Wenye nguvu huiongoza dunia na kuamua namna wanavyotaka.
Ili uwe na nguvu, uheshimike na uogopeke, lazima uwe na matumizi sahihi ya akili.
Matumizi sahihi ya akili huzaa mipango sahihi ambayo humfanya binadamu acheke na Mungu.
Kwa muda mrefu sana Marekani ilijinasibu kama taifa kubwa, na hilo halipingiki. Taifa kubwa na imara linahitaji mshindani aliye imara na mkubwa pia.
Mshindani mkubwa wa Marekani na aliyewahi kumtunishia misuli na ataendelea kuwa imara dhidi ya Taifa hilo ni Urusi.
Marekani alitumia ukaribu wake na Ukraine kumdhoofisha Urusi.. lakini Urusi alisimama kidete kuhakikisha kuwa analinda hadhi yake na kuonesha uwezo wake wa vita katika dunia hii.
Urusi inapigana vita nyingi tusizoziona dhidi ya Marekani, na kwa sasa kama Marekani alivyomtumia Ukraine dhidi ya Urusi sasa huenda Urusi alimtumia Hamas kudhoofisha juhudi za Marekani kuisapoti Ukraine.
Ni kwa mipango hiyo ya wababe hao wa Dunia, kwamba hadi leo Marekani amehamisha fikra zake na pesa toka kuiwezesha Ukraine hadi Israeli. Kwa muda huu Urusi anayo kazi nyepesi sana kuitindua Ukraine atakavyo.
Ni matumaini yangu kuwa mwendelezo wa vita ya Urusi Vs Ukraine, vita ya Israel Vs Hamas zitaendelea kuzaa vita nyingi zikiwemo za kiuchumi hadi pale litakapoibuka taifa jingine litakalokuwa na nguvu sawa au zaidi ya Marekani.
Sisi tusiokuwa na matumizi sahihi ya akili tuendelee kuomba huruma za Mungu ili tusijekumbwa na mwendelezo wa vita hizo huku kwetu machakani.
Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app