Kumtegemea mtu kama Haji Manara ili mpira wetu usonge mbele ni kujitekenya wenyewe na kisha kucheka sana

Hammyboytz

New Member
Jul 18, 2022
2
11
Kwa miaka ya hivi karibuni hapa nchi katika septa ya michezo kumekua na porojo sana kuliko uhalisia wa mwelekeo wa mchezo wetu wa mpira wa miguu tumekua, tukiweka nguvu kubwa katika kuwahamasisha washabiki na kuwaaminisha kuwa uwepo wao uwanjani na upigaji kelele ndio chanzo kutuletea ushindi kitu ambacho kwenye uhalisia wa wachezaji wetu ni uongo unaopaswa kutupiliwa mbali sana na haraka iwezekanavyo kwa mustakabali wa mpira wetu nchini.

Wasemaji au wahamasishaji kama (Haji Manara) wamekuwa wakiudhorotesha na wachezaji wetu kwa porojo zao huku tukizidi kudidimia kimpira bila kujijua

Ukweli unaofichwa nyuma ya porojo za kina manara ni ukosefu wa (quality players) katika vilabu vyetu ambao ndio wanaounda kikosi cha Taifa Stars, timu kubwa kama Simba, Yanga, na Azam zimekuwa zikiwatolea macho wachezaji wa kigeni ili kuboresha vikosi vyao ni kwanini?

Ni kwa sababu ndani hatuna wachezaji wenye viwango vya kutosha kuweza kuzipigania nembo za klabu zao, kwaiyo kabla hatujaendelea kupoteza muda zaidi ji vyema kuwekeza katika kuwapata wachezaji wenye viwango vya kutosha kuonekana kwenye ligi kuu kisha kwenye timu ya taifa lakini kwa kinachofanyika sasa hivi kuendelea kupiga porojo kwenye vyombo vya habari kuhusu hamasa ni kuendelea kuudidimiza mpira wetu, tumeona siku za hivi karibuni kuna taifa limeshiriki kwa mara ya kwanza katika michuano ya afcon na kuonesha maajabu ni kwa sababu gani? Ni kwa sababu waliweza kuwa na (quality players) hilo la kwanza lakini la pili wachezaji walijitoa kuipigania nchi yao wao wenyewe wala hawakuhitaji porojo za hamasa.

Mtu kama Manara amekua akiamini yeye ni kila kitu kwenye nchi hii katika mpira wa miguu kwa sababu tu ya porojo zake kwenye vyombo vya habari kiasi kwamba anafikia hatua ya kugombana mpaka na Rais wa shirikisho akiamini hawezi fanywa lolote. Lakini kiuhalisia kumtegemea mtu kama yeye kwenye mpira wetu ni kuendelea kuudidimiza na hatutofika popote labda yesu arudi.
 
Huyu mpuuzi amejikweza saaana sasa ni wakati wa anguko lake
IMG-20210908-WA0004.jpg
 
Simba walilijua hilo, ndomana hawakumlilia Manara kubaki Simba!
 
Huwezi kuelewa umuhimu wa Haji Manara kama hayupo kwenye timu unayoishabikia

Kwahiyo endeleeni kutulia hvyo hvyo ili sindano isije kukatika kwenye matako yenu
 
Back
Top Bottom