Kuna jambo lazima litafanyika hivi karibuni nchini Urusi ili kumaliza vita ya Urusi na Ukraine, na bei ya mafuta inaweza kuanguka kuliko kawaida

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Vita ya Urusi na Ukraine imeathiri karibu nchi zote duniani, na hasa upande wa mafuta. Vita hii imeleta hali ambayo haikubaliki duniani kote na ndani ya Urusi pia. Kimsingi, Putin ndio anaonwa kua chanzo cha haya yote.

Na ni wazi Putin hakutarajia kwamba hali ya vita na Ukraine ingekua kama ilivyo sasa. Kwa sasa anawaza sana jinsi ya kuepukana na aibu ya kupigwa na Ukraine. Juzi hapa alichukua hatua ya kulipiza kisasi na kupiga miji katika maeno ya raia, jambo ambalo alijua kabisa ni kosa kubwa sana katika sisa za kimataifa. Anatapatapa (desparate) na sasa kuna wasiwasi nje na ndani ya Urusi kwamba anaweza kutumia silaha za nuklia.

Mafanikio ya Ukraine yametokana na silaha sa kisasa sana tuka NATO. Ni silaha ambazo huwezi hta kukificha kifaru, na zinafanya Ukraine waone kila sehemu silaha za Urusi zilipo na kuzipiga wanavyotaka. Urusi ndio sasa wanatambua teknolojia ya NATO kwenye kuziona silaha zake iko juu sana. Kutumia vifaru kwenye vita ni sawa na kuamua kujiua! Ukraine amepiga maghala ya silaha karibu yote yanayoonekana katika sehemu zilizochukuliwa na Urusi, na lengo sasa ni kuizuia Urusi kupeleka silaha zaidi maeneo hayo, ndio maana wanaharibu madaraja.

Na juzi hapa kajaribu kujikosha na kusema nchi za Ulaya bado zinaweza kuendelea kutumia gesi ya Urusi maana kuna bomba lipo kusafirisha gesi hii kupitia Germany. Putin ameanza kulia poo lakini Wajerumani wamekataa ofa yake.

Na pia Ulaya imeamua kwamba hata vita ikiisha hawataki tena kuitegemea Urusi kwa gesi na mafuta. Hivyo hata vita ikiisha na Putin bado akawa raisi, hali ya uchumi kwa Urusi haitakuwa nzuri kwa kuwa atakuwa na mafuta na gesi kwa wingi bila kuwa na sehemu za kuyauza. Hili litaporomosha sana bei ya mafuta na gesi duniani. Saud Arabia kwa kutambua hili ameanza kujiweka karibu na upande wa Ukraine. Wamewapa USD 400 milioni kukabili athari za makombora ya Urusi kwa wananchi.

Katikati ya mafanikio ya kivita ya Ukraine, nchi hiyo na Ulaya wanatambua kwamba hata kama Ukraine wakifanikiwa kuyaondoa majeshi ya Urusi Ukraine na kurudisha maeneo yote huku Putin akiendelea kuwa Raisi wa Urusi, kuna sku atarudi tena akiwa amejiandaa vizuri zaidi na vita itakuwa mbaya zaidi. Kwa hiyo wanaona suluhisho la kudumu ni Putin kutokuwa raisi wa Urusi, eidha kwa kulazimishwa kuondoka, au ikibidi kuuwawa (assassination). Wanasema hili ndilo lilikuwa lengo la vikwazo vya uchumi kwa Urusi na matajiri wa Urusi, na lazima lifanikiwe ili amani ipatikane.

Ndani ya Urusi, kutambua kwamba kuendelea kwa Putin kuwa raisi wa Urusi ni janga litakaloendelea kuwakabili hata kama vita na Ukraine ikiisha, kumeanza kuleta vuguvugu wanalotaka mataifa ya Ulaya - Putin aondoke kwa njia moja au nyingine. Apinduliwe? Auwawe? Moja kati ya haya mawili linakuja na litaathiri sana bei ya mafuta, hasa kuitelemsha. Watch this space
 
Mataifa yameanza kujipanga upande unaoonyesha dalili za ushindi. Hzi ndizo siasa bwana. Hakuna rafiki au adui wa kudumu
 
Hii thread nitakuja kuifufua haya yatakapotokea. Kwa sasa ni wachache sana wanaweza kuchangia

1665943681569.png
 
Uchafu unaomwagwa hapo Ukraine umeshindwa kuamua mwisho wa mapambano,hata sasa wanajigeuza magaidi,wakiendelea kumtibua mwamba watakiona cha moto,endapo naye akaamua kutumia njia hizo za kigaidi 🤸🤸
 
We umemsikia nani hizi habari? Waache kutumia gesi Ili waokote kuni Kwa ajili ya kuotea moto majira ya baridi? Unawazimu bila shaka .
Wewe inaonekana upo gizani.

