Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,658
- 20,903
Zamani suala la kumpatia mtoto ujuzi utakao mfaa maishani lilikuwa ni jukumu la mzazi. Mzazi mvuvi alimfundisha mtoto uvuvi. Mfua chuma, mganga, mkulima, mfinyanga vyungu, mrina asali, mfugaji, mfanyabiadhara nk. Ujuzi ulitoka kwa mzazi kwenda kwa mtoto.
Ikaja hii elimu rasmi. Jukumu la kumfundisha mtoto ujuzi likawa la shule na waalimu huko. Na mbaya huu ujuzi wa shuleni mzazi ni ngumu kumrithisha mtoto. Na kibaya hata zaidi, ujuzi huu wa shuleni umeanza kutokuwa na msaada kwa alioupata. Kuajiriwa ni kazi na wala hawezi kujiajiri.
Mi naona kuna haja kubwa ya kurudi utaratibu wa kufundisha watoto ujuzi. kwa sababu wazazi wenyewe haeana ujuzi wowote wa maana, badi Badala ya mtoto kwenda twisheni ya hesabu, basi aende twisheni ya computer programming, umeme, upishi, ufundi bomba, magari, ujenzi nk nk nk.
Kwenye likizo mwezi mwezi wa sita apate kozi mbalimbali za ujuzi. Kwanza watoto wa tz ni moja ya wanaotumia muda mchache sana shuleni kwa mwaka. Wana muda mwingi nje ya shule wa kujifunza ujuzi unaoweza kuwafaa maishani.
Jambo hili linawezekana? Linafaa?