Kama Israel imeshindwa vita dhidi ya Hamas, basi Urusi imeshindwa vita dhidi ya Ukraine

MTZ 255Dar

JF-Expert Member
Sep 25, 2018
1,114
3,768
Kumekuwa na maoni mbalimbali hasa ya wale wanaoongozwa na Hisia kusema kwamba Israel imeshindwa vita dhidi ya Hamas. Sababu kuu ni kwamba wanadai malengo ya Israel ya kuivamia Gaza ilikuwa kuwaokoa mateka jambo ambalo limeshindikana na hivyo Israel imeshindwa vita.

Tukienda kwa Mkitadha huo basi na Urusi imeshindwa vita dhidi ya Ukraine. Kwasababu zifuatazo:

Malengo makuu ya Urusi kuivamia Ukraine yalikuwa yafuatayo;
(i) Kuondoa wanazi ambao wanatawala pale Ukraine(Denazification)
(ii) Kuharibu Silaha zote za Ukraine na kuifanya Ukraine isiwe na uwezo tena kijeshi(Demilitarization)
(iii) Kuyakomboa majimbo yote matatu(Dotnesk, Luhansk na Kherson) kutoka kwenye utawala wa Ukraine.

Matokeo yake
(i) Lengo la kwanza la kuwaondoa wanazi pale Ukraine limefeli. Kwanini? Mwanzo wa Vita Putin na Waziri wake wa Mambo ya nje Sergei Lavrov waliweka wazi kwamba Ukraine inatawaliwa na Wanazi ambao wanachochea mauaji ya watu wanaozungumza Kirusi kule mashariki mwa Ukraine, hapa maana yake kuanzia Rais Zelensk, na Mawaziri wake walio wengi ni Manazi ambao wanatakiwa kuuawa au kuondolewa madarakani. Mpaka leo sote ni mashahidi, huu ni mwaka wa pili, hakuna kiongozi yoyote yule wa ngazi za juu wa Ukraine ambaye alishauawa hasa viongozi wa kisiasa. Kwahiyo lengo la kuwaondoa Manazi kwa mjibu wa Putin nalo limefeli pakubwa make ndio kwanza kabisa Warusi wanachukiwa zaidi nchini Ukraine na hata nchi jirani za Baltics(Estonia, Latvia na Lithuania) kuliko kabla ya vita hivyo.

(ii) Lengo la Pili la Kuharibu uwezo wa kijeshi wa Ukrane limefeli tena sana. Mwanzo wa vita Urusi iliweka ushahidi wa maneno na madai lukuki kwamba Ukraine inatumiwa na nchi za Magharibi kwa maandalizi ya kuivamia Urusi kupitia jimbo la Crimea. Wakati huo, Ukraine ilikuwa haijawhi kurusha hata jiwe moja kuelekea nchini Urusi. Sasa leo hii mwaka wa pili wa oparesheni ya kuharibu uwezo wa kijeshi wa Ukraine tunashuhudia Ukraine ikipata uwezo wa Kijeshi wa Kurusha ndege zisizo na rubani mpaka sio tu mji mkuu wa Moscow bali mpaka kwenye makazi ya rais wa Urus pale Kremlin. Tumeshuhudia manowari ya kijeshi(Flagship) ya Urusi kwa jina MOSKVA ikizamishwa na makombora ya NEPTUNE ya Ukraine. Je, Is Ukraine Stronger or weak after the War?

(iii) Lengo la tatu la Kuyateka majimbo matatu ya Ukraine nalo limefanikiwa kisiasa lakini kijeshi bado kabisa. Ukweli ni kwamba, mpaka tunavyozungumza hivi sasa, Urusi imefanikiwa kuteka vipande tu vya majimbo yafuatayo kule mashariki na kusini mwa Ukraine, kwenye mabano ni % ya eneo lilotekwa na Urusi kwenye jimbo husika.
  • Kharkiv(12%)
  • Dotnesk (70%)
  • Luhansk(85%)
  • Kherson(60%)
  • Zhaporizhia(40%)

Majimbo ya Dotnesk la Luhansk hata kabla ya vita tayari yalikuwa yanatawaliwa na waasi wa DPR na LPR ambao wanaungwa mkono na Urusi. Licha ya Urusi kutoyadhibiti majimbo hayo kijeshi kwa 100% basi iliamua kujichukulia ushindi wa kisiasa zaidi ya kuamlu upigaji wa kura ya maoni wa vipande vya majimbo hayo kujiunga na Urusi. Ikumbukwe kuwa miji mikuu ya majimbo hayo iko chini ya udhibiti wa Ukraine mpaka sasa.

Mwisho
Licha ya wengi kuwa na madai kwamba Ukraine inapata msaada wa Silaha kutoka nchi za Magharibi, lakini wakumbuke kuwa Silaha bila Molare ya vita lazima ushindwe. Licha ya kupewa silaha za kutosha na mafunzo kede wa kede, Serikali ya Ashraf Ghan wa Afghanistan iliangushwa na Wapiganaji wa Taaliban masaa 48 tu baada ya Wanajeshi wa Marekani kuondolewa nchini humo.

NB
Kama kushinda vita ni kufikia malengo ya Vita, basi Urusi na Israel wameshindwa Vita kwa Mkitadha huo.
 
Msitake kuficha ubovu ya jeshi lenu teule kwa kujificha nyuma ya mgongo wa vita ya Urusi.
Alafu Urusi hata akishindwa vita nchini Ukraine haiwezi kuwa hoja kubwa sana kwa sababu atakuwa ameshindwa kwa kupigana na jeshi lenye kila kitu ambacho jeshi linatakiwa kuwa nacho vitani.
Jeshi ambalo mpaka sasa limesha tumia silaha zenye thamani ya zaidi ya $ 200 billion kutoka katika nchi zaidi ya 50.

Wakati hilo jeshi teule linapambana na wapiganaji wasio zidi 30,000 wasio na silaha zaidi ya bunduki,Ant tank tena zisizo na nguvu sana na vijiroketi vya kutengenezwa kwa zege. Tena ambao wamezungukwa kwenye kieneo kidogo zaidi ya mara mbili ya kigamboni.

Usirudie tena kulifananisha jeshi la Urusi na hao wahuni wanao jiita jeshi maana jeshi la Urusi halijawahi kuvamia hospital na kuanza kuuwa vichanga jiti.
 
Hamas kinachowabeba ni kuwa wana mateka na wanapigana mjini
 
Kama ni hivyo basi hakuna aliyeshinda maana hata lengo la HAMAS halijafanikiwa!
 
Usirudie tena
20230316_002207.jpg
 
Unafananisha Urusi na vitu vya kijinga unazani russia ana shindwa kupiga icho ki Ikulu cha ukraine
 
Back
Top Bottom