Mataifa ya Ulaya yanafanya kila jitihada kupata vyanzo vipta vya gas. Vita hii ikienda mpaka mwishoni mwa 2023, Urusi itashuhudia anguko kubwa la uchumi wake.

Kuna bomba la gas linajengwa toka Qatar kwenda Ulaya, toka Nigeria mpaka Ulaya. Miradi hiyo ikikamilika, Ulaya haitategemea gas ya Urusi. Pia kuna miradi kadhaa ya namna hiyo inaendelea kati ya Norway na nchi nyingine za Ulaya.

Mataifa haya ya Ulaya yanaamini sana katika akili zao kuliko mali asilia. Tulitaifisha migodi ya natural mica hapa Tanzania toka kwenye makampuni yao tukijua lazima watatupigia magoti, wakaja na synthetic mica. Hata gas isipokuwepo kabisa, mwishoni watakuja na suluhisho.
 
Watu wengi walio kwenye nchi maskini na wengine wanaochukia ubepari wameegdmea upande wa urusi, na ni kundi hilo hilo linamshabikia Rais wa Korea ya kaskazini. Hata hivyo, pamoja na madhira yaliyosababishwa na Marekani kwa nchi nyingi zilizo kinyume na msimamo wake, tunapaswa kutambua hii vita ya Russia na Ukraine, Putin ni kama yuko peke yake pamoja na ujasiri alionao. Ukraine anasaidiwa na wengi tena wazi wazi. Nchi za magharibi zinaijua urusi zaidi kuliko sisi wa mitandaoni. Kujitoa wazi wazi kuisaidia Ukraine, maana yake hazitishwi na uwezo wa urusi kama tunavyofikiri. Wako wengi wenye tekinolojia ya juu zaidi. Viinchi kama Norway unaweza kuvidharau, lakini viko mbali sana kwenye sayansi ya nyuklia. Wakati mtambo wa nyuklia unavuja huko urusi mwa miaka ya 90 waliogundua ni wasweden ndo waliwapa taarifa warusi. Pia wakati nyambizi ya kirusi iliyobeba silaha za nyuklia ilipolipuka na kuzama na baadaye kuua wanamaji wote 118. Walioweza kwenda kuifunga nyambizi hiyo ikiwa kwenye kina cha mita zaidi ya 100 ni waNorway, kumbuka warusi wenyewe walikuwa wameshindwa. Kwa hiyo, vita hii siyo nyepesi kwa urusi kama wengi wanavyofikiria. Vita inapochukua muda mrefu huharibu uchumi. Urusi inatumia gharama kubwa sana kwenye vita hii. Tena ingekuwa bora huko nyuma ikiwa imekumbatia ukomunisti, sasa hivi urusi ina uchumi wa soko huria, kama ilivyo china. Wakati huo ilikuwa siyo rahisi raia kiipinga serikali yao kwenye mission kama hizi.
 
Hii ni mada itakuja kuwa reference baada ya vita hii kuisha....mtoa mada nakupa hongera Kwa kuliona Hili
Kwa ujumla vita hivi vimeiweka mahali pabaya sana Urusi. Sasa ule udhaifu wa nguvu za kijeshi umewekwa wazi, na kuonekana kuwa kumbe Urusi si chochote.

Silaha zake nyingi za kisasa, mrusi alikuwa anaokoteza parts kadhaa toka Ulaya. Baada ya vikwazo hawezi kutengeneza silaha mpya wala kufanyia marekebisho ya zile zilizoharibika. Sasa Urusi imefikia kutumia silaha za kale, silaha za wakati wa enzi za USSR, silaha zisizo na ubora wala umakini.

Askari wa Urusi, kila mmoja analazimika kujinunulia vest ya kujikinga na risasi yeye mwenyewe. Maana yake ni kama Putin anawaambia kuwa usiponunua shauri yako, unaenda kuishia huko huko.

