SoC04 Tumjenge kijana kiujasiriamali kwa kumpa uzoefu na ujuzi

Tanzania Tuitakayo competition threads

HARASA SANGODA

New Member
Apr 25, 2024
2
4
TUWEZESHE VIJANA KIUJASIRIAMALI KWA UZOEFU NA UJUZI

Tunaeza kufikia Tanzania tuitakayo kwa kumuezesha kijana tangu akiwa mtoto kiujasiriamali kwa uzoefu na ujuzi.
Nchi yetu ni miongoni mwa nchi zinazo jaribu kusaidia vijana kiujasiriamali kwa kuwezesha vikundi vidogo vidogo vya ujasiriamali kwa mikopo. Vikundi hivi ni vichache vinavyo weza kudumu ila vingi hukaa muda mfupi na kupotea. nyenzo Moja wapo ya kumfanya mtu afanikiwe katika jambo ni kumfundisha mbinu za kukifanya anacho taka kukifanya, kumpa mtaji mtu bila ya Elimu juu ya mtaji huo ni sawa na kumpa mbwa nyama mbichi atakula hivyo hivyo bila ya kupikwa maana Hana ujuzi wa kuandaa nyama hiyo.

TANZANIA TUITAKAYO

Serikali iweke utaratibu wa kupata mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana ikiwezekana hata somo la ujasiriamali kuanzishwa mashuleni (shule za misingi na Sekondari) kuwa wezesha vijana waliopo mashuleni kupata ujuzi juu ya ujasiriamali na si kumpatia ujuzi tu pia wapate nafasi za kuongeza uzoefu kwa kuwepo taratibu za wanafunzi kufanya ujasiriamali kwa vitendo mashuleni kukiwa na ratiba hizi itaweza kusaidia kujenga taifa lenye vijana wenye ujuzi na uzoefu wa kutosha juu ya ujasiriamali.

Vijana wanapomaliza shule za Sekondari wengi wao hawaendelei na masomo na Hawa Wana baki mitaani kwa kukosa maarifa Ambayo yange msaidia kuendeleza maisha yake taifa Lina kumbwa na changamoto la kuongezeka kwa wahuni mitaani, vibaka na madada poa. Hawa wanapigwa na maisha na mwisho wa siku wanaamua kujiingiza katika vikundi visivyo vizuri. Tutaweza kuzuia janga hili kama tutamuwezesha kijana kiujasiriamali kwa maalifa na ujuzi.

Pia kwa Tanzania tuitakayo lazima tutambue kuwa wapo watu wasio na uwezo lakini Wana vipaji mbali mbali katika sekta tofauti tofauti hivyo ni jukumu la serikali kuwa na mchango wa kumuezesha kijana waki Tanzania kutambua kipaji chake na namna ya kukitumia ili tuweze kuongeza na kukuza soko la bidhaa za kitanzania. Vijana wakitanzania Wana uwezo wa kuvumbua bidhaa mpya kwa kutumia malighafi zinazo patikana ndani ya nchi hivyo ni lazima serikali kutambua na kujikita kwenye kumsaka mtoto wa kitanzania mwenye kipaji kinacho weza saidia kuikuza Tanzania kiuchumi.

MBINU ZA KUTEKELEZA MPANGO HUU

  • Kuwa na mpango wa kusaka na kuvumbua vipaji vya wajasiriamali katika sekta mbali mbali.
  • Kuwaendeleza wajasiriamali wadogo wenye uwezo wa kuvumbua bidhaa na huduma mbali mbali.
  • Kuanzisha kufundusha somo la ujasiriamali katika shule za misingi na Sekondari.
  • Kuwepo matamasha ya ujasiriamali kwa wanafunzi ili kuweza kupata maarifa zaidi.
  • Kuwepo na siku za mashindano juu ya ujasiriamali kwa vijana.
  • Kuanzisha mifumo ya utoaji Elimu za ujasiriamali kwa vijana waliopo mitaani.
  • Kuendeleza zoezi la mikopo kwa vikundi vidogo vidogo vya ujasiriamali.
  • Kuwa tumia wafanya biashara wakubwa kama nyenzo ya kuwahamasisha vijana.
  • Kuwakutanisha vijana na watu walio fanikiwa kibiashara.

JUKUMU LA SERIKALI KWENYE KUTENGENEZA TANZANIA TUITAKAYO KWA KUMUWEZESHA KIJANA KIUJASIRIAMALI KWA UZOEFU NA UJUZI

Tuna tegemea serikali kujikita zaidi katika kuimarisha mfumo wa utoaji Elimu kwa shule za misingi kwa kuufanya mfumo wa Elimu uwe wenye manufaa kwa wahitimu wa shule za misingi na Sekondari na hili nikwa kuuweka mfumo wa Elimu utoe Elimu ya ujuzi zaidi ili KIJANA anae hitimu masomo na kushindwa kuendelea mbele anapo Rudi mitaani awe na uwezo wakujiendeleza mwenyewe kutokana na ujuzi na uzoefu alio upata akiwa shule uweze kumsaidia.

