Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,255
- 113,669
Msimamo wangu unajulikana. Nausimamia bila chembe ya soni.
Na ndani kabisa katika kilindi cha moyo wangu, najua kuwa niko sahihi. Tena sahihi kabisa.
Lakini kuna suala moja ambalo nimeanza kuliona humu ambalo halinipendezi hata kidogo.
Hii habari ya kuuhusisha uwezo duni wa Rais Samia na wanawake wengine wote nchini!!
Nasoma soma hapa na pale pindi nipatapo wasaa wa kufanya hivyo humu [isomeke: pale mtu anaponinunulia salio la mtandao😀. Umaskini mbaya nyie watu….usikieni kwa mbali tu].
Naweza kusema mara nyingi sasa nimeona watu wakisema humu kuwa Rais Samia kathibitisha kuwa wanawake hawafai kabisa katika nyanja za uongozi…wengine wanasema kuwa Rais Samia ndo keshawaharibia fursa wanawake wenye ndoto za kupata nafasi za juu za kiuongozi, n.k.
Kuna makosa kadhaa hapo ya kimantiki ambayo yananifanya nihoji pia uwezo wa kiakili wa watu wanaoshikilia aina hiyo ya mitazamo;
1. Kushindwa kutenganisha uwezo wa mtu binafsi na badala yake kuuhusisha utovu wake wa uwezo wa kiuongozi na jinsia nzima yenye mamilioni ya watu nchini, ni uwezo duni wa kufikiri.
How come I am able to [easily] compartmentalize her serious lacking of leadership ability and separate it from her gender and therefore not lump all the women together with her? Seriously, how come?
2. Kosa jingine la kimantiki ni; Kama Rais Samia kaonyesha kuwa wanawake hawafai katika nyanja za uongozi wa juu kitaifa, ina maana wanaume ndo wanafaa?
Mpaka kufikia hivi sasa, kati ya marais 6 ambao tumewahi kuwa nao, watano ni wanaume. Mwanamke ni Samia tu.
Ina maana hao wanaume watano wote walifanya kazi maridadi sana katika vipindi vyao vya uongozi?
Walikuza GDP kwa viwango vikubwa sana? Waliboresha viwango vya maisha vya Mtanzania? Walitengeneza ajira nyingi na zilizo bora kwa Watanzania? Walifuta kabisa deni la taifa? Walikuza demokrasia? Walilinda na kutetea haki za watu?
Kama kuna kati ya hao watano wanaume ambao hawakuwa viongozi wazuri, kwa nini hatukusikia maneno ya kuwa hao ambao hawakuwa viongozi wazuri wamethibitisha kuwa wanaume hawafai kushikilia nafasi za juu za kiuongozi nchini?
Zaidi ya miaka 60 ya uhuru, Tanzania bado ni nchi maskini ya kutupwa. Tuko wa mwisho mwisho karibu kwenye kila kigezo cha ubora wa maisha.
Sehemu pekee ambayo tupo juu juu kidogo ni jeshi. Jeshi letu ni la 6 kwa ubora duniani 🤣🤣🤣.
But seriously, kama marais wanaume ambao hawakuwa na uwezo mzuri wa kiuongozi hawatumiki kuwa ndo kigezo cha kusema kwamba wanaume hawafai kuwa viongozi, kwa nini Samia ndo atumike kama kigezo cha kusema kwamba wanawake hawafai kuongoza?
Ambaye hafai ni Rais Samia. Siyo wanawake.
Deuces ✌️.