Putin ameamua kuwapeleka mpaka wazee wenye miaka 60 mstari wa mbele, alimradi kama una mafunzo ya kijeshi. Jana, wapiganaji wawili miongoni hawa wa kuokoteza waliamua kuwaua wenzao 11, na kujeruhi wengi kadhaa waliokuwa kwenye mafunzo, kwa risasi. Jana hiyo hiyo, bogari yao moja ya mafuta huko Ukraine imelipuka moto, ni mikasa kila siku.
 
Umenena ukweli mtupu. Urusi imeachwa nyuma sana kiteknolojia na haya mataifa ya NATO. Urusi ni kama China, zimepiga hatua lakini bado pengo la tekinolojia na maendeleo kati yao na mataifa ya Ulaya Magharibi ni kubwa.

Mtambo wa nuclear ulipovuja, Waswidi waliwwza kuziba, tena tokea angani. Teknolojia ambayo Urusi haina.

Hata kwenye vita hii, makombora mengi ya Urusi yanayoangukia maeneo ya raia siyo kwa sababu wamepanga iwe hivyo, bali ni kutokana na poor precision ya silaha zao Wenzao wa Ukraine, wakipata target, zile guided misiles, error ni 10cm.
 
Wewe inaonekana upo gizani.

Mataifa ya Ulaya yanafanya kila jitihada kupata vyanzo vipta vya gas. Vita hii ikienda mpaka mwishoni mwa 2023, Urusi itashuhudia anguko kubwa la uchumi wake.

Kuna bomba la gas linajengwa toka Qatar kwenda Ulaya, toka Nigeria mpaka Ulaya. Miradi hiyo ikikamilika, Ulaya haitategemea gas ya Urusi. Pia kuna miradi kadhaa ya namna hiyo inaendelea kati ya Norway na nchi nyingine za Ulaya.

Mataifa haya ya Ulaya yanaamini sana katika akili zao kuliko mali asilia. Tulitaifisha migodi ya natural mica hapa Tanzania toka kwenye makampuni yao tukijua lazima watatupigia magoti, wakaja na synthetic mica. Hata gas isipokuwepo kabisa, mwishoni watakuja na suluhisho.
Kumbe unaongelea habari za kusadikika, siwezi kukupinga ni ndoto zako.
 
Kwa ujumla vita hivi vimeiweka mahali pabaya sana Urusi. Sasa ule udhaifu wa nguvu za kijeshi umewekwa wazi, na kuonekana kuwa kumbe Urusi si chochote.

Silaha zake nyingi za kisasa, mrusi alikuwa anaokoteza parts kadhaa toka Ulaya. Baada ya vikwazo hawezi kutengeneza silaha mpya wala kufanyia marekebisho ya zile zilizoharibika. Sasa Urusi imefikia kutumia silaha za kale, silaha za wakati wa enzi za USSR, silaha zisizo na ubora wala umakini.

Askari wa Urusi, kila mmoja analazimika kujinunulia vest ya kujikinga na risasi yeye mwenyewe. Maana yake ni kama Putin anawaambia kuwa usiponunua shauri yako, unaenda kuishia huko huko.

Putin ameamua kuwapeleka mpaka wazee wenye miaka 60 mstari wa mbele, alimradi kama una mafunzo ya kijeshi. Jana, wapiganaji wawili miongoni hawa wa kuokoteza waliamua kuwaua wenzao 11, na kujeruhi wengi kadhaa waliokuwa kwenye mafunzo, kwa risasi. Jana hiyo hiyo, bogari yao moja ya mafuta huko Ukraine imelipuka moto, ni mikasa kila siku.
Wiki iliyopita Putin kapiga Hadi kindergarten pale Kiev yaani ni full kupagawa
 
Wewe ndo hujui.

Dunia Iko kwenye mchakato wa kuibuka Kwa pande mbili ama wee ni pro US, au Pro Urusi .

Hilo halirudi nyuma , hamna Cha Putin Kufa, Wala Bibi yake .

Wamagharibi wanataka Unipolar World ,Mfumo. Dunia ambao utaongozwa na wao.

Warusi,Uchina,India , Brazili , S.Africa, ( BRICS) Hawa wanataka multipolar world na kwakua wao ndio wenye idadi kubwa ya watu Duniani , umoja wao kama Hautakua na usaliti, basi Utakua umoja wenye nguvu Sana.

Kusema Putin Auliwe, ni sawa nakusema Xi Jinping Auliwe .

IMPOSSIBLE!!!
 
Back
Top Bottom