Kuna aina ya watu hawarogeki

Kuna aina ya watu hawarogeki

Hivi vitu vingi vinavyohusika na vchawi zimebaki story tuu
Hicho kitu kinachoitwa zongo hakipo?
Make duh kuna mdada ye mwanae akilia anasema kapigwa zongo, akikataa kula kapigwa zongo, ndo nikamuuliza zongo ni nini, ipo au imani tu?
 
Mshana watoto wanarogeka?
Kuna kitu nasikia kinaitwa zongo ila mi sijui kama kweli yanaexist? Hii kitu ni kweli? Ni uchawi?
Zongo ipo na inafanywa sana mkoani Tanga ni uchawi tu, tena huo haulogi mtoto tu hadi mtu mzima. Nimezaliwa Tanga na kabila ni mdigo, kijijini ilipo asili ya baba yangu watu wanaogopa kukaa kifua wazi kisa zongo.
 
Hicho kitu kinachoitwa zongo hakipo?
Make duh kuna mdada ye mwanae akilia anasema kapigwa zongo, akikataa kula kapigwa zongo, ndo nikamuuliza zongo ni nini, ipo au imani tu?
Zongo lipo na ni uchawi wa kitanga, na unakaa machoni ukipigwa zongo ama tumbo litauma sana ama utaharisha sana tiba yake ni mavumba yanaitwa makata
Zongo likipigwa kwenye chakula hakiivi hata upikeje na kikiiva hakina ladha
Huyo dada ni mwathirika tu wa mambo ya kishirikina
 
Mantiki ni kitu kingine na uwepo wake ni kitu kingine
Hakuna kilichopo bila kuwana mantiki.

Hata ukisema "Mantiki ni kitu kingine na uwepo ni kitu kingine" ushatumia mantiki.

Labda huelewi maana ya mantiki.
 
Okay sasa umeajuaje kuwa hakuna kisichorogeka?
Nina elimu kidogo juu ya hilo ndo mana nasema hvo,,ila km wewe utakua ni muislam jiulize swali kwann mtume Muhammad(S.A.W) aliweza kurogwa na ilihali ana ulinzi maalum kutoka kwa Allah.
 
Ngoja nikutesti na hii

images
hapana babu
 
Nina elimu kidogo juu ya hilo ndo mana nasema hvo,,ila km wewe utakua ni muislam jiulize swali kwann mtume Muhammad(S.A.W) aliweza kurogwa na ilihali ana ulinzi maalum kutoka kwa Allah.
Hapana mimi si Muislam
Na kama una elimu kidogo basi jitahidi usome zaidi
 
Mi sio mchawi mkuu

Umesema hakuna asierogeka, mimi naomba kurogwa, kama kuna mchawi unamjua mwambie mimi naomba kurogwa na details zangu nilitoa kwenye huu uzi hapa Naomba kurogwa hivyo unaweza kupitia ukawasaidia hao wachawi.

Uchawi/ulozi haupo duniani. Hakuna kitu kama hicho.
 
Basi elewa kurogwa kupo na ni moja kati ya mtihani na unaweza kumfika mtu yyte.
Hapana si kweli Nina uzoefu kwenye hili kielimu na kiutafiti, si kila mtu anaweza kuwa mhanga wa mchawi na ukicheki hapo nimeainisha kwa uwazi kabisa
 
Back
Top Bottom