Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,633
- 697,787
Dunia ya makaratasi.. Ndivyo ninavyoweza kusema. Makaratasi yaitwayo nyaraka ndio yanaiongoza dunia
Makaratasi ya vibali mbalimbali
Makaratasi ya vyeti mbalimbali
Makaratasi ya pesa mbalimbali
Makaratasi ya mikataba mbalimbali
Makaratasi ya hati za kusafiria
Makaratasi ya utambuzi nknk
Tangu kuzaliwa mpaka kufa ni makaratasi ndio yanatuongoza, kuanzia nyumbani, makazini, michezoni, kwenye biashara, sanaa, ubunifu, mahusiano, viwango vya elimu nknk.! Bila makaratasi hutambuliki kwa chochote kile, huaminiki wala hujulikani.
Karatasi ndio zitakutambulisha siku na mahali pa kuzaliwa na mwaka pia
Karatasi ndio zitatambulisha viwango vyako vya elimu
Karatasi ndio zitatambulisha mahusiano yako kisheria
Makaratasi ndio yatatambulisha vitu na mali unazomiliki
Makaratasi ndio yataamua kiwango cha ukwasi ama ufukara wako
Hivyo basi daima sisi ni watu wa makaratasi na tunayatunza kweli kweli. Ni karatasi hiyo hiyo inayotengenezwa kutokana na miti ndio tunaitumia hiyo hiyo kuhimiza watu wasikate miti
Kwenye makabati yetu tunayo makaratasi mengi tu tumeyatunza vema na yakipotea tunapata tabu kweli LAKINI kuna karatasi moja tu linalokuhusu sana wewe pekeyako ambalo hutakaa ulione.. Nalo ni katarasi litakaloandikwa kuthibitisha mwisho wako.
Linaitwa HATI YA KIFO. Hili watabaki nalo utakaowaacha na ndio litakuwa MUHIMU kuliko yale yote uliyoyatunza maisha yako yote.