Kumuona Daktari Tsh.10,000/=

Kumuona Daktari Tsh.10,000/=

Yalinikuta, niliambiwa nikamuone specialist muhimbili, nilipofika mapokezi wakanishauri nipitie FAST TRACK ili iwe rahisi kumuona daktari siku iyo iyo. Nikaripia kumuona, 10,000/- nikaelekezwa niende reception ya fast track, kufika nikakuta foleni ya FAST TRACK,

dah hamna jinsi nikakaa saa1 asubuhi nikapewa namba ya saa5 nikaenda benchi ya daktari mpaka saa 8 mchana zamu yangu , uyooo ndani...nikakuta specialist yuko na sijui Interns wa kike kama3 ivi anawafundisha kwa vitendo, yaani wanapiga story tu full time...kama dakika5 ivi nimekaa wanapiga stori then doctor akanisikiliza, tukusaidie...

nikajielezaaaaa, naye akanipa maelezooo, kama dakika3 ivi then akasema 'ndugu itabidi urudi kesho asubuhi tukucheki maana muda umeenda na nakaribia kuondoka' ...nilitaka kulia , nikatoka nje na kikadi changu mpaka receiption kuuliza nikirudi naanzia wapi, wakasema au unachukua faili pale chini unakuja folen au unakuja dirisha la FAST TRACK unalipia tena 10,000....

shenzi type naumwa niuambie ugonjwa 'daktari kasema kesho' ....nilinyoosha mpaka kwa Kahiruki Hospital, nakumbuka nilikutana na Dr Nelson msomalia na Dr Ndille wa Mikocheni, ilikuwa jumatano, nikapangiwa Operation kubwa ALHAMIS, Dr ndille alisema ndugu usiporudi ijumaa wasalimie mbinguni... usile kitu , usilambe glucose....' ijumaa nilikua wodini mapema, operation iliyochukua masaa kama5 na gharama ya milioni 2, huu ndio ulikuwa KURUDISHA UHAI WANGU

SINA CHA KUKUPA ILA DR NDILLE NA UYO MSOMALIA DR NELSON MUNGU AWABARIKI KWA KAZI ZA MIKONO YENU!!
 
Kuna hospital ya macho pale tropical house; victoria kumuona daktari TShs 80,000 sembuse huyo skin specialist wa temeke anayetoza 10000.
 
Huo ubingwa wake sijauona maana maelezo yake aliyonipa hayatoshelezi kabisa kwa yeye kuitwa bingwa,na kama yangetosheleza nisingesema chochote,mnajivisha majoho ya ubingwa kumbe bure kabisa.Huu ni wizi.

Siyo bingwa ndiyo maana ukalipa elfu 10

That's all mkuu™
 
Kila mbuzi anakula urefu wa kamba yake,bora watoze hivyo kuliko kugoma au kutupiga sindano za malimao
 
chakii kweli kabisa hiyo 10000/ bei ya kawaida sana...je angeenda ona mabingwa wakina kaushik au wakina prof matuja wa tumaini huyo kumuona ni maumivu.
 
Songea referal hospital soon itakuwa 15000/=
 
Huyo sio specialist nadhan mbona amekuchaji kiduchu ulipaswa ulipe c chini ya 50 elfu watz wataelewa tu taratibu medicine ckuhz z bussness
 
.. chakii kweli kabisa hiyo 10000/ bei ya kawaida sana...je angeenda ona mabingwa wakina kaushik au wakina prof matuja wa tumaini huyo kumuona ni maumivu

Huyu jamaa atakuwa anatania mkuu

Nilienda Regence kumuona Dr. Rugajo specialist nikaambiwa nilipe 50 elfu tena cash siyo bima.

Afya ni kitu kingine ikanibidi niingie mfukoni bila ajizi.

Namshukuru Mungu mkubwa alinihudumia vizuri.


Kumuona Specialist akiwa Private hospital is quite expensive tofauti ukionana naye akiwa government hospital kama Muhimbili ambayo itabidi iwe Fast Track la sivyo utasuburi saana!

Ndivyo nchi inavyoenda sasa.
 
Last edited by a moderator:
Gsana

Heri yako ulikuwa na milioni mbili ukaokoa maisha yako, sisi tunaotegemea Mwananyamala, Temeke, Amana tungekuwa tumeshakufa zamani.
 
Last edited by a moderator:
Sisi wa hali ya chini kwa kweli hawatutakii mema
 
.. chakii regency hosptl balaaaaa
 
Last edited by a moderator:
tanzania ni kama hatuna raisi kila mtu anafanya yake sasa kumwona daktari ni 10000 bado vipomo bado dawa kwa hali hii maskini tutakufa wengi inauma sana
 
Hawa Ma Dr wanachaji hela nyingi sana hasa kama unatumia kadi Consultation Fee ni 70,000/= kukuuliza unaumwa nini na kukuambia rudi kesho tu huu ni wizi.
 
Hawa Ma Dr wanachaji hela nyingi sana hasa kama unatumia kadi Consultation Fee ni 70,000/= kukuuliza unaumwa nini na kukuambia rudi kesho tu huu ni wizi.

matibabu ni garama sana mkuu kuanzia kumuona dokta au specialist hadi tiba, kama huna hela wakina sisi ni maumivu.......mfano kuna mzee mmoja ana kisukari lakini hana uwezo wa tiba kila akienda kwa mtaalam anaacha 50000/ bado madawa yaani mpaka mwenyewe kakata tamaa....
 
Back
Top Bottom