwahio inamaana hati ya Mwendazake imeshawanufaisha familia
 
Dunia ya makaratasi.. Ndivyo ninavyoweza kusema. Makaratasi yaitwayo nyaraka ndio yanaiongoza dunia

Makaratasi ya vibali mbalimbali
Makaratasi ya vyeti mbalimbali
Makaratasi ya pesa mbalimbali
Makaratasi ya mikataba mbalimbali
Makaratasi ya hati za kusafiria
Makaratasi ya utambuzi nknk

Tangu kuzaliwa mpaka kufa ni makaratasi ndio yanatuongoza, kuanzia nyumbani, makazini, michezoni, kwenye biashara, sanaa, ubunifu, mahusiano, viwango vya elimu nknk.! Bila makaratasi hutambuliki kwa chochote kile, huaminiki wala hujulikani.

Karatasi ndio zitakutambulisha siku na mahali pa kuzaliwa na mwaka pia
Karatasi ndio zitatambulisha viwango vyako vya elimu
Karatasi ndio zitatambulisha mahusiano yako kisheria
Makaratasi ndio yatatambulisha vitu na mali unazomiliki
Makaratasi ndio yataamua kiwango cha ukwasi ama ufukara wako

Hivyo basi daima sisi ni watu wa makaratasi na tunayatunza kweli kweli. Ni karatasi hiyo hiyo inayotengenezwa kutokana na miti ndio tunaitumia hiyo hiyo kuhimiza watu wasikate miti

Kwenye makabati yetu tunayo makaratasi mengi tu tumeyatunza vema na yakipotea tunapata tabu kweli LAKINI kuna karatasi moja tu linalokuhusu sana wewe pekeyako ambalo hutakaa ulione.. Nalo ni katarasi litakaloandikwa kuthibitisha mwisho wako.

Linaitwa HATI YA KIFO. Hili watabaki nalo utakaowaacha na ndio litakuwa MUHIMU kuliko yale yote uliyoyatunza maisha yako yote.

giphy.gif
AMA KWA HAKIKA HAKUNA AIJUAYE KESHO NA HATA YULE MTUNZI WA KALENDA
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom