Kumuona Daktari Tsh.10,000/=

Kumuona Daktari Tsh.10,000/=

sisi tuzidi kumuomba mungu maana likitukuta jangaaa balaaaa itabidi tuanze daftari la mchango litembezwe
Ni kweli kabisa ndugu na ndio maana Mungu anatusaidia sana maradhi yanatupitia mbali sana, afya tele. Tuzidi kumuomba sana bila kuchoka
 
Hapo Kapuku hatii mguu yaani ataambulia magamba mwili mzima kule Kijijini hii ni bajeti ya familia kabisa.
 
Na kwa Neema za muumba hiyo migonjwa mikubwa inawapata hao wenye mihela... Mlalahoi kama mimi nikipata tu maradhi ambayo tiba yake inagharimia million moja....nawaambia kabisa ndugu zangu msisumnuke na michango niacheni nife hivyo visenti vilivopo jiandaeni na kigharamia msiba.....

Sasa kama mchango wa million moja utachukua zaidi ya miezi miwili unadhani kuna uhai hapo?
 
Elfu 10 unashangaa? Nakumbuka niliumwaga nikaamua kumuona specialist na gharama kumuona elfu 40 nikasema its okay maana ni afya basi akanisikiliza then akaniandikia dawa akaniambia nikatumie baada ya week nirudi tena nilivyofika nikajua nitamuona free

lakini wakaniambia ni huduma mpya ikabidi nitoe elfu 40 tena then nikaambiwa nikapime kipimo elfu 40 halafu at the end naambiwa sina tatizo yani nilihisi kulilia hela yangu japo rohoni nashukuru sina tatizo.So hiyo ni hela ndogo kwa specialist.
 
Hivi unaelewa tofauti ya General medical doctor na Medical specialist? Kuwa specialistsiyo kitu cha mchezo kijana. Tena hiyo ni ndogo mimi ningekutoa upepo wa Tshs 50,000/= (Consultation fee).

advice he got doesn't add any value thus why he's complaining
 
Ibravo,

Utaratibu huo nilikutana nao mhimbili kuleee first track,ndo mambo ya kosti shearingi hayo mdau,zama za huduma za bure za afya aliondoka nazo nyerere in 1980s.
 
Last edited by a moderator:
hospital my ass, hapa utakua mwendo wa sangoma tu mitishamba itarudi kwenye game
 
Kwa hali ilivyo sasa ukiugua/kuuguliwa ni stress tupu sababu ya gharama na urasimu. Consultation fees zitaendelea kuongezeka kila kukicha.. Hiyo 10,000 nadhani ndo the lowest fee kumwona specialist Tz..

WAY FORWARD.....
Serikali inatakiwa kuweka utaratibu utakaowawezesha watanzania wote wawe na uwezo wa kujiunga na mfuko wa bima ya afya wa taifa..
 
10.000 wakati nimeona daktari kwa 25.000 ? Yaani akikuambia njoo siku fulani unalipa tena , hivyo hivyo
 
Hospital ya primere care Kinondoni -Namanga,Kumuona daktari ni Tsh 58000/= wakuu,nilikwenda hapo last week,
Madaktari ni Wafaransa,Wajerumani,Wakenya na Mcuba.
 
Umaskini wa mbaya, hasa wa fikra. Ulitaka cheap panga foleni haizidi 1000! udaktari ni biashara ya huduma na ni huduma pia!
 
Back
Top Bottom