Serikali pia inajukumu la kutambua na kujari kuwa tunao vijana wenye vipaji mbali mbali na hawawezi kujiendeleza wenyewe bila ya kupata msaada kutoka juu, hivyo serikali inatakiwa kuangalia namna ya kumtambua kijana mwenye kipaji na kumsaidia kuweza kukuza kipaji chake.

KUIWEKA JAMII KATIKA KUTEKELEZA MPANGO HUU

Pia jamii lazima ihusishwe kwenye kutekeleza mpango huu ili wazazi waweze kumsaidia pia kijana mjasiliamali mwenye kipaji chake aweze kutoboa. Wazazi wapewe Elimu pia kwenye mpango wa kuijenga Tanzania tuitakayo ili kusiwe na mivutano ama vipingamizi baina ya serikali katika kutekeleza mpango wake na mzazi kwa kijana wake.

Mzazi anaweza kuwa ni kizuizi kwenye kutimiza ndoto za mtoto hasa pale anapokuwa shuleni, hili serikali pia yapaswa kulitambua maana wapo baadhi ya wazazi hasa kwa maeneo ya vijijini ambako Bado watu hawaja elimika na maeneo haya ndio yenye vipaji vingi ila vina fukiwa bila ya kujua serikali yapaswa kulitambua hili ili iweze kuona namna ya kuzisolve changamoto kama hizi.

FAIDA ZITAKAZO PATIKANA KUTOKANA NA MPANGO HUU
  1. Kujenga taifa lenye vijana wenye ujuzi na uzoefu wa kutosha juu ya ujasiriamali.
  2. Kuongeza vyanzo vya ajira za kujitegemea.
  3. Kuimarisha sekta mbali mbali ikiwemo ya uchumi.
  4. Kuongeza vyanzo vya Pato la taifa kupitia ongezeko la walipa Kodi.
  5. Kuwawezesha waliopo chini wenye vipaji mbali mbali.
Kwa kumalizia serikali na jamii kwa ujumla tuna jukumu la kuitengeneza Tanzania tuitakayo kwa kujitoa kumsaidia mtoto ama kijana wa Tanzania kutimiza ndoto zake na kujitoa kiuchumi, nimeona somo la ujasiriamali nimuhimu kwa kijana wa kitanzania kwa sababu nime kuja kulikuta chuo na nimegundua ningeli pata Elimu ya ujasiriamali tangu nilipo kuwa mtoto wallah ninge weza kupiga hatua mapema kwasababu nilikuwa napenda kufanya ujasiriamali ila nilikwama kwa kukosa maarifa ya ujasiriamali nilikuwa nikifanya ilimradi.

Serikali na jamii lazima tushikamane kumjenga Tanzania tuitakayo.

PIA TUSAKE NA KUVUMBUA VIPAJI TUJENGE MACHIPUKIZI KATIKA NYANJA MBALI MBALI.

HAMZA RASHIDI SAIDI kutoka DAR ES SALAAM.
 
Hakika umenena vema.

Taifa linainuliwa na ujasiriamali wenye tija kwa maslahi mapana ya nchi.

Kwa kuongezea tu mimi ninaonelea tuwekeze katika soko la ndani na nje. Kwa hili tujifunze kwa UCHINA na nchi nyingine za Asia.

Tuangalie tu mfano Kilimo na ufugaji. Unadhani ni nini kinawavutia wasomi kufuga kuku zaidi na sio kulima mahindi? Easy SOKO.

Ninaamini ikiwa soko litakuwa poa. Maslahi yakawa murua kabisa. Tutavutia akili kubwa kujiunga na ujasiriamali. Viwanda vidogo na vikubwa vitatamalaki.

Hivi sasa, ipo shida maana tumezidi sana ku'export' ajira zetu nje. Maslahi yamebaki kwenye siasa na uchuuzi zaidi. Vitengo husika viwajibike.

Wazo la ujasiriamali na uchumi wa nyumbani linaweza kututoa kama Taifa.
 
Hakika umenena vema.

Taifa linainuliwa na ujasiriamali wenye tija kwa maslahi mapana ya nchi.

Kwa kuongezea tu mimi ninaonelea tuwekeze katika soko la ndani na nje. Kwa hili tujifunze kwa UCHINA na nchi nyingine za Asia.

Tuangalie tu mfano Kilimo na ufugaji. Unadhani ni nini kinawavutia wasomi kufuga kuku zaidi na sio kulima mahindi? Easy SOKO.

Ninaamini ikiwa soko litakuwa poa. Maslahi yakawa murua kabisa. Tutavutia akili kubwa kujiunga na ujasiriamali. Viwanda vidogo na vikubwa vitatamalaki.

Hivi sasa, ipo shida maana tumezidi sana ku'export' ajira zetu nje. Maslahi yamebaki kwenye siasa na uchuuzi zaidi. Vitengo husika viwajibike.

Wazo la ujasiriamali na uchumi wa nyumbani linaweza kututoa kama Taifa.
Hakika
 
Back
Top Bottom