Wamuyaya
Member
- Apr 4, 2021
- 72
- 68
Ndugu zangu, nimesimama mbele yenu ili kuwashirikisha ukatili wanaofanyiwa watoto wadogo (wa kiume na kike) na wazazi/walezi wao. Wazazi na walezi wa watoto hawa naamini wanawafanyia ukatilii huu watoto wao kwa sababu ya ujinga tu.
Kwa mfano, utakuta binti mdogo anatobolewa masikio tena wakati mwingine bila ganzi kwa kisingizio kuwa wanamfanya awe mrembo. Hii naona haipo sawa, ni ukiukwaji wa haki ya mtoto. Wewe mzazi/mlezi nani amekwambia kuwa mtoto huyo anahitaji urembo huo? Kwa nini msimwache hadi atakapokuwa mtu mzima aamue yeye mwenyewe kuutafuta urembo huo? Acheni mambo ya kishamba! Binafsi nimekataa katakata kuwatoboa masikio mabinti zangu...mama yao ananilaumu na kuniona mimi ni mshamba, nimemwambia acha nibaki na ushamba wangu.
Vivyo hivyo, tupo wazazi/walezi tunaowatahiri watoto wetu wa kiume ili kudumisha mila zetu. Hebu fikiria mtoto mdogo wa miaka 12 au 15 anapelekwa porini/jando anatahiriwa bila ganzi. Huu ni ukatili na ukiukwaji wa haki ya mtoto. Kuna wazazi wengine pia tuna kawaidi ya kuwapeleka hispitali watoto wadogo kwa lengo la kuwatahiri, tukisingizia sababu za kiafya. Sina uhakika kama sababu hiyo ina mantiki yoyote...Mbona zamani hatukuwa tunatahiriwa kwa umri huo na afya zetu zilikuwa imara tu? Tuache mambo ya kishamba! Tuwape wototo haki zao, watakapokuwa watu wazima wataamua wenyewe kutahiri au kubaki na govi.
Ni jukumu la kila mtu kuhakikisha haki za watoto zinalindwa. Mashirika ya kutetea haki za binadamu pia yanapaswa kuangalia ukatili huu kwa jicho la tatu. Pia wataalam wa sheria wanaweza kukusaidia juu ya hili...Nawasilisha!